Makadirio ya Gharama ya ujenzi wa nyumba ya vyumba vitatu 3

Makadirio ya Gharama ya ujenzi wa nyumba ya vyumba vitatu 3

Upo sahihi,mi yangu ina vyumba 3 pamoja na study room,msingi umenigharimu takribani 3.5m,mawe peke trip 20 zikinigharimu 1.1m,hadi muda huu ambapo sijafunga linta naweza kuwa nimetumia zaidi ya 7m(japo huwa situnzi kumbukumbu za gharama za kila siku..)

Sawa sawa mkuu na ujenzi wako unafanyia dar ay mkoani??nadhani kama wadau walivyosema inategemeana na eneo ulipo.....na mafundi wako wazuri lakini??
 
Sawa sawa kiongozi na ujenzi wako unafanyia dar au unafanyia wapi hasaaa??
 
Ivi maelewano yakumlipa fundi uwa yapoje unamlipa kwa kupandisha tofar yaan idad ya tofal ama ??

Ukisema umlipe kwa tofali huwa hawataki maana wanaona kama unawaibia ila wenyewe wanataka maelewano sema sina utaalam sanaaaaaa upande wa malipo wengine wanafanyeje
 
Nina uzoefu wa ujenzi wa Dom, Dar, AR na Rock City

On average ukiwa na 20Mil unaweza jenga boma plus bati, ukihitaji msauz ongeza hapo 5M (total 25M),
ukitaka kuanza ishi kwenye hiyo nyumba unahitaji at least 15M ili uwe na nyumba basi kabisa, ila ukihitaji makorombwezo ya ziada ongeza another 10M
SO generally ukiwa na 40M unajenga standard house, ila ukiamua kuweke bati la dizain ya ajabu ajabu, madirisha yenye gril za kumeta meta, aluminium ya inch 10, spanish tiles, milango ya mninga, hot water system, makabati ya ukweli ya jikon, makabati ya nguo katika vyumba vyoote, .......... nyumba hiyohiyo inaweza isipungue 70M
 
sabau huyo umemuonyesha haujui kitu juu ya ujenzi, na hauna wakukushauri au kukuanbia ukweli.

Nakushauri ubute subira kupata info zaidi na labda hata mjenzi mzuri, muhimu sana hii kitu ya kuuliza watu wa karibu nawe. Ili wakupe na changamoto na ushauri, hata kukuambia mtu wa kukujengea ambae wameshamtumia.

Hujakosea kabisaa mkuu upo sahihi na ndio maana akafanya hivyo maana ujenzi sipo vizuri na hasaa nilimbana kwenye vifaaa aliweka idadi ten vyote nikaenda kununua mwenyewe nikawa nime save kama 3M hivi....sasa naona hakupendaaa imenibidi nikae kwanza nifatilie na kuulizia zaidi....
 
Isije ikawa ndo kutaka kufaham ID zenu!inamaana unaishi China?wabongo kwakuzubaa mko Ovyo sana!;!
 
Habarini wakuu, naomba kama kuna mwenye uzoefu anipe makadirio ya gharama ya ujenzi wa nyumba ya vyumba vi 3 (chumba kimoja self na viwili vya kawaida), sitting, dinning, jiko, (choo na bafu public). Nataka kutumia matofali ya kuchoma ambapo tofali moja linauzwa sh 120. Msingi utatumia matofali ya block. Heshima kwenu.
Huwezi kuongelea gharama za Ujenzi bila kuwa na ramani ya nyumba husika. Kwanza ramani pili gharama.
 
Sawa sawa mkuu na ujenzi wako unafanyia dar ay mkoani??nadhani kama wadau walivyosema inategemeana na eneo ulipo.....na mafundi wako wazuri lakini??
Mafundi wapo vzr,na huwa nawalipa kwa siku,material zote nanunua mwenyewe......!!kwe linta ambayo natarajia kufunga mwezi ujao ndo nitawalipa kwa jimla........!!!
 
Mafundi wapo vzr,na huwa nawalipa kwa siku,material zote nanunua mwenyewe......!!kwe linta ambayo natarajia kufunga mwezi ujao ndo nitawalipa kwa jimla........!!!

Sawa sawa hapo nimeelewa sasa.....nashukuru sana kiongozi na mfano ulivyoanza na msingi peke yake walichukua mda gani??na je kuwalipa kwa siku sio gharama sanaaa??na upande wa malipo unakubaliana na fundi wote au mkubwa wao??material na mimi nimenunua mwenyewe......
 
