Makala ya wazi kwa Rais Samia imfikie popote alipo na kuisoma

Makala ya wazi kwa Rais Samia imfikie popote alipo na kuisoma

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Hii ni makala yangu ya wazi kwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Samia Suluhu Hasssan Shujaa wa Afrika,Nuru ya wanyonge,Nyota ya Matumaini na jasiri Muongoza njia.Ni makala Ya kumtia moyo,kumpa faraja,kumpa pole kwa kazi nzito afanyayo pamoja na kumuombea afya njema na nguvu za kuendelea kuliongoza Taifa letu.

Mama yangu,mama yetu ,Rais wangu ,Rais wetu nipende kusema na kuanza kwa kusema Shikamoo Mama. Rais wetu, Mamillioni ya Watanzania wanaendelea kukuombea dua njema,kukuunga mkono wewe binafsi na serikali yako. Hii ni kwa kuwa kwa mikono yako umegusa maisha ya wengi,umewafuta machozi wengi,kuwapa matumaini mamilioni ya watanzania,kuwainua wengi ,kuwapa faraja waliokuwa wamekata tamaa,kuwashika mkono waliokuwa wameanguka na kuishiwa nguvu.

Kwa macho yako ya huruma ,kwa maamuzi yako,kwa sera zako ,kwa vipaombele vyako,kwa hatua zako,ajenda zako,kwa maoni yako,kwa ucha Mungu wako,kwa utu,upendo,huruma na unyenyekevu wako umewapa nuru mamilioni ya watanzania waliokuwa gizani, umesaidia wengi kutimiza ndoto zao,umewaondoa wengi katika dimbwi la umaskini,umewaamsha na kuwapa matumaini wagonjwa wengi waliokuwa wamelala Vitandani wakiwa wamekata tamaa kutokana na hali ya umaskini na kukosa pesa za kupata matibabu,lakini wewe uliwapelekea madaktari bingwa huko huko waliko.

Kwa ulimi wako umeliunganisha Taifa,umewaleta watu pamoja waliokuwa maadui na wakaweza kuzungumza lugha moja,kwa ulimi wako na matendo yako ya haki na huruma na hofu yako kwa Mungu umewapa imani waliokuwa wamekosa Imani ya kuishi na kurejea hapa Nchini,umewahakikishia usalama wao.

Lakini Mama yangu na Rais wangu Mpendwa pamoja na hayo mazuri na mengi Mema uliyoyatenda kwa Taifa letu.Bado kuna watu kwa kukosa uungwana na shukurani,kwa chuki binafsi,kwa maslahi yao binafsi,kwa kutumiwa na kutumika na watu wenye nia ovu wamekuwa wakikushambulia kwa lugha za matusi , udhalilishaji,ubaguzi,chuki na kutweza utu wako. Wamekwenda mbali zaidi kwa kuanza kudhalilisha na kushambulia familia yako na kuihusisha na kila aina ya ubaya kwa lengo la kukuchafua na kukuchonganisha na wananchi wako wenye imani kubwa na wewe.

Lengo lao ni moja tu Rais wangu kwako. Nalo ni kwamba wanataka kukuvunja moyo,kukukatisha tamaa,kukudhoofisha,kukupunguza kasi,kukuondoa kwenye reli,kukuhamisha na kukupa ajenda zao ndio uwe mjadala wa kitaifa kwa maslahi yao.wanataka kukunyong'onyesha na kukuvuruga hasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu. Wanataka wakuchosha akili na kukutikisa,kutetemesha,kukutetelesha pamoja na kukupa hofu na uoga.

Ndio sababu ya kuona wakitunga kila aina ya uzushi usio na ushahidi,kutumia lugha kali kali na mbaya pamoja na kuishambulia familia yako hasa mwanao wa kiume.

