Makala: Rais wa kivuli, mvutano ndani ya CCM, nguvu inayoongoza machafuko Tanzania

Makala: Rais wa kivuli, mvutano ndani ya CCM, nguvu inayoongoza machafuko Tanzania

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Makala ya uchunguzi iliyotolewa na Lens TV imeibua mjadala mpana baada ya kutoa maelezo ya kina kuhusu misukosuko ya kisiasa iliyoikumba taifa letu Tanzania kufuatia matukio ya Oktoba 29, 2025.

Makala hiyo inadai kuwa machafuko hayo hayakuwa ya ghafla, bali yalitokana na mgongano wa muda mrefu ndani ya chama tawala, Chama cha Mapinduzi (CCM).

Tanzania iliyozoeleka kama nchi ya utulivu kwa miaka mingi imeingia katika kipindi cha sintofahamu kilichoacha majeraha kwa wananchi, uharibifu wa mali, na hofu ambayo bado haijatoweka.

Madai ya operesheni Iliyoratibiwa​

Makala hiyo inaeleza kuwa kile kilichoonekana mitandaoni ni sehemu ndogo tu ya yaliyotokea, wanadai wameona picha na video zisizoweza kuonyeshwa hadharani kutokana na ukali wake, wakisema zinathibitisha kuwepo kwa operesheni ya kimkakati ya kukandamiza upinzani.

Kundi la wanaharakati wa nje ya nchi linatajwa kuendelea kukusanya saini kuitaka jumuiya ya kimataifa ichunguze kilichotokea baada ya uchaguzi.
Hata hivyo, madai haya hayajathibitishwa na vyombo huru.

Ndani ya CCM​

Moja ya hoja kuu ni kwamba si sahihi kulenga lawama zote kwa Rais Samia Suluhu Hassan.
Wanaeleza mizizi ya mkwamo wa sasa iko ndani ya historia ndefu ya siasa za CCM, hasa kipindi cha mchakato wa urithi wa urais mwaka 2015 chini ya Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete



Makala inaturudisha nyuma namna ambavyo jina la Hayati Rais John Pombe Magufuli lilivyopanda kwa mshangao ndani ya chama, kinyume na matarajio ya viongozi waliokuwa madarakani, hapa ndipo mvutano wa ndani ya chama ulianza kukita mizizi.


Enzi za Magufuli na kuongezeka kwa mashaka ya ndani​

Makala inarejea pia tukio la kupigwa risasi kwa kiongozi wa upinzani Tundu Lissu mwaka 2017, ikisema kuwa baadhi ya wachambuzi wa siasa za ndani ya CCM huamini kuwa tukio hilo lilikuwa sehemu ya mapambano ya kimamlaka kuichafua serikali ya rais Magufuli , madai ambayo hayajathibitishwa rasmi.



Ambapo kufikia mwaka 2019, Rais Magufuli alionekana kuwa mwangalifu zaidi, akipunguza safari na kubadili mifumo ya ulinzi wake kwa sababu alihisi tishio kutoka ndani.

Kifo chake mwaka 2021, ambacho serikali ilitangaza kuwa kilitokana na matatizo ya moyo, kinaelezwa katika makala kama “mwisho wa sura moja na mwanzo wa nyingine.”


Madai ya nguvu ya kivuli kuendelea kushika madaraka​

Makala hiyo inadai kuwa baada ya Rais Samia kuingia madarakani, baadhi ya mitandao ya zamani ya kisiasa ilianza kupata nafasi tena hapa ndipo kivuli cha Rais Mstaafu Kikwete kinaonekana sana

Watu kama Captain Tesha na Mange wanatajwa wakidai kuwa Rais mstaafu Kikwete bado anayo ushawishi mkubwa kwa maamuzi mazito ya serikali madai ambayo hayajathibitishwa na hayajatolewa majibu rasmi.



Inaeleza kuwa kwa sasa sauti ya Rais Samia ni kama inadai mamlaka na kukataa maagizo ya nguvu ya kivuli, mgawanyiko mpya” ndani ya CCM kati ya watu wanaomuunga mkono Rais Samia na wale wanaoaminika kuwa bado wako upande wa Rais mstaafu Kikwete.

Yawezekana Rais Samia ameanza mazungumzo ya chini kwa chini na viongozi wa upinzani, ikiwa ni pamoja na Tundu Lissu, kwa lengo la kutuliza hasira za wananchi.




Sababu ya watanzania kuandamana​

Maandamano yaliofanyika Oktoba 29 haikuwa sababu ya masuala ya kiuchumi wala kisiasa, watanzania waliandamana kupiga kelele dhidi ya ukiukwaji wa haki, utekaji na sauti za watu kuminywa.

Kwa sasa taswira ya taifa hili linaendelea kubadilika kimataifa kwa matukio yanayoendelea



​

NB: Tuhuma hizi hazijathibitishwa na Mamlaka
 
nimesoma mpaka “ndani ya ccm” nikaachia hapo, ujinga mtupu, mhusika mkuu ameshajitaja na kujisema yeye mwenyewe na kuelezea kila kitu bado tu mnamtetea klk hata anavyojitetea yeye mwenyewe? …
 
mrisho ni moja la mastermind ila awamu hii Mgeni amekata soda anataka 600 yake..!!Kuna zile movie za korea mzee mstaafu Ila bado yupo katika Uso wa siasa ma ni mwenye Pesa Na ushawishi katika jamii, Anafanya Mbinu zake akishirikiana na wanasiasa Waliopo kwenye mfumo na makundi yao ya polini Ili kumtoa mfalme kwenye kiti ili amuweke anaemtaka Yeye ili amuendeshe anavyotaka,wapige pesa Na Wakifanikiwa kumdondosha mfalme basi wanamuweka mfalme Wao kutoka kwenye kundi lao Wanakula nchii tu 😄 Ila baada ya muda Yule mfalme kivuli anachoka kupelekwa pelekwa anaamua kufanya maamuzi yake binafsi kuongoza taifa cuz kashatengeneza watu katika mfumo na Ana vikundi kama vyote alivyo vitengeneza na mji kashaujua weeee 😀Huwezi kumpelekapelaka tena!😂 Sasa Hili kundi la wastaaafu halitakubali kabisaa kutoswa na hapo ndio mambo ya kutoleana siri yaanza…!!Hio inaitwa kama vipi tukose wote..Hii ni wao kwa wao haiwahusu wananchi…
 
Back
Top Bottom