Makamanda walioigharimia CHADEMA kwa machozi, jasho na damu, leo ni wakuitwa wasaliti? Karma Haitawaacha salama, itawatandika tu

Makamanda walioigharimia CHADEMA kwa machozi, jasho na damu, leo ni wakuitwa wasaliti? Karma Haitawaacha salama, itawatandika tu

Mkuu Patriot missile , asate kwa utambulisho huu, kwenye bandiko hili nilisema wabunge 5 ni vidumu wa watu wa CC ya Chadema, haiwezekani mwenza wako wa pika pakua, mnalala kitanda kimoja, halafu mara ghafla kaibukia bungeni kuapishwaa halafu wewe ujifanye hujui!.
Tutajie na wale 4 waliobakia, nitakushukuru
Ila Chadema never ceases to suprise me!, nilikuwa najua Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, mke wake ni miongoni mwa wale 19, kumbe sio Naibu Katibu Mkuu wa Zanzibar pekee, kumbe hata Naibu Katibu Mkuu bara!.

Kiukweli nyie Chadema mna dhambi!, yaani mtu amejitoa kwako, akuhudumie huduma zile very personal, halafu unakuja kumfukuza kama mbwa!.

Sasa ndio nimeelewa kwanini Juliana Shonza na Wakudadavuwa wanaichukia sana Chadema!
P
Acha kuipaka Chadema matope wewe kada wa Ccm.
 
Wanabodi,

Mimi ni muumini wa kitu kinachoitwa "Karma", na nimekuwa nikikihubiri mara nyingi tuu humu jukwaani kuwa karma ndio the power pekee ambayo hutoa hukumu ya haki hapa duniani, kwenye karma, mtu unaadhibiwa au kuhukumiwa kwa mawazo, maneno na matendo yako, karma haina mswalie Mtume, wala haujui nani ni nani!, kwenye hukumu ya karma, inatembeza bakra za kutosha na adhabu kubwa ya mwisho ya karma huwa ni kula kichwa!. "The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa Duniani!, Unahukumiwa kwa Matendo Yako!

Leo kikao cha CC ya Chadema, kinakaa as usual, kama kawaida yao, kikao hiki huwa kinakaa as a Kangaroo court!, kama kilivyokuwa kinakaa huko nyuma na kutoa hukumu za kikangaroo za ajabu ajubu ikiwemo timua timua, ambazo karma za hukumu hizo, zinakuja kuigharimu Chadema mbele ya safari, tatizo, wakati wa karma payback time unapofika, when karma strikes back,
no one remembers, hakuna anayekumbuka kuwa kinachotokea ni hukumu ya Karma ya matendo yake ya nyuma!. Tatizo la karma, unaweza kufanya kitu kidogo, tuu, kwako ukakiona ni kidogo, it's nothing and insignificant, lakini when karma takes its toll, mapigo ya karma yanayokushukia ni mapigo makubwa in three folds, kulinganisha na ulichotenda, hadi huwezi kukumbuka ulifanya nini kustahili kinachokupata!. Ila pia, anayehukumiwa pasipo haki, karma pia huwa ina mtake care, na kumu elevate kwa kumuweka mahali pa juu palipoinuka, machoni pa watesi wake!.

