Makadirio ya Gharama ya ujenzi wa nyumba ya vyumba vitatu 3

Makadirio ya Gharama ya ujenzi wa nyumba ya vyumba vitatu 3

Vizuri, umetembea vizuri sana. Na watu wasichofahamu ni kuwa. Ukijenga nyumba kwa gharama na bei za kupigwa,ikija kutokea unataka say kuiuza ama kuikopea, utapewa valuation ndogo sana tofauti na gharama yako ulojengea. But hutokuwa nawa kumlaumu, maana makosa utakuwa umeyafanya wewe katika usimamizi wa ujenzi.

Kingine, mafundi wengi siku hizi wanawapiga wateja wao katika material. Wameachana na njia ya kizamani ya over pricing ya material. Hii ilikuwa say bati ni sh 20000, anawambia 21000 but siku hizi say zinahitajika bati 100, wewe unaweza ambiwa zinahitajika bati 130, automaticaly hapo bei ya bati 30 utakuwa umepigwa.

Halafu hizo bati za ALAF ni za ukubwa gani kwa hiyo bei.?
Ni zile za migongo midogo,za rangi ya blue,mita 3 x1
 
Kweli mkuu,mimi nina nyumba yangu mchakato wake nilianza january mwaka huu...ina master moja,Bedroom tatu,sitting room,dining,kitchen,choo na bafu.Nimefyatua tofari za Block 4000 mimi mwenyewe....gharama yake nimekokotoa kwa kila tofari ni km 770....nilinunua cement kwa 19500 kwa mfuko.Hii ni phase one...so next month nategemea ujenzi uanze mwanzo mpala mwisho maana nimebakiza Nondo tu...na kokoto...Kupaua bado sana bajeti sijaiweka
duuh wap huko mfuko wa cement unauzwa kabei hyo
 
Hujakosea kabisaa mkuu upo sahihi na ndio maana akafanya hivyo maana ujenzi sipo vizuri na hasaa nilimbana kwenye vifaaa aliweka idadi ten vyote nikaenda kununua mwenyewe nikawa nime save kama 3M hivi....sasa naona hakupendaaa imenibidi nikae kwanza nifatilie na kuulizia zaidi....

Kama unajipenda na kutaka jengo bora usimtumie tena huyo, anatakupiga kwenye kumalizia nyumba vibaya ambabapo haitadumu au utapata shida kurudia rudia.

Pia jitahidi sana kuonyesha unajua na ile ya kama unataka kusikia ya mwingine.

Hata vya kuongea unatoa humu kujionyesha nawe upo unayajua kumbe ujanja tu muhimu wasikulize
 
Labour charge haiwezi fika million 7 kwa msingi peke yake. Hata ujenzi wa nyumba nzima sidhani kama unafika huko.

Kiufupi gharama za labor charge kwa fundi bati, ujenzi, umeme, bomba haiwezi fika hiyo gharama kikawaida. Iweje wewe msingi tuu ulipe hiyo pesa.? Kukusaidia tuu hapo nafahamu gharama ujenzi kwa tofali moja huwa wanachaji sh 250 mpaka 350. Hii ni kwa dar es salaam. Sasa kwa kesi ya ujenzi wa msingi ongezea gharama za wachimbaji wa msingi na settings za msingi.

Simply hapo unaelekea kupigwa

Sawa sawa kiongozi hapo nimekueleaa vizuri kabisaa na asante sana na nashukuru sanaa tena sanaaa na ndio hapo na mimi nilikuwa sijaelewa hasa inakuwaje imekuwa gharama hizo zote kwa ujumla nilijaribu kumgusia kumlipa kwa tofali akasema kwamba hapo anajenga tu tofali ila kuna kazi zingine nyingi sana kama kuweka mawe,mchanga,kushindilia na kila kitu so hapo akasema haitowezekana....so hapo itabidi niongee nae tu tufanye kazi kwa kujenga kila tofali maana nimeshanunua tofsli 2000 za msingi tayari....so hapo anawwza kufanya kwa kila tofali lets say 450 plus kuchimba kumwaga mchanga mawe na mpaka kuweka jamvi.....
 
Kama unajipenda na kutaka jengo bora usimtumie tena huyo, anatakupiga kwenye kumalizia nyumba vibaya ambabapo haitadumu au utapata shida kurudia rudia.

Pia jitahidi sana kuonyesha unajua na ile ya kama unataka kusikia ya mwingine.

