Makamanda tunayo ya kujifunza kwa Raila Odinga

Makamanda tunayo ya kujifunza kwa Raila Odinga

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Yapo mengi ya kujifunza kwa nguli mpigania haki huyu:

1. Kutambua siasa ni sayansi yenye kubadilika kulingana na mazingira.

2. Hakuna rafiki wala adui wa kudumu bali agenda.

3. Maandamano yasiyo na ukomo ndiyo njia pekee ya kupata tunachohitaji na kwa wakati.

4. Hakuna nguvu iliyo kuu kuizidi nguvu ya Umma.

5. Maandamano hupangwa na kuratibiwa kikamilifu kuweza kufanikiwa na hata kufika kuliko dhamiriwa.

6. Maandamano hayawezi kuja spontaneous kama mvua.

7. Kwenye maandamano huwa casualties hawakosekani na anaweza kuwa awaye yote.

8. Raila au wakenya katika Mapambano si wajinga wanayo hoja na wanakijua wanachokipigania.

FrqRMejWcAM_Etm.jpeg

Mafunzo mengine karibuni tuongezee.

"Hatuna haja ya kupoteza muda na vijana wa hovyo."

Hadi hapo:

"Shikamoo Raila Amolo Odinga."
 
Chezeeni Serikali na Dola zake.....isitoshe karibia kila uzi majivu yenu ni kudai kuwa akwilina alifanyiwa uovu. Mnalia kila siku....

Subirini matunda mle. Kwani lini yakipatikana huwa hamtokei kudai kumwuunga mkono Mama Kwa mnachoitaga kuwa ni ridhaa yake?

Uthubutu, hiki kitu naona ndilo jambo la msingi zaidi, na linajengeka kulingana na tabia za wahusika hasa kutokana na matukio yaliyopita.

Hivyo, kama bado hapa kwetu hatujawahi kufanya maandamano, itatuchukua muda kuja kuyafanya, na pale itakapotokea tumeshafanya, basi hatutakuwa tunajiuliza tena nini tunajifunza kutokana na yanayotokea kwa majirani zetu, kwani tutakuwa tumeshapata experience.
 
Nakumbuka makamanda waliambiwa kwenye maandamano wakae mbele ili wamwagwe mkojo vizuri...tangia hapo wakapoteana mazima 😊😊

Viongozi wenu walizoea kutanguliza masikini kama chambo huku wao wanatafuna ruzuku wakakutanana na Chuma. No asali ni pumzi ya moto tu 😅😅🔥🔥🔥
 
Tanzania hatuwezi kukubali ujingaa huu utokee mpaka pale wale wanaohimiza maandamano wawepo mbele ya mstari na familia zao.

I mean hauwezi kuandaa mandamano afu siku ya kuandamana ushinde kwenye TV na familia yako ukiwaangalia uliowarubuni wakila mkong'oto kutoka kwa polisi brutal.
 
Hata Odinga hakukaa mbele. Odinga kaja baadaye kutokea kusikojulikana. Hili ni funzo muhimu sana. Amekuja kuhutubia na kuweka msimamo:

Tanzania hatuwezi kukubali ujingaa huu utokee mpaka pale wale wanaohimiza maandamano wawepo mbele ya mstari na familia zao.

I mean hauwezi kuandaa mandamano afu siku ya kuandamana ushinde kwenye TV na familia yako ukiwaangalia uliowarubuni wakila mkong'oto kutoka kwa polisi brutal.

Tunauita ushujaa. Kaeni kwa kutulia. Tunakuja:

FrqgobkX0AEOr7I.jpeg
 
Back
Top Bottom