Makadirio ya kodi

Makadirio ya kodi

Mkuu

Umekokotoa vizuri sana, sasa hapo faida ya mfanyabiashara ndio imepigiwa hesabu au ni mtaji? Vip kuhusu matumizi na kodi ya pango, hata kama faida yote kwa mwaka ni 10% ya mauzo basi utakuwa unaifanyia kazi TRA, kodi kubwa sana hiyo
Unfortunately kwa individual, tax inakua kwenye sales.
Ukihamia kwenye entity ndio kuna kuondoa matumizi, cost, kodi ya pango na kila kitu.
Na hapa utajikadiria mwenyewe kwenye mfumo wa e-filing.
Ila kuna mengi ya kudeal nayo hapa.
Mhasibu, audit firm, kuandaa vitabu, proof za kila cost
 
Unfortunately kwa individual, tax inakua kwenye sales.
Ukihamia kwenye entity ndio kuna kuondoa matumizi, cost, kodi ya pango na kila kitu.
Na hapa utajikadiria mwenyewe kwenye mfumo wa e-filing.
Ila kuna mengi ya kudeal nayo hapa.
Mhasibu, audit firm, kuandaa vitabu, proof za kila cost
Mhasibu waweza kuwa mwenyewe kwa kutumia book keeping apps

Au daftari

Usisahau kutunza risiti, kuzitoa kopi, na risiti ziwe na TIN yako
 
Mimi nahitaji kueleweshwa jambo....

Kwanini TRA wanahesabu mtaji/mauzo ya siku na isiwe faida ya siku?

Wananichosha TRA....

Huduma zao sio rafiki hasa kwa tabaka la chini....
Zamani nilikuwa sijui kwann wafanyabiashara wanakimbia kodi
 
For that case
Kodi yake ni 3.5% of 55,440,000 sawa na 1,940,400

Tofauti ya laki 3 ni kubwa sana.
Kodi aliyokadiliwa ni sahihi hapo hujaweka kodi ya pango, ukifata sheria za kodi hiyo kodi ni sahihi kikubwa apunguze kutoa risiti .kodi ya pango inahesabiwa kwa mfanyabiashara pia
 
Ngozi nyeusi tuna hizo changamoto, anajua unanufaika kwa hiyo anataka akudidimize.
Tumia 'auditing firm' wakusaidie kukufanyia huo mchakato badala ya kufanya wewe; utawalipa.
Tatizo hao audit firm gharama zao zipo juu mwisho wa siku utafika huko nitafute PM tuzungumze nikupe njia rahisi.
 
Back
Top Bottom