Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu tuondolee hayo mabano tafadhali!Kuna simlizi nilizisikia, zikidai huenda hiyo nadharia ina ukweli kiasi ndani yake.
Wanasema, inasadikika kuna baadhi ya maeneo miaka ya huko nyuma, ulikuwa unaenda kununua nyama ukijua ni nyama ya Ng'ombe au Mbuzi ila siyo.
Wale wanaoona yasiyoonwa na wengi walikuwa wanathibitisha kuwa baadhi ya siku inakuwa nyama ya binadamu inayouzwa na si nyama ya mnyama husika uliyemtarajia.
Wanaenda mbali zaidi kwa kusema ukiona nyama umeichemsha ikawa na( .... )tambua hiyo siyo nyama ya ng'ombe au mbuzi bali ya mtu.
Ila yote kwa yote inabaki ni nidharia tu ambazo sidhani ilikuwa ni za kweli bali huenda ni mwendelezo wa simlizi za simba wa karatasi.
Ninasema hivyo maana sikuwahi ona au thibitisha hilo pamoja na umri wangu.
Acha niishie hapo, kumbuka tunaangazia biashara za watu, hivyo isijetokea mtu akakutana na hicho ambacho nimeacha kukiandika ikaleta taswira hasi.Mkuu tuondolee hayo mabano tafadhali!
Ikawa na nini?
Povu?
Chumvi?
Maji?
...?
Kweli mkuu Mimi ninatamani kufahamu.Acha niishie hapo, kumbuka tunaangazia biashara za watu, hivyo isijetokea mtu akakutana na hicho ambacho nimeacha kukiandika ikaleta taswira hasi.
Kuna mengine si busara kuongea kwenye hadhara, ikibidi sana labda PM.
Mkuu, lakini utasaidia wengi ukiandika hapa.Acha niishie hapo, kumbuka tunaangazia biashara za watu, hivyo isijetokea mtu akakutana na hicho ambacho nimeacha kukiandika ikaleta taswira hasi.
Kuna mengine si busara kuongea kwenye hadhara, ikibidi sana labda PM.
Enzi hizo ni hatariSimba kidawa hiyo,, hata mie nilisimuliwa kitambo
Sasa kipenzi si usimulie hii tujue mengi ya kusini? Simba karatasi + kichuguu ni 🔥Halafu usisahau kuna ile ya kichuguu.
Hii nilishuhudiaga mwenyewe.
Sema hii ilikuwa kule Mpilipili Lindi
Moto huu huu unaoangaza au Moto wa kiini macho tu? Unaposema alizikwa mtu asiyeonekana unamaanisha nini haswa?Na
Niliendaga Lindi kutembea baada ya kumaliza shule, pale mjini Mpilipili kuna kichuguu huwa kinawakaga moto usiku, hakuna anayewasha.
Wakazi wa pale siku wanakibomoa wakakutana na damu iliyoganda.
Nahisi kilikuwa kinatumika kwa kafara.
Ila wazee wa pale wanasema pale kazikwa mtu asiyeineonekana....nilistaajabu sana, japo niliushuhudia moto, ila hakuna sarakasi ya 'sayansi' iliyotumika kweli pale🤔
Baki na elimu hiyo hiyo ya mzungu😆😆Mtu anakuwaje simba na nyie acheni kutupanga
Huku kwetu wapo kibao, utaskia "mimi simba" mwengine anasema yeye yanga.Mtu anakuwaje simba na nyie acheni kutupanga
kama ni miaka ya themanini ni yule simba mla watu ambae alitengenezewa documentary kwenye national geographic nadhani title yake imefanana na 'man-eating lion of Rufiji'Hiki kisa ni maarufu sana huko mikoa ya kusini
😂😂😂 wanajiita wanyamaHuku kwetu wapo kibao, utaskia "mimi simba" mwengine anasema yeye yanga.
Wewe uliwaona wakibadilika?? Au kisa babu yako kakusimulia basi ukaamini.Baki na elimu hiyo hiyo ya mzungu😆😆
Kuna ukoo tuna undugu nao huko Mlimba Morogoro kwa upande wa mama, ma babu zao huwa hawafi bali hugeuka simba. Nilibisha na kukataa katakata mpaka nilipokuja kuthibitishiwa na babu nilipotembelea eneo husika na kanisimulia vizuri kilichofanyika mpaka hali ikawa hivyo.
Ila kwasasa hawabadiriki baada ya mambo flani flani kufanyika na kurekebisha hiyo hali.
Kiukweli hilo tukio lina maelezo tofauti tofauti mkuu
Tafuta mwigine,achana nayeHao waganga huko msumbiji bado wapo mkuu? Kuna likamjamaa limeniingilia kwa Valentina Linajifanya linajua kuimbisha mi nachuniwa tu sasa hivi.
Nifanyie mpango wa kontakti bloo nigeuke simba mie nifanye mambo yangu adabu irudi
Hahaha kwakweli nipo nusunusu katika kuamini maana tukio alilonihadithia bibi na mjomba angu nao walithibitisha katika kushiriki baadhi ya matukio la ubadirikaji kuwa simba. Yaani iko hivi huyo mzee alikuwa umri umeenda sana na alikuwa analala tu akimaliza haja zote huko huko katika kijumba walichomjengea kwa pembeni. Huu ndio utamaduni wao pale muda unapofika wa wazee wao kubadirika, huwajengea kibanda then wanamuweka humo ndani. Nje wanaandaa ngoma za kitamaduni na matambiko. So siku ikifika wakati wanaendelea kuomba na kucheza kwenye kile kibanda atatoka simba na kuunguruma na kuelekea porini tena kwa madaha na mkienda kwenye kile kibanda hamkuti mtu yoyote so imani yao inajengeka kuwa huyo mtu amegeuka simbaWewe uliwaona wakibadilika?? Au kisa babu yako kakusimulia basi ukaamini.