Si lazima ulimie mkonge mkoa wa Tanga. Labda kama unaishi huko. Ila mkonge unakubali mikoa mingi sana Tanzania. Pwani, Morogoro, Singida, Kilimanjaro na mikoa mingi ya kanda ya ziwa. Angalia wewe upo karibu na wapi, udongo kama unafaa. Then ingia shambani.
Kama unafikiria kulima eka 1 ya mkonge ili ikunyanyue kiuchumi acha. Hiyo hela na muda wako kafanyie mambo mengine. Kwa ambae yupo Morogoro mjini aende pale shamba la CENTRAL maeneo ya Mkambarani, au nenda Mlingano Tanga. Ukaone huduma inayohitaji mkonge na ulinganishe kama kulima ekari moja is worth the hustle.
Kulima eka 1 ya mkonge itakupa hela ya uhakika ya kula tu. Kuna gharama nyingi sana zipo ndani ya kuzalisha mkonge mpaka upate nyuzi zile ili uuze.
Kulipa wakataji
Usafiri wa kutoa mzigo shambani
Gharama za mwenye mashine
Gharama za wafanyakazi
Chakula na maji
Ushuru
Mafuta(diesel)
Gharama za usafiri kumpelekea mnunuzi kama ana stoo mbali na site ya kuzalisha.
Jinsi gharama za maisha zinavyozidi kupanda na ndio gharama za uzalishaji zinapanda pia.
Wanunuzi wa mkonge wengi ni wakandamizaji sana. Hasa hawa wanunuzi wanaonunua kwa wazalishaji wanaotumia mashine za spadle. Pale Morogoro mjini wananua sh 1800 kwa kilo hiyo ni bei ya leo tarehe 03/07/2023. Utalipia usafiri hadi stoo kwa mnunuzi, mzigo ukifika ataukagua. Hata uwe msafi vipi, huwa wengi wao hawakosi sababu ili ashushe bei zaidi.
Lima angalau ekari 20 na kuendelea. Ili uvune mzigo mkubwa na uzalishe kilo nyingi, endapo ikitokea changamoto, wingi wa kilo zako ulizozalisha bado utakutunza usipate hasara. Kilimo cha mkonge ni uwekezaji mkubwa sana ukifanya kwa ukubwa wake.
Ingia kwa pupa kwenye mkonge utapigwa za uso kama vanilla au matikiti afu uanze kulaumu watu. Nipo kwenye mkonge tangu 2014, nimeshapigwa humo, nimeshalaani, kutukana na kufurahi pia.
NB: Fanya utafiti wa kutosha kabla ya kuingia shambani. Ukitaka shamba ninalo pori Maramba nauza laki 3 na nusu kwa eka 1