Elias Msuya
Platinum Member
- Dec 23, 2011
- 267
- 1,014
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Amos Makalla amesema chama hicho kimesogeza vikao vyavuchujaji wa wagombea wa nafasi za ubunge na wabunge kutoka leo Julai 19, 2025 hadi Julai 26 ambako kutakuwa na kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu (NEC) kitakachotanguliwa na kikao cha Kamati Kuu jijini Dodoma.
Pia amesema mchakato wa kuchuja wagombea utakamilishwa Julai 28, 2025.
Ameyasema hayo leo Julai 19 alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, akisema sababu ni wingi wa wagombea hivyo kuchukua muda mrefu kuwachambua.
Amesema mpaka sasa hakuna aliyekatwa wala kufyekwa, bali chama kitafanya uteuzi na wanachama watapewa taarifa.