SoC02 Makala kuhusu Uwajibikaji

SoC02 Makala kuhusu Uwajibikaji

Stories of Change - 2022 Competition

Sprian joseph

New Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
2
Reaction score
0
Tanzania ni nchi ya Uchumi wa kati kama sijakosea kwa mujibu wa Vyanzo vya Taarifa vya Kiuchumi Uwajibikaji ndio nguzo pekee itayotupigisha hatua kwenda kwenye Maendeleo jumuishi.

Uwajibikaji ni moja kati ya nyenzo kubwa kwenye kuleta Maendeleo katika Taifa lolote duniani,Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ikishirikiana na Wizara ya Kazi,Ajira na Maendeleo ya Vijana huandaa miradi au mikopo ya aina mbalimbali kwa vijana kimaendeleo ambayo ili ifanikiwe huhitaji Uwajibikaji ulio sahihi ambao utaleta tija kwa wanajamii.

Miradi ambayo Serikali huileta kwa wanajamii wake ni miradi ya Kilimo, Mikopo ya Kibiashara kupitia Halmashauri zetu miradi hii yote na mingine wezeshi huhitaji Uwajibikaji ulio timilifu ili kukamilisha malengo husika ya Kimradi.

Wanajamii wengi waliofanikiwa Duniani waliwajibikaji vya kutosha ili waweze kufikia malengo yao kwa wakati na wao wakifaidika kimmoja mmoja hata kiujumla wao na Serikali zao husika nazo zikifaidika.Uwajibikaji pia huchochea Ufanisi wa kazi kwa kiwango kikubwa huku ukiibua changamoto kandamizi zilizo au zinazokwamisha shughuli husika Kimaendeleo.

Unapoutumia Uwajibikaji ipasavyo utakusaidia kupata mibadala aina mbalimbali ya kukabiliana na changamoto pia hufichua watu au jamii iliyokuwa inayokwamisha mikakati au mipango ya Kimaendeleo hapo mwanzo.

Katika miaka ya 1970, China ilianza kutilia maanani maendeleo ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ndipo walianza kuwekeza nguvu kuu za uzalishaji na kuweka mbele fikra za kimkakati za kufufua Uchumi wa nchi kupitia Sayansi,Elimu na Teknolojia.Elimu ,Sayansi na Teknolojia nchini China zimeendelezwa kwa kasi katika miaka ya 1980 hadi 2010, na mafanikio makubwa ya Kisayansi na Kiteknolojia yalipatikana yanaendelea kupatikana tangu miaka ya 1980.

Kuanzia miaka ya 1980 hadi 1990 Serikali ya China ilizindua "Mpango wa 863" na "Mkakati wa Kufufua Nchi kupitia Teknolojia, Sayansi na Elimu" ambao ilisaidia sana kukuza Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia ya China. Serikali ya China ilitilia mkazo Mpango wa 863 kupitia Ufadhili, Mageuzi, na Hadhi ya kijamii kwenye Elimu,Sayansi na Teknolojia kama sehemu ya msingi ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya nchi na pia kwa heshima ya kitaifa.

China imepata maendeleo ya haraka katika maeneo ya kimaendeleo kama vile elimu, miundombinu, utengenezaji wa teknolojia ya hali ya juu, uchapishaji wa kitaaluma, hataza na matumizi ya kibiashara kimtandao.China sasa inazidi kulenga uvumbuzi wa asili na inalenga kurekebisha udhaifu uliosalia.

Unapowawajibisha wanajamii wako au wafanyikazi wako wote kwa kufanya kile wanachopaswa kufanya hukuza uaminifu kati ya watu kibinafsi yao na hata wafanyakazi wako kwa ujumla.Uwajibikaji pia uruhusu watu au wafanyakazi kutegemeana kutimiza majukumu yao au kujisikia vizuri vya kutosha kuwasiliana na mfanyakazi mwenza,meneja au kiongozi wa kijamii kwa usaidizi.Ikiwa wanajamii au wafanyakazi kwenye maeneo husika hawatawajibika au hawatawajibishwa kwa kutofuata makatwa husika, kutofika kwa wakati, kutokamilisha miradi, unapaswa kuchukua hatua na kuwafanya waelewe umuhimu wa uwajibikaji katika jamii zao wanazoishi au maeneo yao wanayofanya kazi.