Msingi wangu ukubwa wake ni 16x12 waliujenga kwa siku mbili,siku ya pili walimalizia kwa kusuka nondo na kumwaga zege.....!!!kuwalipa kwa siku kwangu ilikuwa rahisi kwa sababu nilikuwa nalipa idadi ya mafundi na vibarua,fundi mmoja nilikuwa namlipa elfu 20 na kibarua elfu 10,fundi mkuu nilikuwa namlipa elfu 40,labda na gharama za maji kwa sababu sikuwa nimevuta maji,ambapo kwa pipa nililipa 2500....!!!boma hadi muda huh llimekwisha,linta ndo naweka mwezi ujao Mungu akinijalia uzima na kama mipango yangu itaenda vzr.....!!swala la msingi hapa,anza ujenzi,taratibu utaendelea kutokana na unavyopata pesa.......!!plani yangu ya kuezeka ni mwezi wa tano mwakani,lakini muda huu nipo site ya rafiki yangu wapo wanaezeka,bati alininua ijumaa za alaf,bati 130 kila bati sh 24 elfu,mano za kenchi amenunua jana mbao 310 kwa shilingi 2100000/- fundi wa kufunga kenchi na kuezeka analipwa sh 700000/.....
 
Hapo naongelea tu labour mkuu vifaa tukiweka pembeni hela ya fundi peke yake inaweza kufikia hiyo hela??

Labour charge haiwezi fika million 7 kwa msingi peke yake. Hata ujenzi wa nyumba nzima sidhani kama unafika huko.

Kiufupi gharama za labor charge kwa fundi bati, ujenzi, umeme, bomba haiwezi fika hiyo gharama kikawaida. Iweje wewe msingi tuu ulipe hiyo pesa.? Kukusaidia tuu hapo nafahamu gharama ujenzi kwa tofali moja huwa wanachaji sh 250 mpaka 350. Hii ni kwa dar es salaam. Sasa kwa kesi ya ujenzi wa msingi ongezea gharama za wachimbaji wa msingi na settings za msingi.

Simply hapo unaelekea kupigwa
 
Msingi wangu ukubwa wake ni 16x12 waliujenga kwa siku mbili,siku ya pili walimalizia kwa kusuka nondo na kumwaga zege.....!!!kuwalipa kwa siku kwangu ilikuwa rahisi kwa sababu nilikuwa nalipa idadi ya mafundi na vibarua,fundi mmoja nilikuwa namlipa elfu 20 na kibarua elfu 10,fundi mkuu nilikuwa namlipa elfu 40,labda na gharama za maji kwa sababu sikuwa nimevuta maji,ambapo kwa pipa nililipa 2500....!!!boma hadi muda huh llimekwisha,linta ndo naweka mwezi ujao Mungu akinijalia uzima na kama mipango yangu itaenda vzr.....!!swala la msingi hapa,anza ujenzi,taratibu utaendelea kutokana na unavyopata pesa.......!!plani yangu ya kuezeka ni mwezi wa tano mwakani,lakini muda huu nipo site ya rafiki yangu wapo wanaezeka,bati alininua ijumaa za alaf,bati 130 kila bati sh 24 elfu,mano za kenchi amenunua jana mbao 310 kwa shilingi 2100000/- fundi wa kufunga kenchi na kuezeka analipwa sh 700000/.....

Vizuri, umetembea vizuri sana. Na watu wasichofahamu ni kuwa. Ukijenga nyumba kwa gharama na bei za kupigwa,ikija kutokea unataka say kuiuza ama kuikopea, utapewa valuation ndogo sana tofauti na gharama yako ulojengea. But hutokuwa nawa kumlaumu, maana makosa utakuwa umeyafanya wewe katika usimamizi wa ujenzi.

Kingine, mafundi wengi siku hizi wanawapiga wateja wao katika material. Wameachana na njia ya kizamani ya over pricing ya material. Hii ilikuwa say bati ni sh 20000, anawambia 21000 but siku hizi say zinahitajika bati 100, wewe unaweza ambiwa zinahitajika bati 130, automaticaly hapo bei ya bati 30 utakuwa umepigwa.

Halafu hizo bati za ALAF ni za ukubwa gani kwa hiyo bei.?
 
For real maelezo yko ni finyu kiasi cha mtu kushindwa kukupa exactly cost ya huo mjengo wako labda ungesema mahali ulipo, finishing ya hiyo nyumba na ufafanuz zaidi, lakn kwa ujumla km unataka iwe bora na ya kuvutia km materials yanapatkana kirahc andaa at least 25ml ila ya kawaida tu hata 12ml inatosha (Provided kiwanja unacho maana kinaweza kuwa ghari kushinda gharama za ujenzi!!)
Acha utani bwana. Vyumba vitatu vya kulala pamoja na vyumba vingine vya lazima milioni 25? Hata 12? Hata kama hajasema anajenga wapi kwa ukubwa wa nyumba ya vyumba vitatu matofali ya kujengea msingi, nondo, kokoto, simenti, mchanga na labour havipungui robo ya hiyo milioni 25, bado kuta, linter, mbao,bati, mfumo wa maji taka, plasta, nyaya, ceiling, milango, madirisha - - - - - - - labda kama vifaa anapewa na baba mdogo.
 
Back
Top Bottom