Makamanda tunayo ya kujifunza kwa Raila Odinga

Mkuu hivi umesoma vizuri kweli nilichoandika? Rudia tena kusoma hapo chini afu ndo u comment.

Mi naona kama comment yako ilikuwa ni ya ku quote mtu mungine.
 

Tunajifunza kutoka kwa Raila Amolo Odinga kuhusu hayo kwamba:

"Hatuna haja ya kupoteza muda na vijana wa hovyo."

Raila hawalalamikii wala kuwanyanyapaa hao. Raila anamjua mbaya wake yaani Wiliam Samoei arap Ruto.

Huyo ndiye anayempelekea moto.

Achana na matarishi na vijana wa hovyo.

Tusipoteze muda nao bure!
 

Usipotoshe mjomba. Hata Raila hakuwa mbele wala hakuwa wa kwanza kwenye eneo la tukio:

"He had been holed up at the hotel for the better part of the day, with hordes of his supporters and a battery of local and international journalists held at bay outside the facility by anti-riot police."

Raila versus Ruto: Was it a showdown or shutdown?

Odinga alitokea baadaye akiwa ndani ya nyomi la kufa mtu.

Funzo: "Tunao uwezo wa kulinda viongozi wetu."

Nani asikimbie? Mamboleo? (Bakita wanasema tusiseme) Wafamchezo?

"Pascal Mayalla kulikoni kwenye magoma siku hizi hutaki kufika?" -- Jabali la Muziki.
 
Mkuu wanaokebehi wana majina yao:

"Hatuna haja ya kupoteza muda na vijana wa hovyo."

Hawana mchango wowote kwa taifa hili.

Hao ni mzigo. Hata Kwa Odinga wapo wengine ni walamba asali kama kina Gachagua.
Sawa. Lakini hakuna cha sisi kujifunza toka kwa Raila Odinga. Mazingira ni tofauti kabisa. Nchi hii inazidi kuendeshwa kikomunisti. Halafu wajinga na wanafiki ni wengi mno wanaotumainia “miujiza” na “wateule toka mbinguni” kuleta maendeleo na mafanikio nchini.

Ni hadi siku idadi ya waelewa itakapofikia “critical mass” ndipo tutakaposhuhudia nchi ikifanya mambo ya maana badala huu ujinga wa kuendeshwa na propaganda muflis za kikomunisti.
 
Iko wazi sana, nina elimu yakutosha na akili nyingi. Kama unabisha, jiunge na huyo baba yako muandamane

Kama huna elimu ya kutosha "tuongee mambo ya uganga wa kienyeji tu" -- Dkt. Mwigulu.

Haya ya kina Raila ni level nyingine mkuu.
 
Kama huna elimu ya kutosha "tuongee mambo ya uganga wa kienyeji tu" -- Dkt. Mwigulu.

Haya ya kina Raila ni level nyingine mkuu.
Kama vitu anavyofanya Raila kwako ni vya level ya juu, ninafunga mjadala rasmi.
 
Mkuu usimlaumu Mbowe,tujilaumu wenyewe hata Mimi ninasapoti kabisa Mbowe bora ale asali-huwezi kuwaangaikia watu wasiojielewa.
Jamaa ameanzisha mavugu vugu mengi akakosa support ya watu inataka yeye afanyaje?
 

Hapana sikubaliani nawe. Ona hii:


Hii si vita ya Chadema, ACT au awaye yote.

Tuwaunganishe watu wote chini ya mwamvuli mmoja:

Kuharakisha Katiba Mpya tuunde 'Coalition of the Willing'

Tusinyanyapaane au kuitana majina.

Hakuna aliye bora au mzalendo zaidi kuliko mwingine.

Tofauti yetu Iko humo kwenye ubaguzi wa kijinga.
 
Kama vitu anavyofanya Raila kwako ni vya level ya juu, ninafunga mjadala rasmi.
Afadhali mkuu, kwani najua hata huko Lumumba kwa ujumbe huu wa Raila, nywele watakuwa wanatia maji. 🤣🤣
 
Swali rahisi tu. Lini watanganyika/watanzania kwa ujumla wetu tangu tupate uhuru tumeandama kwa kudai au kupigania maslahi ya nchi especially madai yawe kinyume na uongozi. Ndio tuanze leo? Thubutu!!. Huu ndio ukweli mchungu. Chadema walijaribu kuhamasisha maandamano, yakafeli. Mange naye alijaribu, akashindwa. It has nothing to do na makamanda. Ni hulka yetu wa TZ.
 
Mkuu usimlaumu Mbowe,tujilaumu wenyewe hata Mimi ninasapoti kabisa Mbowe bora ale asali-huwezi kuwaangaikia watu wasiojielewa.
Jamaa ameanzisha mavugu vugu mengi akakosa support ya watu inataka yeye afanyaje?

Kwa Raila Mbowe na sisi tunayo ya kujifunza mengi tu:

"Uwanja wa mapambano Kenya na wetu uko sawa sawa. Sisi tunakwama hapa:

1. Raila anapigana vita hii kama mkenya, siyo kama ODM au Azimio la Umoja.
2. Raila anatumia lugha rafiki akiwaunganisha wakenya kutokea katika magumu yanayowagusa wote.
3. Raila hawanyooshei vidole Kenya Kwanza, mtu au chama chochote bali William Ruto.
4. Raila haondoki alipo kuelekea kwenye maandamano bila kuzungukwa na nyomi ya haja.
5. Raila hahangaiki na wasaliti au vijana wale wa hovyo.
6. Raila amewaandaa watu kufahamu kwenye mapambano kama haya: kukamatwa, kujeruhiwa au hata kufa kumo na hakuna mwenyewe.
7. Raila anapigana huku akiongea pia, ndiyo maana shughuli hii ni ya jumatatu Kwa jumatatu, Hadi kieleweke.
8. Raila yuko wazi mapambano yake ni ya amani.
9. Nk.


Post #192 inahusika.
 
Odinga hajakimbilia ubelgiji dubai wala canada kama kina fulani...amekaza 😅😅

Kwa hiyo wewe umekaza au umelegeza? Kwamba wewe hii inakuhusu au ni Kwa wengine tu?

Zingatia maana ya vijana wa hovyo mkuu 🤣🤣.
 
Na hajawahi kupigwa risasi

Mkuu sikubaliani na huyo kijana wa hovyo uliye mjibu, ila huyu mwamba ni jembe pia.

Amekaa jela mara nyingi ikiwamo miaka 8 mfululizo aki endure mateso makali.

Tunayo mengi ya kujifunza kutoka kwake.

Tutofautishe kujifunza na kuzodoana.
 
Ready to die
Gas kidogo anajificha

Huko siyo kujificha mkuu. Huko ni kujipanga kwa mapambano ya muda mrefu.

Tofautisha kutokuogopa kifo na kukikimbilia au kukitafuta kifo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…