Lakini Mheshimiwa Rais Wangu Napenda kukuambia ya kuwa usiogope,usiteteleke,usiteteleshwe,usikate tamaa,usikatishwe tamaa wala kuvunjwa au kuvunjika moyo,usiumie Rais wangu maana tayari umeshaogelea katika bahari ya siasa yenye kila aina ya Mawimbi mpaka hapo ulipofika umri huo .Najuwa umepitia mengi na umekomaa na kuiva na hakuna geni kwako la kuweza kukuondoa katika reli ya kuwatumikia watanzania wenye imani kubwa na uongozi wako.

Rais wangu Mpendwa Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hasssan,Uwe Hodari na Moyo wa Ushujaa . USIOGOPE kwa kuwa Mungu aliyekuinua kwa mkono wake Hodari yupo bado na wewe.Uso wake upo na wewe na mkono wake upo juu yako na yeye yupo ndani yako.

Narudia tena kusema Mama Yangu USIOGOPE. Uwe HODARI na Moyo wa USHUJAA. MUNGU yupo pamoja na wewe.

Kikubwa nakuomba uhakikishe unaendelea kulinda Taifa letu kuendelea kuwa na amani na umoja wa kitaifa. Linda kwa uzalendo ,Wivu ,jasho na Damu kila kitu kilicho mali ya watanzania ndani na nje ya Taifa letu. Usibabaishwe na yeyote. Tumekukabidhi kila kitu mikononi mwako kikatiba. Tumekupa na kukuwekea Vyombo vyote vya ulinzi na usalama vyenye uzalendo uliotukuka na wa mfano kuwa chini yako. Vitumie na saidiana navyo kupigania na kulinda maslahi ya Taifa letu.

Ni mimi Lucas Hebel Mwashambwa. Naweka kalamu yangu chini na kuishia hapa.
 
Mleta mada Siku ingibe ukiandika chochote Kwa Raisi kisizidi sentensi 10

Ana kazi nyingi za kufanya Sio kusoma mangonhera Yako marefu hayo

Nikufundishe unapoandika Kwa mtu wa Chini ikiwa raia wa kawaida unaandika kirefu unapoandika Kwa bosi aliye juu unatakiwa kuandika kifupi na direct to the pointi
 
Mleta mada Siku ingibe ukiandika chochote Kwa Raisi kisizidi sentensi 10

Ana kazi nyingi za kufanya Sio kusoma mangonjera Yako marefu hayo

Nikufundishe unapoandika Kwa mtu wa Chini ikiwa raia wa kawaida unaandika kirefu unapoandika Kwa bosi aliye juu unatakiwa kuandika kifupi na direct to the point
 
Mleta mada Siku ingibe ukiandika chochote Kwa Raisi kisizidi sentensi 10

Ana kazi nyingi za kufanya Sio kusoma mangonhera Yako marefu hayo

Nikufundishe unapoandika Kwa mtu wa Chini ikiwa raia wa kawaida unaandika kirefu unapoandika Kwa bosi aliye juu unatakiwa kuandika kifupi na direct to the pointi
Nimepokea ushauri wako ndugu yangu mtanzania.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Hii ni makala yangu ya wazi kwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Samia Suluhu Hasssan Shujaa wa Afrika,Nuru ya wanyonge,Nyota ya Matumaini na jasiri Muongoza njia.Ni makala Ya

Ni mimi Lucas Hebel Mwashambwa. Naweka kalamu yangu chini na kuishia hapa.
Well done...
 
Kila saa mama, mama, mama, mama, mara tuko mbele yako, tuko nyuma yako na upuuzi mwingine, vitu hivi havimsaidii kiongozi wa familia, mtaa, kijiji ama nchi kutambua anapohitaji kufanya marekebisho ama kusawazisha mahali, acheni tabia za kujikomba komba kwa viongozi, sema ukweli unapohisi kuna shida hiyo ndio njia sahihi. Mtu kama ni mwizi sema huyu ni mwizi sio kuleta lugha tamu tamu kwenye vitu nyenye kuhitaji kusawazishwa.

NB: Wazazi watarajiwa zingatieni matumizi ya Condom msije kujaza dunia kwa watoto wenye utapia mlo wa akili
 
Aisee!
 
Back
Top Bottom