Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla amezungumzia mabadiliko mapya ya sheria kuhusu haki za Wafungwa kupiga kura ambapo amefafanua kuwa kwa sasa Wafungwa wenye vifungo vya chini ya miezi sita wataweza kushiriki katika uchaguzi wakiwa Gerezani.
Amesema, "Lakini pia wasimamizi wa uchaguzi badala ya kuwa viongozi watakua maafisa waandamizi wa umma, lakini mabadiliko yako mengi ni kwamba katika sheria hata wafungwa watapiga kura. Narudia kama mlikuwa hamjui, ndio mabadiliko ya sheria. Wafungwa ambao kifungo chao hakizidi miezi sita watapiga kura wakiwa magerezani. Hivo hivo kwa upande wa Zanzibar wanaiita vyuo vya mafunzo ndio magereza yenyewe na mahabusu."
Makalla ameyasema hayo siku ya Alhamisi Machi 06, 2025 wakati akizungumza na Wananchi pamoja na Viongozi wa CCM katika katika Mkutano wa ndani uliofanyika kwenye Uwanja wa Toto Tundu uliopo Segerea Wilaya ya Ilala Dar es saam ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku tano Mkoani humo.
Aidha CPA Makalla alieleza kuwa ni muhimu kwa Wataalamu wa sheria kuwa na ufahamu wa mabadiliko haya ya kisheria kwani bado kuna baadhi yao ambao hawaoni umuhimu wa haki hii mpya kwa Wafungwa.
Video: Millard Ayo
Pia, Soma

- Makalla: Wakurugenzi hawatasimamia Uchaguzi, ahoji hofu ya CHADEMA kuhusu Uchaguzi licha ya marekebisho ya mfumo
- Tume ya Uchaguzi: Waliohukumiwa kifungo cha zaidi ya miezi sita jela, kuondolewa kwenye daftari la Wapiga Kura
- Tume ya Uchaguzi: Wapigakura milioni 34.7 wanatarajiwa kushiriki Uchaguzi mkuu Oktoba