CCM YAMJIBU MARTHA KARUA
•Tanzania ni nchi huru yenye mamlaka kamili
•Uhusiano wa Kenya na Tanzania ni mzuri na wakihistoria
KATORO: KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Amos Makalla amesema Tanzania ni nchu huru, na dola iliyokamilika na yenye mamkala kamili ya kuruhusu Raia wa kigeni kuingia au kutokuingia nchini.
Pia amesema Idara ya Uhamiaji inazingatia sheria na kanuni za watu kuingia nchini ,hivyo haiwezi kushinikizwa kufanya mambo kinyume na taratibu zake
Makalla ameeleza hayo akihusisha keleleza mitandaoni juu ya tukio la kuzuiliwa kwa wanaharakati kutoka Kenya amabao ni Mwanasheria, Martha Karua na wenzake wawili wakidai kuwa kama sehemu ya utetezi katika kesi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.
“Tanzania hii ni nchi huru, ni dola iliyokamikika yenye mamlaka kamilika na uwezo wa kuruhusu au kutoruhusu mgeni yeyote kuingia, kwahiyo hatuwezi kulazimishwa lakini hakuna sheria yeyote duniani inayoweza kushinikiza taifa huru ikiwemo Tanzania kwamba wanashinikiza mtu fulani apokelewe,” amesema Makalla.
Ameongeza idara ya uhamiaji inayomamlaka ya kuruhusu au kutoruhusu raia wa kigeni kuingia na kusisitiza Tanzania haina hitaji za ukombozi kwa sababu tayari ni nchi huru.
Makalla amesema Tanzania ni nchi Salama na ya mfano pia na uhusuano wake na Kenya ni wa kihistoria na ndugu wa pamoja katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na wataendelea kushirikiana na wakenya bila wasiwasi na sio kwa sababu ya wanaharakati akiw
USSR
View attachment 3340295emo Karua .