Makala: Mfahamu Simba Karatasi wa Umakondeni

Na
Kichuguu kinakuwaje?, mimi ninajua tu baadhi ya maeneo huko Masasi vijijini ukanda wa Lupaso wanatumia vichuguu kuzika wafu.
Niliendaga Lindi kutembea baada ya kumaliza shule, pale mjini Mpilipili kuna kichuguu huwa kinawakaga moto usiku, hakuna anayewasha.
Wakazi wa pale siku wanakibomoa wakakutana na damu iliyoganda.
Nahisi kilikuwa kinatumika kwa kafara.
Ila wazee wa pale wanasema pale kazikwa mtu asiyeineonekana....nilistaajabu sana, japo niliushuhudia moto, ila hakuna sarakasi ya 'sayansi' iliyotumika kweli pale🤔
 
Hiyo ndo naisikia kwako, lakini kusini kwa ujumla kuna mambo ya jadi mengi.

Kuna sehemu huko Newala kuna mlima baadhi ya siku huwa kuna sehemu inawaka moto ila ukienda asubuhi hauoni sehemu iliyoungua.

Pia kuna tukio lingine Mtwara alikuwepo bibi ambaye alikuwa anauwezo wa kuzuia gas isiende popote, walifanikiwa baada ya kumalizana wajuavyo.
 
We acha tu.
Kusini kuna mengi mno
 
Bibi Somoe wa Msimbati. Nasikia walimjengea mjengo wale wazungu wa Artmus, maana baada ya kazi kuisha mradi uligoma kufanya kazi hadi huyo bibi alipofanya matambiko yake.
 
Umenikumbusha mbali sana miaka ya sitini. Mimi mkazi wa Kanda ya Ziwa. Enzi zile tukiwa shuleni tulikuwa tukiimba nyimbo nyingi za makabila mbali mbali ya hapa Tanzania. Moja ya wimbo ambao hata chanzo chake sijui ulikuwa unahusu Simba. Maneno yake ni haya: Yalamile, Simba yalamileee Simba X2. Tunduru yalamileee, Simba yalamilee Simba X2. Je yawezekana kuwa huko Tunduru pana hao wanyama kwa wingi. Ajuaye anisaidie kwa hili.
 
Reactions: K11
Mkuu nilishaeleza kwenye hitimisho la makala hii, kuwa mikoa ya kusini hasa Tunduru-Ruvuma kulisifikana sana kuwa na simba wengi na wakorofi. Hivyo mkichokiimba ni kweli kabisa.
 
Ukifika Lindi, wilaya ya Liwale kijiji cha Lilombe kulikuwa na Mzee mmoja anaitwa Mbomolele. Alikuwa na bustani kabisa ya kufuga Simba na Chui miaka ya 90.
Mimi nilikuwa mdogo enzi hizo lakini kaka yetu mkubwa alithibitisha kwa macho baada ya kupelekwa garden na huyo Mzee ambaye alikuwa ndugu yetu ingawa sijaulizia undugu huo ulitokeaje.
Amekufa miaka zaidi ya 15 iliyopita sijui bustani yake alimwachia nani.
Watafiti nendeni
 
kuna mikoa bado watu wameukamatia uchawi hawataki uende.
 
Hiki kisa ni cha kweli mkuu, sema kinasimliwa kwa namna tofauti lakini wote wanaishia kuthibitisha uwepo wa Simba wa Karatasi.

Matukio haya ni miongoni mwa sababu zilizopelekea kuzaliwa kwa nadharia isemayo kusini wanakula watu.
Uvumi wa Wamakonde kula nyama ya watu ulifika maeneo mengi nchini, mpaka Kanda ya Kaskazini.
 
Kuna simlizi nilizisikia, zikidai huenda hiyo nadharia ina ukweli kiasi ndani yake.

Wanasema, inasadikika kuna baadhi ya maeneo miaka ya huko nyuma, ulikuwa unaenda kununua nyama ukijua ni nyama ya Ng'ombe au Mbuzi ila siyo.

Wale wanaoona yasiyoonwa na wengi walikuwa wanathibitisha kuwa baadhi ya siku inakuwa nyama ya binadamu inayouzwa na si nyama ya mnyama husika uliyemtarajia.

Wanaenda mbali zaidi kwa kusema ukiona nyama umeichemsha ikawa na( .... )tambua hiyo siyo nyama ya ng'ombe au mbuzi bali ya mtu.

Ila yote kwa yote inabaki ni nidharia tu ambazo sidhani ilikuwa ni za kweli bali huenda ni mwendelezo wa simlizi za simba wa karatasi.

Ninasema hivyo maana sikuwahi ona au thibitisha hilo pamoja na umri wangu.
Uvumi wa Wamakonde kula nyama ya watu ulifika maeneo mengi nchini, mpaka Kanda ya Kaskazini.
 
Hao waganga huko msumbiji bado wapo mkuu? Kuna likamjamaa limeniingilia kwa Valentina Linajifanya linajua kuimbisha mi nachuniwa tu sasa hivi.

Nifanyie mpango wa kontakti bloo nigeuke simba mie nifanye mambo yangu adabu irudi
 
Hao waganga huko msumbiji bado wapo mkuu? Kuna likamjamaa limeniingilia kwa Valentina Linajifanya linajua kuimbisha mi nachuniwa tu sasa hivi.

Nifanyie mpango wa kontakti bloo nigeuke simba mie nifanye mambo yangu adabu irudi
Labda waje watu wa mipakani ndiyo watakusaidia kuwapata mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…