Makamanda walioigharimia CHADEMA kwa machozi, jasho na damu, leo ni wakuitwa wasaliti? Karma Haitawaacha salama, itawatandika tu

Hiki ndo umeweza kuandika

Ila hukuweza kutujua NEC walijibu nini kuhusu Nusrat


Jitahidi huenda utachukua nafasi ya Gason Msigwa
Sema wew sio TISS so huwez kufika pale
Unasema huyu siyo TISS? Waulize waliokuwa nae jeshini. Hakuna mwandishi aliepitia jeshini akawa si agents kuanzia enzi za Rumi mpaka Leo. Maafisa wengi hujificha kwenye kivuli cha uandishi wa habari na upiga picha.
 
Paskali kwani wewe wakiwafukuza Hao 19 betrayers utakuwa umepungukiwa nini mbona unatumia nguvu nyingi kuwasemea chadema?Tupe Faida yako humu kama mwanaCCM nguli na mgombea ubunge mthubutu??

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Huyu mpuuzi hana analojua, kadri anavyozeeka ndiyo anazidi kuwa mjinga sijui kwanini?
 
Kumbuka msukuma mwenzako alifukuza watu kuwa hawana vyeti akamuacha Makonda na Kabudi na wakati hao watu hawajawahi kushitakiwa kuwa wameshindwa kutekeleza majukumu yao sababu ya vyeti fake na wametumikia taifa kwa uaminifu sn, pia MUNGU alikuwa na shetani tena akiwa Malaika shetani alipokosea alifukuzwa na MUNGU hakuangalia mazuri ya shetani ya nyuma, ukiwa mtumishi wa serikali ukikosea kidogo utafukuzwa haraka sana hawataangalia mazuri yako yote, Membe amekulia kwenye chama kuliko Mwenyekiti wako(msukuma mwenzako) lakini alikukuzwa CCM hawakuangalia mazuri yake ya miaka 60 iliyopita na hatukuona ukiandika kumtetea. Namalizia kwa kukuita wewe ni mpuuzi kama wapuuzi wengine wanaosaka teuzi kama Benson Bana, hapa upo kutetea njaa zako wala huna lolote wewe mzee usiye na aibu
 
Paschal,
Hiyo miungu yako labda inakusaidia mwenyewe na wenzio mnaoiabudu.
Kama kweli huamini kuwa haki itatendeka, unaonaje mkiwachukua haraka hao wasaliti wa CHADEMA mkawatafutia 'pazuri' huko kwenye pango lenu, badala ya kudhani waweza kubabaisha watu kwa malinganisho ya kitoto kabisa.
Kwa karibu miaka minne, Yuda Iskariote alikuwa mmoja wa wanafunzi thenashara wa Yesu Kristo ,alikuwa pia mtunza mfuko wa team hiyo, lakini bado alimsaliti Yesu.
Kwa wewe, nadhani wewe ungeweza kumsifu kuwa alifaidi kwa kupata vipande 30 vya fedha, lakini pamoja na kuamua kujinyonga, kawa ndio mfano mbaya kuliko yote dunuani.
 
Tena chama chao kitakuwa na wanachama wengi mbona hataki kuwa nao?
 
Kweli mkuu, karma is one real bitch!

Hata wewe hadi leo inakutesa dhidi ya JPM kwa kumuuliza lile swali gumu siku ile na zile posts zako hapa JF za kiroho mbaya kumnanga poti wako. Karma has now come back to haunt you under this regime - left right and centre!
 
Wewe mwenyewe hapa JF ulikuwa unaheshimika sn ulipoleta njaa zako kila mtu akakudharau hatuangalii mazuri ya mtu tunataka watu wenye akili timamu
 
Kuna mtu mwerevu mmoja alisema kuwa unapomnyooshea mwenzako kidole kumbuka vinne unajinyooshea. Kama Kamati Kuu ya Chadema ni kangaroo court basi hata hao unawatetea leo kwa nguvu zako zote walikuwa sehemu yake wakati ilipowashughulikia wakina Silinde. Na kwa maneno yao wenyewe, " mnalia lia nini, Kamati ikishaamua ndio imeamua". Au ni mambo ya mkuki kwa nguruwe?

Bila aibu unasema Slaa alikuwa tortured wakati juzi tu amefariki Ameir kutokana na yaliyomkuta akiwa ndani na haujasema kitu. Huyo Slaa alikuwa water boarded?

Wewe ni kada wa CCM. Ya Chadema yanakuhusu nini? Wakati hao wakina Halima wanasulubiwa uliwahi kuwatetea? Leo ndio unawaona watu?

This is beyond pathetic.

Amandla...
 
Mwenyekiti alikulawiti?

Sent from my SM-A705FN using JamiiForums mobile app
Mwenyekiti hana suluhishi lolote la maana kwa matatizo yanayokikuta chama. Wamefanyiwa uhuni uchaguzi wa serikali za mitaa hakuja na suluhisho lolote la maana. Wabunge na madiwani wananunuliwa na kuhama yeye anaishia kubeza. Wamezuiwa kujenga chama miaka mitano yeye hana suluhisho kakaa tu.
Chama kimekufa taratibu chini ya uongozi mbovu.
 
Ingeleta maana Sana kama pasco mayalla unge declere interest kwenye mwisho wa makala zako ungeandika,"Ni mimi pascal msaka uteuzi".
Hiii ingesaidia watu kujua makala zako kwa sasa zipo bias kwakuwa unanyemela uteuzi kwa jiwe.
 
Kwa wanaomuelewa Mayalla, ameeleza mtego Wa CCM ambao unalenga kudhoofisha CDM. Wakifukuzwa CCM inawatafutia nafasi mzuri serikalini - vyeo kama walivyofanya kwa aliowatolea mfano. Wasipofukuzwa wanataka wanachama Wa CDM waanze kulaumu uongozi. Lengo la sakata hili Ni kuibomoa CDM. Lakini macho ya walimwengu yanaona nia mbaya ya CCM juu ya upinzani. Inakuwaje bunge, tume ya uchaguzi, mwanasheria Wa serikali wabariki uwunjwaji Wa katiba ya CDM wazi wazi, mchana kweupe.
 
Leo yaweza kuja kuwa siku NZURI SANA ya maamuzi magumu kwa FAIDA ya CHADEMA.
 
Paskali sasa nimetambua kwanini ulipata kura 1
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…