Mifano michache ya baadhi ya Matendo ya Chadema, na Matokeo ya Karma Zake.
  1. Chadema walipo establish a torture chamber pale makao makuu yake na kumshughulikia ipasavyo Mlinzi wa Dr. Slaa, Kagenzi, nilionya kuhusu karma. Kwa vile hii ilikuwa ni internal operation, na mimi sio inside man wa Chadema, naombeni ndugu zangu wa Chadema, jifanyieni tathmini, nani alifanya nini, the roles walizo play, then angalia kilichokuja kuwakuta the players, na sasa Kagenzi yuko wapi na ana hali gani!. Bodigadi wa zamani wa Dr. Slaa, Khalid Kagenzi akanusha kutaka kumuua Dr. Slaa, Ya mke wa Slaa na Mlinzi binafsi wa Dk. Slaa, Tena tazameni karma ilivyo, aliyetuhumiwa kumpa sumu Kagenzi ili amtilie Dr. Slaa, na yeye alikuja kutiliwa sumu na ikamwingia na kumdhuri, tena alikuwa ni almanusura!, asingewahishwa saa hizi tungekuwa tunazungumza mengine!.
  2. Chadema mlipokuwa kwenye kikao chenu cha ndani, CC Arusha, kukatokea mtu miongoni mwenu aliyekuwa akivujisha jf, kilichokuwa kinajadiliwa ndani, mlimuita msaliti, kwa kuvujisha info humu JF, jiulizeni ni nani alimdakua mtu huyo, na mlimfanya nini!, then jikumbumbusheni kilichompata huyo kamanda shupavu aliyemshughulikia msaliti!. Kinachoendelea CHADEMA Mitandaoni: Je, ni Ushujaa wa Mhe. Lema au ni Udhaifu wa "Kule Juu"?
  3. Chadema mlipomtimua Juliana Shonza na masalia kwenye kangaroo court yenu, nililizungumzia hili, sasa leo angalieni waliomshughulikia Shonza, nini kiliwakuta, leo wako wapi, na mlinganishe na Juliana Shonza alipo!. Wito: CHADEMA Watendeeni Haki Wanachama Wenu Ili Kuwatendea Haki Watanzania 2015!
  4. Mlipowatimua kina Kitila kwa hoja ya ule Waraka wa Mabadiliko, ambao nyinyi mliuita ni waraka wa mapinduzi, mimi nikawaambie ule ni waraka wa kui transform Chadema kutoka Chama cha kiharakati, kukigeuza Chama Tawala in waiting, hivyo waraka ule haukuwa wa mapinduzi, bali a "winning coalition" kuu revamp uongozi static na stagnant wa Chadema, na kuleta uongozi mpya vibrant na dynamic, angalieni makamanda wa timua timua hiyo nini kiliwakuta, linganisha na mahali alipo Prof. Kitila, tena anakuwa Waziri kwenye key ministry!. Ningekuwa CC ya CHADEMA ningemsamehe Kitila Mkumbo
  5. Mlipomtimua Zitto kwa kutumia CC kangaroo, niliwauliza humu, CC ya Chadema, inapata wapi mamlaka ya kumuadhibu NKM wakati mamlaka yake ya nidhamu ni Baraza Kuu?!, hakuna aliyejibu, angalieni nini kiliwakuta waliomtimua Zitto, na angalieni Zitto ni nani, tena anakwenda kuteuliwa mbunge wa kuteuliwa kwenye zile nafasi 10 za uteuzi za JPM, linganisha makamanda waliosimamia kutimuliwa kwa Zitto!. Opinion: Kung'atuka Kwa Zitto, CHADEMA, Msishangilie, Mkajisahau, Jiandaeni kwa "Karma!"

    Hii ni mifano michache tuu ya dhambi ya dhana ya usaliti inavyoendelea kuitafuna Chadema ndani kwa, ndani, hapo sijamtaja Dr. Slaa, hadi watu kumuita Dr. Mihogo!, leo angalia waliombeza Dr. Slaa wako wapi, ulinganishe na mahali Dr. Slaa alipo!, haiwezekani watu na makamanda wameipigania Chadema kwa kuigharimikia kwa Machozi, Jasho na Damu, halafu leo uje uwaite wasaliti na kuwatimua kama mbwa!, kamwe Karma haiwezi kuacha salama Chadema!.
Hapa nilizungumzia karma kuitandika Chadema. Tunasubiria kwa hamu tamko la Mwenyekiti Mbowe kesho saa 5, asubuhi, akiamua kutetea kiti chake, then mtashuhudia karmic effects kusambaratika kwa Chadema zikianza.

Kuna wakati Mungu anapanga mambo mazuri, kama kumuokoa Lissu na hatari ya kifo kwasababu amemuanda kuja kuwa rais wa Tanzania 2025 kupitia Chadema, lakini shetani akawa hataki, hivyo shetani atamuingia Mbowe, kumfanya moyo wake uwe mgumu, aamue kuitetea nafaso yake. Hapo sasa ndipo mtafunguka macho jinsi bakora za karma zitakavyo itandika Chadema na kuisambaratisha!.
Tusubirie kesho saa 5 asubuhi.
P
 
Wanabodi,

Ndani ya majina yale 19 ya wabunge wa viti maalum wa Chadema, walioapishwa, wabunge 5 ni wake na 'vidumu' vya wajumbe wa CC ya Chadema ambao sio vile 'vidumu' vya 'mpango kando', no!, ni vidumu vya cohabitation, mnaishi nyumba moja, mnalala chumba kimoja, kitanda kimoja!, huku mkiishi katika dhana ya ndoa, na kila mtu anawatambua kama mke na mume!, haiwezekani mwenza wako, akaibukia kwenye majina ya viti maalum bila wewe kujua, kisha akaamkia Bungeni Dodoma kuapishwa bila wewe, kujua!, namhurumia sana KM. JJ. Nnyika ni mtu muadilifu sana, lakini hajui, the games people plays!.
“Unawezaje kwenye meza kuu Mwenyekiti unakaa na manaibu Katibu wakuu wawili ambao wake zao ni sehemu ya wabunge 19 waliopo bungeni, halafu Msigwa akawa hatari, mimi niliongea Mtwara kuwa wanapaswa kujiuzuru msitupe ugumu wa Maisha, haiwezekani wawe wanaanda nyaraka za Ushahidi za Kwenda mahakamani dhidi ya wake zao.”

“Inawezekanaje mbunge Msigwa ambaye mmekorofishana pengine kwa maneno ambayo hayana maana, mnashindwa kupatana halafu Halima Mdee ambaye walikipeleka chama Mahakamani, wanakuwa kwenye ‘Party’ yako ya kufunga mwaka.” Godbless Lema

View attachment 3201877
P
 
Back
Top Bottom