Nguruka
Senior Member
- Dec 6, 2006
- 189
- 129
Ndugu yangu kiukweli hata kama wewe ni Chadema au Chama chochote kile nakupongeza kwa kusema ukweli. Mgombea anatakiwa kusema yale yaliyo katika ilani ndio yapewe kipaumbele hata katika kusam,bazwa katika mitandao ya kijamii, kuliko shutuma. Leo unalalamika wanahabari hawakavi mikutano yako lakini kama kila siku wakija wanakutana na Mipasho na Vijembe, Kebehi, Dhihaka na kashfa na shutuma pasipo kueleza yaliyo katika ilani ya Chama chake itakavyofanya katika kuongoza wananchi basi anatakiwa arekebishwe.Nashangaa sana makamanda wenzangu mnamshambulia Wilson Mahera wa NEC kwa kitendo cha kumuita mgombea wetu kwa kamati ya madili ya taifa.
Je, hamjui kuwa NEC inasimamia uchaguzi ili watanzania wapate maendeleo? Hamjui aliposema watanzaia wanahitaji barabara, sekta ya afya iliyoimalika, sekta ya elimu iliyoimalika na miundo mbinu iliyoimalika. Haya ni maendeleo ya wananchi.
Sasa kama mgombea wetu akisimama jukwaani kazi yake ni kutoa tuhuma za JPM kutokuwa na cheti cha kuzaliwa,kupigwa risasi,ufisadi wa uwanja wa ndege Chato, ufisadi wa ununuzi ndege Atcl n.k. Je hizi ni sera za kuwaletea maendeleo wananchi?
Tuwe wakweli mgombea wetu anatakiwa ajirekebishe sana. Kama anataka urais aseme atatufanyia nini watanzania sio kutuhumu wagombea wenzake.
Je, hizi tuhuma anazozitoa ataweza kuzithibitisha?
WENYE UELEWA WAMEKUELEWA