Makamanda tunayo ya kujifunza kwa Raila Odinga

Makamanda tunayo ya kujifunza kwa Raila Odinga

Unaamini umma ukiamua kuandamana kuna polisi atakayethubutu kuzuia?

Wote watakimbia kunusuru maisha yao mkuu.

Rejea nchi mbalimbali namna watawala walivyolewa madaraka wakaamini hakuna mbwa atakasogea barabarani kwakuwa watatumia jeshi kuwapa kichapo lakini siku isiyotarajiwa waliacha starehe zote walizozoea kuponda nakukimbia makazi yao ya kifahari.
Mkuu hivi umesoma vizuri kweli nilichoandika? Rudia tena kusoma hapo chini afu ndo u comment.

Mi naona kama comment yako ilikuwa ni ya ku quote mtu mungine.
Tanzania hatuwezi kukubali ujingaa huu utokee mpaka pale wale wanaohimiza maandamano wawepo mbele ya mstari na familia zao.

I mean hauwezi kuandaa mandamano afu siku ya kuandamana ushinde kwenye TV na familia yako ukiwaangalia uliowarubuni wakila mkong'oto kutoka kwa polisi brutal.
 
vijana wa tz ni wa hovyo kabisa,hawajiamini,wako busy mitandaoni kuunga mkono mafisadi na ufisaji.wanatumiwa vibaya na wanasiasa bila kujua nini hatma yao huko mbeleni.wengine ni maskini wa kutupwa lkn wamerubuniwa na watoto wa familia za kifisadi kuunga mkono ufisadi.

Tunajifunza kutoka kwa Raila Amolo Odinga kuhusu hayo kwamba:

"Hatuna haja ya kupoteza muda na vijana wa hovyo."

Raila hawalalamikii wala kuwanyanyapaa hao. Raila anamjua mbaya wake yaani Wiliam Samoei arap Ruto.

Huyo ndiye anayempelekea moto.

Achana na matarishi na vijana wa hovyo.

Tusipoteze muda nao bure!
 
Tanzania hatuwezi kukubali ujingaa huu utokee mpaka pale wale wanaohimiza maandamano wawepo mbele ya mstari na familia zao.

I mean hauwezi kuandaa mandamano afu siku ya kuandamana ushinde kwenye TV na familia yako ukiwaangalia uliowarubuni wakila mkong'oto kutoka kwa polisi brutal.

Usipotoshe mjomba. Hata Raila hakuwa mbele wala hakuwa wa kwanza kwenye eneo la tukio:

"He had been holed up at the hotel for the better part of the day, with hordes of his supporters and a battery of local and international journalists held at bay outside the facility by anti-riot police."

Raila versus Ruto: Was it a showdown or shutdown?

Odinga alitokea baadaye akiwa ndani ya nyomi la kufa mtu.

Funzo: "Tunao uwezo wa kulinda viongozi wetu."

Nani asikimbie? Mamboleo? (Bakita wanasema tusiseme) Wafamchezo?

"Pascal Mayalla kulikoni kwenye magoma siku hizi hutaki kufika?" -- Jabali la Muziki.
 
Mkuu wanaokebehi wana majina yao:

"Hatuna haja ya kupoteza muda na vijana wa hovyo."

Hawana mchango wowote kwa taifa hili.

Hao ni mzigo. Hata Kwa Odinga wapo wengine ni walamba asali kama kina Gachagua.
Sawa. Lakini hakuna cha sisi kujifunza toka kwa Raila Odinga. Mazingira ni tofauti kabisa. Nchi hii inazidi kuendeshwa kikomunisti. Halafu wajinga na wanafiki ni wengi mno wanaotumainia “miujiza” na “wateule toka mbinguni” kuleta maendeleo na mafanikio nchini.

Ni hadi siku idadi ya waelewa itakapofikia “critical mass” ndipo tutakaposhuhudia nchi ikifanya mambo ya maana badala huu ujinga wa kuendeshwa na propaganda muflis za kikomunisti.
 
Iko wazi sana, nina elimu yakutosha na akili nyingi. Kama unabisha, jiunge na huyo baba yako muandamane

Kama huna elimu ya kutosha "tuongee mambo ya uganga wa kienyeji tu" -- Dkt. Mwigulu.

Haya ya kina Raila ni level nyingine mkuu.
 
Kama huna elimu ya kutosha "tuongee mambo ya uganga wa kienyeji tu" -- Dkt. Mwigulu.

Haya ya kina Raila ni level nyingine mkuu.
Kama vitu anavyofanya Raila kwako ni vya level ya juu, ninafunga mjadala rasmi.
 
Unapoteza muda wako bure kubishana na mtu ambae akili yake iko ndani ya mfuko wa suruali ya Mbowe.

Mbowe amekuwa na utaratibu wa kutembea na akili za nyumbu wake ili iwe rahisi yeye kuwadhibiti pale wanapotaka kufikiri nje ya box.

Ndio maana ni vigumu sana kukuta msukule wa Mbowe unaandika mambo ya maana kuhusu taifa, kwa vile mwamba anawa control kila kitu.
Mkuu usimlaumu Mbowe,tujilaumu wenyewe hata Mimi ninasapoti kabisa Mbowe bora ale asali-huwezi kuwaangaikia watu wasiojielewa.
Jamaa ameanzisha mavugu vugu mengi akakosa support ya watu inataka yeye afanyaje?
 
Sawa. Lakini hakuna cha sisi kujifunza toka kwa Raila Odinga. Mazingira ni tofauti kabisa. Nchi hii inazidi kuendeshwa kikomunisti. Halafu wajinga na wanafiki ni wengi mno wanaotumainia “miujiza” na “wateule toka mbinguni” kuleta maendeleo na mafanikio nchini.

Ni hadi siku idadi ya waelewa itakapofikia “critical mass” ndipo tutakaposhuhudia nchi ikifanya mambo ya maana badala huu ujinga wa kuendeshwa na propaganda muflis za kikomunisti.

Hapana sikubaliani nawe. Ona hii:
FroxCXHX0AAHIzk.jpeg

Hii si vita ya Chadema, ACT au awaye yote.

Tuwaunganishe watu wote chini ya mwamvuli mmoja:

Kuharakisha Katiba Mpya tuunde 'Coalition of the Willing'

Tusinyanyapaane au kuitana majina.

Hakuna aliye bora au mzalendo zaidi kuliko mwingine.

Tofauti yetu Iko humo kwenye ubaguzi wa kijinga.
 
Kama vitu anavyofanya Raila kwako ni vya level ya juu, ninafunga mjadala rasmi.
Afadhali mkuu, kwani najua hata huko Lumumba kwa ujumbe huu wa Raila, nywele watakuwa wanatia maji. 🤣🤣
 
Sisi siyo waoga na issue ni sisi makamanda:

1. Kwanini tunahangaika na vijana wa hovyo? Kuwalalamikia waoga ni kuhangaika na vijana wa hovyo.
2. Raila hataki wavae dare za vyama kwa suala la wakenya. Tusinyoosheane vidole hapa. Hili si la Chadema, ACT, CUF au Rungwe. Hili ni la watanzania.
3. Tusimkere anayeweza kuwa mshirika. Tuwe na Kauli thabiti za kuwaongelea watanzania siyo kuwakwaza
4. Nk

Rejea #1 - #9 pale kuona tunapokwama.
Swali rahisi tu. Lini watanganyika/watanzania kwa ujumla wetu tangu tupate uhuru tumeandama kwa kudai au kupigania maslahi ya nchi especially madai yawe kinyume na uongozi. Ndio tuanze leo? Thubutu!!. Huu ndio ukweli mchungu. Chadema walijaribu kuhamasisha maandamano, yakafeli. Mange naye alijaribu, akashindwa. It has nothing to do na makamanda. Ni hulka yetu wa TZ.
 
Mkuu usimlaumu Mbowe,tujilaumu wenyewe hata Mimi ninasapoti kabisa Mbowe bora ale asali-huwezi kuwaangaikia watu wasiojielewa.
Jamaa ameanzisha mavugu vugu mengi akakosa support ya watu inataka yeye afanyaje?

Kwa Raila Mbowe na sisi tunayo ya kujifunza mengi tu:

"Uwanja wa mapambano Kenya na wetu uko sawa sawa. Sisi tunakwama hapa:

1. Raila anapigana vita hii kama mkenya, siyo kama ODM au Azimio la Umoja.
2. Raila anatumia lugha rafiki akiwaunganisha wakenya kutokea katika magumu yanayowagusa wote.
3. Raila hawanyooshei vidole Kenya Kwanza, mtu au chama chochote bali William Ruto.
4. Raila haondoki alipo kuelekea kwenye maandamano bila kuzungukwa na nyomi ya haja.
5. Raila hahangaiki na wasaliti au vijana wale wa hovyo.
6. Raila amewaandaa watu kufahamu kwenye mapambano kama haya: kukamatwa, kujeruhiwa au hata kufa kumo na hakuna mwenyewe.
7. Raila anapigana huku akiongea pia, ndiyo maana shughuli hii ni ya jumatatu Kwa jumatatu, Hadi kieleweke.
8. Raila yuko wazi mapambano yake ni ya amani.
9. Nk.

Post #192 inahusika.
 
Odinga hajakimbilia ubelgiji dubai wala canada kama kina fulani...amekaza 😅😅

Kwa hiyo wewe umekaza au umelegeza? Kwamba wewe hii inakuhusu au ni Kwa wengine tu?

Zingatia maana ya vijana wa hovyo mkuu 🤣🤣.
 
Na hajawahi kupigwa risasi

Mkuu sikubaliani na huyo kijana wa hovyo uliye mjibu, ila huyu mwamba ni jembe pia.

Amekaa jela mara nyingi ikiwamo miaka 8 mfululizo aki endure mateso makali.

Tunayo mengi ya kujifunza kutoka kwake.

Tutofautishe kujifunza na kuzodoana.
 
Back
Top Bottom