SoC02 Makala: Kwanini Rais wako hawezi kukuletea maendeleo

SoC02 Makala: Kwanini Rais wako hawezi kukuletea maendeleo

Stories of Change - 2022 Competition

Mr AB

New Member
Joined
Aug 23, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Ninaandika makala hii kwa uchungu mkubwa, na kwa maumivu makubwa ambayo yamenitokea baada ya kukatiza katika mitandao ya kijamii na kusikiliza vyombo vya habari. Mara nyingi nimeona hivi vyombo vya kupasha habari katika jamii yetu hasa katika nchi za Afrika zinapishana. Kila mtu akitetea masilahi yake.

Kwanini naongea hivi? Naongea kwa sababu mara nyingi sana, viongozi wa nchi zetu wamekuwa wanafiki na wala kuwili, wasioongea ukweli hata siku moja, wanaojifanya wanapenda kila kiongozi aliyeko juu yao kwa ajili ya masilahi binafsi.

Mfano, mara nyingi viongozi waliyoko chini ya rais huwa wanamsifia rais aliyeko madarakani hata kama akifanya jambo ambalo sio zuri au sio la maendeleo katika taifa, hii ni kwa ajili ya kuogopa kupoteza vibarua vyako.

Kasi hii ya unafiki inaonekana pale rais huyo anapotoka madarakani na kuingia mwingine, mapenzi yote yanahamia kwa yule mpya, na hata kuponda yule aliyekuwa anasifiwa kipindi akiwa madarakani, kwa maana wanafanya hivi kuonyesha yule aliyeondoka hana mamlaka au msaada wowote katika tumbo lao kwani ni muda wa mwingine kumsifia ili awape vyeo na kadhalika.

Tukiachana na hayo, mara nyingi lawama zimekuwa zikimuangukia rais katika maendeleo yanayozubaa au katika taabu wanayopitia wananchi anaowaongoza, hii ni kwa sababu rais hana uwezo wa kuwasaidia katika matatizo yao ya kijamii na kiuchumi, kwani huwa mafanikio au matunda wanayapata wachache tena wanayapata wale ambao wana uwezo tayari, mfano viongozi na hata watu walioko katika biashara kubwa.

Hii hali imekuwa ikiimbwa na watu mbalimbali, kuanzia wananchi wa kima cha chini na hata wapigania haki za binadamu na wanaharakati wengine, lakini limekuwa ni jambo gumu sana kusikilizwa na serikali kuu yoyote ile kwa sababu watu hao nguvu zao huishia midomoni na mtendaji hukaa kimya kwa sababu hawana kitu cha kumfanya chochote kile aliyeko juu.

Wananchi huishia kutaabika na kushindwa kufikisha maoni yao kwa kiongozi mkubwa, kwa sababu ya umbali walioko nao, huku viongozi ambao wako karibu yao wakiyapokea maoni lakini kamwe hawayafikishi juu kwa sababu ya kuwaogopa viongozi hao wakubwa, sio kuogopa fimbo au matusi, la hasha viongozi hao wako kwenye mbeleko za viongozi wakubwa, hivyo huogopa kuwaongelesha mambo magumu wakiamini wanaweza kupoteza vibarua vyao.

Swali kubwa ambalo kila mtu wa kima cha chini hubaki akijiuliza ni kwamba kwanini rais haoni matatizo ya wanachi wake wanaolia kila siku?

Licha ya kujiuliza swali hili, wananchi wadogo hushindwa kupata jibu sahihi kabisa lakini mara zote huhisi ni ubinafsi umewakumba viongozi wakubwa kila waingiapo madarakani.

Lakini majibu ninaweza nikawapa hapa na wakitafakari wanaweza wakaelewa ninachoongea, ni hiki hapa, wakati mtu anaandaliwa kuwa rais wa nchi huanzia katika hali ya uchumi wa chini kama wananchi wengine ilivyo, japo mara nyingine wapo wanaotokea familia za kitajiri.

Mara nyingi watu hao huwa na ndoto kubwa za kuifikisha nchi katika sehemu nzuri sana, lakini kamwe hakuna mtu aliyeweza kutoka moja kwa moja kwenye ukulima na kurukia ikulu, la hasha, viongozi huanza ngazi kwa ngazi, kuanzia udiwani, ubunge, uwaziri mpaka urais.

Hizi ngazi nilizozitaja ni ngazi ambazo huchukua takribani miaka 20 hadi thelathini mpaka kufikia hatua ya kuwa na kigezo cha chama kumkubali mtu na kuhisi anafaa kukiwakilisha chama, au hata kuongoza nchi nzima.