Uwajibikaji pia hukuza imani miongoni mwa wafanyakazi au wanajamii wanapoweka malengo yao kwenye kumbukumbu. Kujiamini kwa wanajamii au wafanyakazi kunatokana na mazingira yanayokubalika na kuwezesha mwingiliano wa uaminifu na ukosoaji unaothamini mawazo yao kuyaingiza katika shirika au jamii husika na kuwapa uhuru wa kufanya maamuzi kuhusu kazi yao au malengo yao.

Uwajibikaji pia huokoa muda na fedha wakati wanajamii au wafanyakazi kwenye mashirika jamii wanapowajibika shuguli zao za kila siku , matumizi ya muda na fedha hutumika vya kutosha miongoni mwao, hubainisha ufumbuzi wa changamoto zinayopingana kimaamuzi na kujaribu kubainisha matatizo husika. Katika hali hii uwajibikaji hunamaanisha kuwa kila wanajamii au wafanyakazi hutekeleza majukumu yao kwa ufasaha na tatizo likitokea, huliibua badala ya kunyamaza na kuliacha lilete matokeo makubwa zaidi.

Uwajibikaji huwafanya viongozi wa kijamii na viongozi wa makampuni kuwa viongozi bora kwa kuweka misingi ya tabia ya utendaji kazi wa wanajamii na wafanyakazi wao. Iwapo wanajamii au wafanyakazi husika watawajibika itakuwa ni rahisi kwa wanajamii wengine au wafanyakazi kutoka makampuni mengine kuvutiwa na kuiga uwajibikaji wenu kiutendaji kazi.

Uwajibikaji wa kijamii unatambuliwa kama ujuzi muhimu ambao viongozi wa kijamii au waajiri wanatarajia kukutana nao katika uajiri wao au viongozi wa kijamii katika kuongoza kwao. Kushiriki katika uwajibikaji wa kijamii katika umri mdogo kwa vijana wanaochipukia kunahusishwa na matokeo bora katika utu uzima ikiwa ni pamoja na kutambua uzalendo halisi wa eneo unalokulia.

Uchunguzi wangu usioa kina na kifani unaonyesha matokeo chanya ya juu Uwajibikaji kufanya huduma ziwe shirikishi zaidi na kuboresha maendeleo kuelekea Malengo ya Maendeleo ya Milenia, kunufaisha jamii pana. Manufaa ya maendeleo yanayotarajiwa kupatikana kutokana na Uwajibikaji yanazidi kupatikana katika fikra za Sera za wafadhili na midahalo ya kimataifa, ikijumuisha mfumo wa Malengo ya Maendeleo Endelevu ya baada ya 2015.Uwajibikaji wa Kisera umewasaidia wanawake wa Tanzania kuepukana na mifumo kandamizi ya Kijinsia huku kwa upande wa wasichana wadogo nao wakizidi kupambana na ndoa za utotoni.

Tutakapoutumia Uwajibikaji kiusahihi utatukuza Ushiriki wetu kwenye mipango ya Maendeleo na hata umiliki wa mali kwa wanajamii kwa sababu kila mtu atajua wazi majukumu yake Kiuwajibikaji na matarajio yake ni kwenye jamii .

Sio tu kwamba hii inatufundisha wanajamii na wafanyikazi wa makampuni husika nchini kuthamini na kujivunia kazi zao lakini pia inaelezea jinsi kazi yao inavyolingana na picha kubwa.Uwajibikaji pia huleta tija ya Kimaendeleo kwa husaidia Miji yetu kujengeka kisasa.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom