Makamanda walioigharimia CHADEMA kwa machozi, jasho na damu, leo ni wakuitwa wasaliti? Karma Haitawaacha salama, itawatandika tu

Ndio ni wasaliti 100 pasee!! Halima alishalalamika kwamba uchaguzi haukuwa huru na aliibiwa kura ,lakini mbele ya Ndugai akasema kwamba kutokana na kura halali walizopata chama "chao" (CHADEMA) ndio wao wakapata kuwa wabunge wa viti maalumu aksisitiza kwamba hii sio hisani na pia wamepata baraka kutoka kwa MBOWE yaani uongo uongo mtupu! huo ndio usaliti wa Covid19.
 

Ukiwa na taasisi ni lazima ufuate sheria. Huwezi kufanya kugushi barua halafu ukaachwa. Huwezi kuweka urafiki mbele ya Chama. Chama kina taratibu zake. Lakini watu wote wanaopinga ni walewale ambao hawajasema lolote kuhusu wizi wa kura na ukiukaji wa demokrasia hivyo sio watu wenye kuipenda au hata kuwepo kwa Chadema. Kama ni uonevu umefanyika kwa Watanzania wote kwa kuingiza usalama wa taifa kuchagulia wananchi viongozi na kila mtu mwenye busara anaona hilo.
Lakini kwasababu ni Magufuli kuna ambao wata unga mkono kila baya la serikali
 
Ila we jamaa na safari hii ukikosa uteuzi itabidi ujitafakari unakosea wapi? Ujirekebishe ili lengo lako litimie.
 
Aboud Jumbe alikuwa mjumbe wa kamati kuu ya CCM ilikuwaje akaishia kifungo cha ndani,Seif Sharif alikuwa kijana aliyekulia CCM ilikuwaje akatoswa,Sofia Simba aliondokaje CCM kabla ya kurudishwa,Mansour Himid alikuwa nani CCM,Bernard membe alimtukana nani CCM mpaka kufutwa uanachama.

Paskali wewe ni mwana CCM na hii inakukosesha kuwa impartial.Chadema ni chama kinachojijenga na bila kuwa na msimamo kitapotea.
Unapandisha nyuzi nyingi lakini siku hizi hoja zako ni za ukada zaidi.
Ni nani ndani ya CCM angeweza kuvumilia yaliyofanywa na Mkumbo na Zitto?
 
Mkuu Drifter, kwanza asante kwa mchango wako, very objective, kiukweli tangu nimepandisha uzi huu, wewe ndio mtu wa kwanza kunielewa, kwasababu, kiukweli kabisa, hii jf ya sasa, tuna watu wachache sana, wenye kuweza kusoma bandiko na kisha kujiuliza what is the motive behind.

Chama cha Mapinduzi ni chama cha ukweli na haki, kiliasisiwa na Mwalimu Nyerere, mpenda haki na mtenda haki. Baada ya Mwalimu, CCM ilipitia mageuzi na kuishiwa kuhodhiwa na wenye fedha, hivyo kuzalisha kada kubwa ya makada wa CCM ambao ni makada maslahi, na kwenye uchaguzi, wanakuwa wako tayari kutumia mbinu zozote kushinda uchaguzi. JPM alipoingia, amekuja kuibadili CCM kuirudisha ile CCM ya Nyerere. Sasa ndani ya makada wa CCM, kuna makada wa aina mbili, kuna "CCM Die Hard", hawa ndio wanaotaka kuhakikisha CCM inaupondaponda upinzani na kushinda kwa asilimia 99.9% kwa kutumia mbinu zozote.

Tupo sisi makada "Modern CCM" ambao kutokana na good track ya kazi nzuri ya JPM, CCM innashinda kwa mshindi mzuri safi na clear victory, kushinda kwa haki bila kufanya figisu figisu zozote.

Kwa vile Bunge letu ni Bunge la vyama vingi, mimi naamini kuna baadhi ya wana CCM very genuine, hakupenda kuona baadhi ya wapinzani wakishindwa akiwemo mtu kama Zitto!. Lakini kutokana na wapinzani kukataliwa na wananchi, ili Bunge lichangamke, zile kamati 2 za oversight committee, PAC na LAAC, lazima ziongozwe na wabunge wa upinzania ambao ni vichwa vya ukweli, kwenye hao wabunge wote sijaona watu wa kalibre hiyo ndio maana kila siku, tunamuomba Mwenyekiti wetu, JPM, katika zile nafasi zake 10, awateua wapinzani 4, Zitto, JJ Mnyika, Mbatia na kale kabinti Queen Sendiga.

Ili CCM itawale vizuri inahitaji Upinzani makini, ndio maana kila uchao, naibalasa Chadema humu na ACT Zanzibar, waache ujinga wa kususa. Ili kusasa kwa akili ni kususa kama kwa kususa huko utaachieve something, lakini kususa tuu for the sake of kususa, huku you won't achieve anything huu ni ujinga!.

Karibu tena.
P
 
Pamoja na kuwatakia wengine karma, hujawahi kuomba radhi hadharani au hujawahi kuiambia umma wa watanzania karma iliyokupata.

Je upo tayari Sasa kukiri karma iliyokupata ili sisi wengine tujifunze?
 
Nakuhrshimu sana mkuu.kwanza kwa kusimamia unayoyaamin.achana na huyu mtu.alisoma akiwa mkubwa huyu
 
Naifahamu Karma. Imani hiyo nikubwa katika kabila ninalotoka. Wazee wa huko wanasema kuwa Karma inafanya kesi kwanza maana yenyewe haimuonei mtu. Kesi ya Karma ni ya haki kwa sababu haihukumu kwa maneno bali kwa kuona. Inaona na kupima matendo na nia ya ndani kabla haijashusha rungu lake. Tuisubiri hiyo maana haikosei katika hukumu zake.
 
Kwahiyo umeelekeza hoja yako juu ya meza ya uteuzi wa wabunge katika nafasi nane zilizobakia [emoji849][emoji849][emoji849]

Nakuhakikishia KARAMA inakutafuna hupati ng'oo yaani KARAMA iliyokukumba wewe imekutia giza Magu hakuoni, kadri unavyo kukuruka kunyoosha kidole hakionekani

Mungu wa mbinguni azidi kukutia giza kupitia KARMA aliyokugubika nayo ni giza mwanzo mwisho hutoonekana kamwe utastukia tu mitano tena imekatika upo kitaa

[emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787] KARMA BWANA kwa wanafiki huwa ipo very instant ase!!!
 
Pamoja na kuwatakia wengine karma, hujawahi kuomba radhi hadharani au hujawahi kuiambia umma wa watanzania karma iliyokupata.

Je upo tayari Sasa kukiri karma iliyokupata ili sisi wengine tujifunze?
P
 
PISIKALI MALAYA.
 

Mkuu hii takataka imetoka kichwani mwako?
 
Chadema inaonekana kuwa na wasaliti sana; je ni chama cha wasaliti? Je wakipewa nchi wataisaliti pia? Nilipokuwa mwanachadema damu kwa kipindi fulani tuliwahi kuwaita wanachama wenzetu akina Mwigamba, Kitila, na Zitto kuwa ni wasaliti wakajiondoa. walivyoondoka, bado msamiati huu uko kwenye chama, je kina wasaliti wengi, na je ni usaliti wa namna gani?
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kwamba tayari wanachama wake 19 waliofukuzwa uanachama na Kamati Kuu ya chama hicho wameshapelekewa wito wa kwenda kusikiliza matokeo ya rufaa yao waliyoikata siku ya Mei 11, 2022.
Hiki ni kikao muhimu sana, na kitakwenda kujenga heshima kubwa kwa Chadema kama chama cha siasa chenye vikao,kinachoendesha mambo yake kwa kufuata katiba yake!. Haiwezekani chama, an established party kukaa kama a kangaroo court na kufanya maamuzi ya kiajabu ajabu !.
P
 
Wanabodi.

hili ni bandiko la swali "Je Wabunge 19 wa Chadema Walijiteau?. Je CC-ya Chadema ni Kangaroo Court?. Je Baraza Kuu Litabariki Ukangaroo Ule?. Likibariki, Karma Itawatafuna!"
Nawatakia wana Chadema, kikao chema cha Baraza Kuu.

Paskali
Kikao cha Baraza Kuu Chadema, kimelazika, limebariki ule Ukangaroo uliofanywa na CC ya Chadema, uamuzi wa Baraza Kuu Chadema ni uamuzi wa mwisho, final and conclusive. Sijasikia popote juhudi zozote za kumtafuta aliyesaini barua ya uteuzi, sijasikia popote Chadema wakisema kuna forgery au kuripoti popote forgery ile, hivyo hoja za bandiko hili zinasimama, wabunge hao 19 wa Chadema, hawakujiteua wenyewe, waliteuliwa na kiongozi wa Chadema aliyesaini barua yao ya uteuzi!. Hakuna forgery yoyote iliyofanywa kwenye uteuzi wao ndio maana Chadema hawajaripoti forgery popote!.

Tena kiukweli, Halima Mdee ni mwanamke wa shoka kweli kweli nilidhani mbele vya kikao cha Baraza Kuu Chadema angesimama na kuyasema ukweli wa barua yao ya uteuzi, wajumbe wangebaki midomo wazi!.

Kama it's a battle, kina Halima have lost the battle, they have nothing more to loose au ni kukubali kufa kikondoo kwa kuisubiria karma iwalipie, au to keep on fighting hadi risasi ya mwisho na tone la mwisho la damu limwagike kwa kuhamishia mpambano kwenye wiwanja vingine vya Kisheria!.

Halima anamjua aliowasainia barua ya uteuzi, ili kumlinda, waliamua kunyamaza kwa imani kuwa atawaombea msamaha, kumbe... kwenye siasa hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu.

Life goes on
P
 
Bwana P. Umezingumzia sana kuhusu Karma. Na umeonyesha wengi wa waliofukuzwa ktk Cdm kwa makosa mbalimbali walivyokumbatiwa na serkali na ccm kwa kuzawadiwa nyadhifa mbalimbali au ulaji, na umetabali na hao Covid 19 nao watazawadiwa udc,Rc na hata ubalozi na nafasi nyinginezo, KWAKO UNAONA NI KARMA INAWALIPA HUKU UKISAU KUWA ALIYEKUTUMA KUTENDA UOVU KWA MAKUBALIANO ATAKUPA VIPANDE 30 MLIVYOKUBALIANA, WEWE HUO KWAKO NI USHUJAA. Nimesikitishwa sana nawewe ulisaliti hapo uko unasubilia uteuzi, . Huo ni ubinafisi. Watazawadiwa lakini Cdm wamelinda heshima ya chama Chao. Wabinafsi kama wewe na hao COVID 19 hamfai, endeleeni kusubili VIPANDE 30
 
Haya mambo tutaendelea kuyasema hadi yafike mwisho.
P
 
Wewe umeshapoteza credibility humu. Zamani ulikuwa na hoja zenye mantiki, siku hizi umefunikwa na blanketi la ukada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…