Msingi wangu ukubwa wake ni 16x12 waliujenga kwa siku mbili,siku ya pili walimalizia kwa kusuka nondo na kumwaga zege.....!!!kuwalipa kwa siku kwangu ilikuwa rahisi kwa sababu nilikuwa nalipa idadi ya mafundi na vibarua,fundi mmoja nilikuwa namlipa elfu 20 na kibarua elfu 10,fundi mkuu nilikuwa namlipa elfu 40,labda na gharama za maji kwa sababu sikuwa nimevuta maji,ambapo kwa pipa nililipa 2500....!!!boma hadi muda huh llimekwisha,linta ndo naweka mwezi ujao Mungu akinijalia uzima na kama mipango yangu itaenda vzr.....!!swala la msingi hapa,anza ujenzi,taratibu utaendelea kutokana na unavyopata pesa.......!!plani yangu ya kuezeka ni mwezi wa tano mwakani,lakini muda huu nipo site ya rafiki yangu wapo wanaezeka,bati alininua ijumaa za alaf,bati 130 kila bati sh 24 elfu,mano za kenchi amenunua jana mbao 310 kwa shilingi 2100000/- fundi wa kufunga kenchi na kuezeka analipwa sh 700000/.....