Siri iliyopo ni kwamba, ndani ya kipindi hicho kuanzia kwenye udiwani ni kwamba mtu hupitia maisha ya kupata pesa nyingi ambazo huzizowea na hata kuona milioni hamsini ni pesa ya kawaida.

Mtu huyo huyo huingia katika ubunge na kuanza kuona bilioni ni pesa za kawaida sana, hata hivyo hufikia katika hatua ya uwaziri na kuzidi kuzizoea starehe na hata kusahau maisha magumu ambayo asilimia kubwa ya watu hupitia.

Mtu huyo ambaye anaandaliwa kuwa rais, husahau kutembea kwa miguu, husahau kula vyakula vibaya, husahau kutibiwa katika hospitali za kawaida, husahau shule wanazosoma watoto wa masikini, husahau kwamba shilingi elfu moja inatosha sahani ya wali maharage.

Kwake mtu huyo kula sahani moja ya wali wa shilingi elfu hamsini huona kawaida, kuvaa nguo ya laki tatu huona ni kawaida, kulala nyumba ba milioni mia mbili huoni ni jambo la kawaida, vile vile kuweka hata vocha ya milioni kwa mwezi au wiki huona ni jambo la kawaida sana.

Tena zaidi anaweza kusafiri kwenda nchi yoyote duniani bila kutumia gharama yake hata kidogo, halafu kila mtu anayekaa karibu naye ni mtu mwenye maisha mazuri, huwa hana muda wa kukaa karibu na wale wenye maisha magumu ili ajue mambo yanaendaje huko mtaani.

Hii humuathiri kisaikolojia na kusahau kwamba bado hizo shida zipo, hivyo basi wakati anaingia katika madaraka makubwa ya kuongoza nchi, hujikuta ameshasahau kila aina ya shida, hivyo hata kuhisi wananchi wanaolalamika maisha ni magumu ni kama vile wanaigiza tu.

Maisha huzidi kuwa magumu, rais huwa katika hali ya kiyoyozi muda wote, halipi kodi ya pango, halipii mafuta ya gari anayosafiria, hata maji na chakula na umeme vyote hutumia pesa za serikali, huku mshahara ukizidi kujaa katika akaunti yake ya benki na kusubiri mafao baada ya kumaliza kipindi chake cha kuwa madarakani.

Swali jipya ambalo najua utaniuliza kama nikiishia hapo, ni kwamba nini kifanyike?

Kuna mambo mengi ya kufanya hili kukabiliana na tatizo la kuwa na viongozi wasiojua maumivu wanayopitia lakini mimi nitaongelea mambo mawili tu hapa.

Jambo la kwanza ni kwamba ili kidogo rais au kiongozi ajue uchungu wa maisha wananchi wanayopitia, lazima apunguziwe starehe, mfano kuna nchi ambazo rais akiwa ikulu huwa anakatwa kodi ya pango kumaanisha pale ikulu ni kama amepanga, vile vile hula chakula kinachokatwa kwenye mshahara wake na hata umeme na maji hukatwa kwenye mshahara wake.

Kama safari anazosafiri sio kwa ajili ya umma basi huwa anatumia pesa zake.

Hivyo basi hili jambo kama lingekuwepo kwa kiongozi anayeongoza watu ambao asilimia zaidi ya tisini ni masikini wa kutupwa, basi angejua jinsi gani wanapitia magumu katika kulipia vitu hivyo, na kujua jinsi ya kuvilinganisha (balance).

Jambo la pili ni namna ya kukaa karibu na watu wenye hali ya chini sana.

Kama nilivyotangulia kusema, viongozi wengi huishia kukutana na watu wenye maisha mazuri tu, na kusahau wenye maisha magumu katika jamii...hii inafanya kutokuelewa kama kuna watu masikini katika jamii yake.

Hivyo basi ingetengeneza link au njia ya kuwaweka karibu, mfano labda kwa kuchagua baadhi ya watu masikini au wananchi wa kawada kila baada ya mwezi kutoka katika jamii fulani na kukaa karibu na rais wamueleze matatizo wanayopitia.

Hii ingeweza kuboresha zaidia mfumo wa kuihudumia jamii yote na ikafurahia.

ASANTENI SANA
 
Upvote 1
Fahari ya jamii ni kilimo cha kisasa karibu unipigie kura katika chapisho langu hili.
 
Back
Top Bottom