Hata vya kuongea unatoa humu kujionyesha nawe upo unayajua kumbe ujanja tu muhimu wasikulize

Aiseeeee wakuuu mmenifungua kwa mambo mengi sanaa na nashukuru sanaa tena sanaaa sio kidogo asante sanaaa na ndio nilikuwa makini sanaaa toka mwanzoni kabisaaaaa na ikabidi nimekuja kuomba ushauri humu ndani so nashukuru na asante sanaa kwa mawazo mazuri.....

Na itabidi nitafute mwingine tu maana hamna tena fundi pale zaidi ya tamaaaa
 
Haya wakuu wa JF kama mna mafundi wazuri na waaminifu tafadhali wekeni number zako au nitumieni number zako tafadhali me hasaaa nilikuwa nataka kujenga msingi mpaka kupiga jamvi then nitaendelea pole pole na ikiwezekana nianze kupandisha pole pole sasa msaada unahitajika na eneo ni kigamboni.......
 
Kuwa makini na wa humu as watakuwa wameshakusoma unakotokea na kupiga dili na fundi hata aongeze chao.

Jaribu kwanza kuuliza au tembelea maeneo hayo unakojenga angalia kazi zinazokuvutia ongea na mwenyekiti wa serikali za mitaa etc wanawajuaga sana hata ambao wanaletewa malalamiko na matapeli.

pia watu wa karibu nawe ndugu na marafiki, utashangaa unao wajuao bali hujasema wakakupatia unayohitaji hata kutoka kwa watu wanaowafahamu wanajua unachotafuta.
 
Pigia garama ya boma kwanza... Yaani kiwanja, msingi, tofali , renta , misumali, cement, mchanga mbao , mabati na milango . kisha finishing utaenda nayo taratibu ukiwa usha hamia au bado .
 
Ndiyo inaweza fanyiwa marekebisho ila yasiwe makubwa sana!

jamani naomba kujuzwa kwa wale wachora ramani na wajenzi.
je inawezekana kuibadirisha ramani kwa nyumba iliyojengwa ikafika nusu halafu ikabadirishwa kwa kutumia msingi uleule??
 
nami pia nipeni gharama ya kujenga nyumba mpaka kwenye linta tofali nishapiga ukubwa wa nyumba ni 13mmx15mm ya vyumba 4 eneo lilipo ni tanga mjini.

Millioni 15 - 20

Sio 13mmx15mm, ni 13m by 15m
Mzingo wa nyumba yako ni 13+15+13+15= 56m gawanya kwa 0.45 hapo utapata ni tofali ngapi zinafanya mzunguko mmoja. Ukizidisha na kozi za nyumba utajua unahitaji tofali ngapi. Hilo ni kadirio la juu kabisa na wala usiongeze hata tofali moja kwani wakati wa ujenzi kuna milango na madirisha.
 
Habarini wakuu, mi ni technician wa civil, kwa yeyote aliye serious kufanyiwa tathimini au ushauri anaweza kuni pm!!
 
Mzingo wa nyumba yako ni 13+15+13+15= 56m gawanya kwa 0.45 hapo utapata ni tofali ngapi zinafanya mzunguko mmoja. Ukizidisha na kozi za nyumba utajua unahitaji tofali ngapi. Hilo ni kadirio la juu kabisa na wala usiongeze hata tofali moja kwani wakati wa ujenzi kuna milango na madirisha.

Mkuu kwa hesabu hizi si ni kama anajenga darasa kwa hiyo akipiga hiyo hesabu anapata idadi ya tofali za kumaliza darasa
 
Haya wakuu wa JF kama mna mafundi wazuri na waaminifu tafadhali wekeni number zako au nitumieni number zako tafadhali me hasaaa nilikuwa nataka kujenga msingi mpaka kupiga jamvi then nitaendelea pole pole na ikiwezekana nianze kupandisha pole pole sasa msaada unahitajika na eneo ni kigamboni.......

Kuna gtoup moja facebook linaitwa "Ujenzi zone"

Kuna mengi, maswali na majibu, ushauri etc

Itakupa moyo pia
 
Kuna gtoup moja facebook linaitwa "Ujenzi zone"

Kuna mengi, maswali na majibu, ushauri etc

Itakupa moyo pia

Hilo group nimeona humo ndani kuna kila kitu naonaaaa....mafundi umeme kil kitu nashukuru sanaa hatua kwa hatua tutafila tu bila kujali au kukata tamaaaa.....asante sana cocochanel
 
Back
Top Bottom