Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Mtaa wa Longdon kata ya Sokoni One Jijini Arusha, wamedai kuwa hawatashiriki uchaguzi wa kumchagua mwenyekiti wa eneo hilo kutokana na aliyeongoza kupata kura za maoni 189 jina lake limekatwa na aliyepata kura 36 jina kurejeshwa kama mgombea kupitia chamba hicho.
Inaelezwa kuwa katika matokeo ya kura za maoni ndani ya chama hicho ndugu Ibrahimu Mkurunzi ambaye alikuwa anatetea kiti chake amepata kura 189 na Jeradi Saitoti amepata kura 36.
Chanzo: Gadi TV