LGE2024 Makalla: CCM hatuhitaji upendeleo wala kubebwa kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, TAMISEMI itende haki

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Maneno matupu haya. Kule Jimbo la Serengeti wamefuta wagombea wote wa upinzani
 
Haya majitu yanayuchukuliaje wananchi?
 
Mahakama ya Katiba Mozambique yataka wasimamizi wa uchafuzi wa uchaguzi kujitetea madudu ya wazi yaliyojitokeza katika uchaguzi wa 9 Oktoba 2024 nchini Mozambique

 
Mbona 2019 na 2020 waliengua wagombeaji wote wakabakiza wa CCM tu?

Ni dhahiri chama chetu hakikubariki tena na kinatumia maguvu na jinai kubaki madarakani na hiki ndio chanzo cha umaskini wetu. Kiongozi alieyeingia madarakani bila kuetegemea kura za wananchi hawezi kuwa na tija

Wenzetu Kenya walishatoka huko kwenye wizi wa kura ndio maana nchi ipo juu.
 
Waangalizi nao kama Mahakama ya Katiba yaona madudu mengi ya uchaguzi wa chama rafiki cha CCM

Uchafuzi wa Uchaguzi nchini Msumbiji 2024 :

View: https://m.youtube.com/watch?v=9GouOQKDmHQ
Waangalizi wanataja kasoro ikiwemo utekaji wa mchakato mzima wa uchaguzi uliofanywa na FRELIMO
Waangalizi wa uchaguzi kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Republican (IRI) na Umoja wa Ulaya EU, nchini Msumbiji, wanataja kasoro katika mchakato wa upigaji kura, kuhesabu na kuchapisha matokeo ya uchaguzi mkuu wa tarehe 9 Oktoba 2024 ...
 
Tundu Lissu - Huwezi Kuwekewa Pingamizi na Mtu Asiye Mgombea,

Tundu Lissu achambua Maana ya zoezi hili la uteuzi 07 November 2024 lililofanywa na TAMISEMI


View: https://m.youtube.com/watch?v=nECJK6jR04Q
Majina yote yanatakiwa kwanza yawekwe katika ubao wa matangazo ili wagombea wawekewe pingamizi ikiwa lipo, na pia mkurugenzi au TAMISEMI haina mamlaka kisheria kuengua, kuweka pingamizi kwa wagombea asisitiza Tundu Lissu...

Sasa hawa wagombea wetu wamewekewa pingamizi na nani kwa siri kuu? ...
 
Mbinu za CCM ni za kijinga sn
Hakuna mahali CCM inatumia mbingu za kijinga isipokuwa imejaa kiburi na madharau kwa watanzania ndiyo wanaweza kufanya vitu vya kuudhi kama hivi bila kujali chochote. Haya mambo hayakuanza leo.
 
Haki imetendeka, Tamisemi imekata majina ya wagombea karibia wote wa chadema nchi nzima.
 
Na bado
 
Kuwaengua maelfu ya wagombea wa Chadema ni ishara kuwa mnawaogopa, mumepima mumeona wao wanakubalika kwa wapiga kura ndiyo maana mnawaogopa vinginevyo waachiwe wapiga kura kwani ni watu wazima na wana akili timamu wanajua ni watu gani wanawafaa.Hii dhambi anayotenda Mchengerwa ambaye ni Mkwe wa Rais Samia itawatafuna wote.
 
Kimejiandaa ipasavyo kuiba maana makada wake walishasema Mungu atawasamehe baadaye
 
My Take

Naunga mkono msimamo huu thabiti wa Katibu Mwenezi wa CCM Taifa comrede Amos Makala.

Nimeona maeneo Fulani eti Watendaji wamewaengua wagombea wa Chadema Kwa visingizio vya kipuuzi na Baadhi ya maeneo Wananchi wakawapa kichapo.

Tamisemi acheni ujinga,Kila kitu kilichofanywa na CCM kinaonekana Kwa Wananchi so hakuna haja ya mbeleko ndio maana Baadhi ya maeneo Wananchi waliandana baada ya Wagombea wao kutoka CCM kukatwa.

CCM haihitaji mbeleko kushindana na Vyama ambavyo havina uwezo wa kusimamishw wagombea Mitaa ,Vitongoji na Vijijini vyote achilia mbali mawakala.

Hongera Makala

======
Your browser is not able to display this video.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, CPA Amos Makalla, amesisitiza kwa Ofisi ya Rais, TAMISEMI kutenda haki kwa vyama vyote katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji, na Vitongoji unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024. Alisema kuwa vyama vya upinzani vimekuwa wakidai kuwa wagombea wao pekee wamewekewa pingamizi, jambo ambalo linakosa ukweli.

Akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam, CPA Makalla alieleza kuwa CCM pia ina wagombea waliowekewa pingamizi, na kwamba madai hayo ya upinzani ni ya kujaribu kuwahadaa wananchi. Alisisitiza kuwa chama kimejiandaa kushiriki uchaguzi huo na kitatoka kidedea kwa ushindi wa haki.

Makalla alitoa wito kwa TAMISEMI kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na haki, bila upendeleo kwa chama chochote. Alisema CCM inahitaji usawa na haki katika uchaguzi, na kwamba wataendelea kushindana kwa njia ya haki, huku wakiamini kuwa ushindi utapatikana kwa haki na utangazwe ipasavyo.

View: https://x.com/kwamekivaisi/status/1855116413934956684?t=pKN5OGMKN5CtpRoiquVP-g&s=19
@amosmakalla
 
Bora CPA Makalla kuweka msisitizo huo, kuwe na fair grounds kwa vyama vyote nchi hii ni yetu sote. Tamisemi wasijisahau wakaona wanamfurahisha rais, kumbe wanatengeneza machafuko ndani ya nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…