SoC04 Makala juu ya namna Tanzania inavyoweza kutatua changamoto mama katika sekta ya uvuvi nchini

SoC04 Makala juu ya namna Tanzania inavyoweza kutatua changamoto mama katika sekta ya uvuvi nchini

Tanzania Tuitakayo competition threads

piusluckness

New Member
Joined
May 31, 2024
Posts
4
Reaction score
1
Tanzania kama nchi inayoendelea kiuchumi, sekta ya uvuvi ni miongoni mwa sekta muhimu inayochangia ustawi na ukuaji wa pato la Taifa, ikiwa ni sekta inayotoa ajira nyingi rasmi na zisizo rasmi kwa wazawa ikiongozwa na sekta ya kilimo. Na Tanzania kama nchi Chini ya mifumo yake tendaji, imekua ikichukua na kufanya jitihada mbalimbali ili kuboresha na kuongeza ustawi katika sekta ya uvuvi. Ikiwemo utungaji wa sera, ufanyikaji wa Tafiti mbalimbali na uundwaji wa Taasisi za uvuvi kama TAFIRI na FETA. Lakini pia ushirikishwaji wa Taasisi binafsi katika utekelezwaji wa miradi mbalimbali ndani ya sekta ya uvuvi.

Pamoja na jitihada mbalimbali ambazo zimechukuliwa bado sekta ya uvuvi ukuaji wake umekua wa kudorola na kutoridhisha kitaifa na hasa kimataifa.Sekta hii imekua ikikabiriwa na changamoto nyingi kitaifa na kimataifa, pamoja na uwepo wa changamoto mbalimbali kumekua na changamoto kuu ambazo ni UWEPO NA UTUMIAJI WA VIFAA DUNI, UHIFADHI USIORIDHISHA na changamoto ya MASOKO kitaifa na kimataifa. Makala hii inalengo la kutoa mawazo bunifu kwa namna Tanzania inaweza kusuluhu changamoto kuu tajwa ili kuweza kusogea mbele katika sekta ya uvuvi kitaifa na kimataifa.

1. changamoto ya uwepo na utumiaji wa vifaa duni katika shughuli za uvuvi nchini Tanzania. Kwa asilimia kubwa vifaa vinavyotumika katika shughuli za kiuvuvi ni vifaa asili ambavyo kiwango chake ni cha chini, mfano Neti, ndoano na maboti asili ambayo bado uwezo wake ni mdogo. Japokua serikali inaendelea kuongeza vifaa wezeshi lakini bado hafikidhi mahitaji kulingana na matakwa ya watumiaji, na hii inapelekea wavuvi wengi kutumia njia batili kama baruti ili kuweza kuvuna samaki wengi zaidi. Na ili kupambana na changamoto hii Tanzania inapaswa kufanya yafuatayo

i) Tanzania inapaswa kufanya marekebisho ya kibajeti, kwa kuongeza asilimia za uwekezaji wa ki nchi katika manunuzi ya vifaa endani na yakinifu kwa kushirikiana na nchi bora kiuvuvi kama China na Madagaska ili kuweza kuongeza kasi ya uvunaji bora wa samaki katika maziwa, mito na mabwawa na kupitia hii itafungua milango bora ya uwekezaji ambapo nchi itapata fursa ya kufanya namna mbalimbali ikiwemo kutumia mifumo ya kugawana gharama na wawekezaji wasio wa kiserikali ili kuweza kusukuma maendeleo ya sekta hii ya uvuvi, mfano mzuri ni uingizwaji wa maboti ya kisasa yanayoendana na asili ya maeneo yetu ya uvuvi.

ii) Tanzania inapaswa kuhakikisha inawajengea uwezo makini wavuvi ambao ni wazawa juu ya matumizi na faida ya teknolojia ya kiuvuvi nchini na kimataifa. Utumiaji wa mitambo ya kiteknolojia ya uvuvi bado ni changamoto kubwa kwa wazawa wengi, na hii inapelekea baadhi kushikilia njia za kiasili kwa kuogopa kukabiliana na mabadiliko. Kama nchi inawajibu wa kuandaa mafunzo chini ya taasisi zake yaani TAFIRI na FETA, Taasisi hizi zinapaswa kuwajibika kujenga uwezo na kuondoa hali za uoga kwa wazawa hasa wenye elimu duni na wasomi ambao hawakupata fursa ya kujengwa zaidi. Mfano nchi inaweza kutoa elimu za makundi katika maeneo husika na kuonesha mfano wa nchi zinazo nufaika kwa matumizi ya teknolojia katika uvuvi. na hii itaongeza ari ya kuchangamkia mabadiliko bila uoga.

iii) Pia Tanzania inapaswa kuhakikisha weledi katika matumizi ya vifaa hivyo vya kiteknolojia kwa kufanya usimamizi na uchunguzi ili kuhakikisha matokeo bora katika sekta ya uvuvi. Ikiwemo kuandikwa kwa taarifa juu ya mendeleo katika miradi husika ya uvuvi. Na hii inapaswa kusimamiwa na Taasisi ya sayansi ya uvuvi kitaifa (COSTECH).

Na kwa kupitia mbinu hizi Tanzania inaweza kupunguza uwepo na utumiaji wa vifaa duni katika shughuli za kiuvuvi nchini na kuongeza mavuno bora ya samaki.

2. Changamoto ya uhifadhi usio bora. Uhifadhi bora wa vyanzo muhimu vya shughuli za kiuvuvi bado imekua ni changamoto Tanzania,ikiwa mabadiliko ya hali ya hewa na uchafuzi wa rasilimali ya maji vinachangia kwa kiasi kikubwa kupungua zao la samaki mitoni, kwenye maziwa na baharini,ikiwa sababu kuu ni uchafuzi wa mazingira na Tanzania chini ya wizara ya uvuvi inaweza kutumia njia zifuatazo kupambana na changamoto hii.

i) Uundwaji wa Sera elekezi na madhubuti za utunzaji wa vyanzo muhimu vya shughuli za kiuvuvi Tanzania. Uundwaji wa Sera elekezi na madhubuti ni jambo muhimu kutokana na Sera zilizopo kuwa Sera bubu na zisizo endanishi na mazingira halisi. Kwa mtazamo huo wizara ya uvuvi na mifumo yake Tendaji inapaswa kuandaa Sera zitakazo endana na mazingira halisi ya nchi na vyanzo vyake. Mfano kuzingatiwa kwa ukuaji wa miji,idadi ya wavuvi na wazawa katika miji husika. Hii itasaidia kupunguza utekelezwaji usio na tija kimazingira. Na Sera hizi zinapaswa kuundwa na wizara husika ya uvuvi na mifumo yake tendaji kwa ushirikishwaji wa Taasisi zisizo za kiserikali na wadau mbalimbali wa mazingira.

ii) Kuhakikisha uwajibikaji wa Taasisi husika za uvuvi kama TAFIRI na FETA katika shughuli zake za usimamizi na utoaji elimu juu ya uvuvi salama na namna ya utunzaji wa vyanzo muhimu vya shughuli za kiuvuvi. Hii itasaidia kupunguza tatizo la uvuvi wa kupita kiasi nchini kwa kuhakikisha elimu zinatolewa mara kwa mara na kua zoezi endelevu.

iii) Utungwaji, Uanzishwaji na usimamizi wa sheria kali kufuatia uharibifu wa mazingira na vya uvuvi nchini, na hii itajenga nidhamu juu ya matumizi mazuri ya mazingira ya uvuvi.

Na kwa kupitia mbinu hizi Tanzania inaweza kupunguza changamoto ya uhifadhi mbovu wa vyanzo vya mazingira.

3. Changamoto ya masoko.
Changamoto ya masoko inachangiwa na changamoto nyingii ikiwemo uhifadhi na vifaa duni. hii ni hatua inayojengwa na hatua nyingine zote ili kustawi.

Na ili Tanzania iweze kustawi kimasoko inapaswa

i) Kufanya maboresho makubwa katika uandaaji, uhifadhi, uangalizi na usafirishaji wa bidhaa za samaki hasa katika uwanda wa kimataifa ili kukidhi matakwa ya walaji kimataifa.

ii) Kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa kwa muda stahiki katika masoko ya ndani na nje kwa kuzingatia ubora wa viwango vya bidhaa kimataifa.

iii) Kujenga mahusiano chanya kimasoko baina ya nchi zilizoendelea katika nyanja za uvuvi ili kukuza ujuzi na uwezo hasa kiteknolojia. Mfano nchi kama china.

Hizi ni miongoni mwa njia ambazo Tanzania ikiziakisi kiutendaji sekta ya uvuvi itakua kwa kiasi kinachoridhisha na kufungua fursa nyingi ikiwemo kuongeza uwanja wa ajira kwa vijana ni wajibu wa serikali kukusimamia mashauri ya wananchi kwa maendeleo ya nchi kiuchumi.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom