Lumbeuwanja sawa kati ya wazee na vijana au nini? anacholalamikia ni nini kwa kuwa ni mtoto wa makamba? na je angekuwa si mtoto wa makamba?
Amekuwa mbunge hapo for 25yrs na aliahidi kutogombea 2010, hii inamaanisha bila kumsukia fitina hawezi kutoka, aachie wengine, whether is January au mwingine ye yote. Tunahitaji fikra mpya.
My take; I don't think JM is that fir and good to be MP for Lushoto though. I would support someone else, not the two of them.
This was an irresistible bait. You got a response kaka. Haya shangilia. Anytime you want to debate ishuz instead of this silly baits--holla at your guala.
"My intelligence begins where yours peaks at" -CANIBUS
he he hee,kama kweli aliahidi nadhani aliona 2010 mbaaali ndio mana anakua mbishi haamini kama imefika.:lie:Huyu mzee mcharuko tu, wakati anaomba kura 2005 alisema hataki tena ubunge 2010 sasa anapiga kelele ya nini wakati huu ndio 2010 aliosema hagombei? Amuachie kijana akamate jimbo kwani muda wake umeisha na hakuna alicho fanya, miaka 25 nothing, hebu asepe mazeya ebooooo.
Bahati nzuri namfahamu Mzee Shelukindo kama mwenyekiti wa bodi wa iliyokuwa General Tyre [ea] Ltd kwa zaidi ya miaka kumi na tano.Mzee Shelukindo ni kati ya watu waliochangia kifo cha General Tyre,nasema tena bila ya kutafuna tafuna maneno huyu Mzee ni fisadi kama mafisadi wengine tunaowajua kwa majina na vitendo.
Mzee Shelukindo kama mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi General Tyre alishindwa kusimamia mkopo wa tsh 12 bilioni kutoka NSSF 2005.Chini ya uongozi wake General Tyre haikukaguliwa mahesabu yake kuanzia mwaka 2005 mpaka mwaka 2009 iliipozikwa.Mzee Shelukindo simfagilii January Makamba kwasababu najua nae pia ni zao la mafisadi lakini wewe ni miongoni mwa watu ambao sitawasahau katika maisha yangu yote hapa duniani kwa kusababisha watanzania zaidi ya mia nne 400 kukosa kazi kwasababu ya ulafi wako.Nilimshangaa sana Mzee Shelukindo jinsi alivyokuwa shupavu katika lile sakata la Richmond lakini akawa lege lege kusimamia fedha zetu za kodi.
Waw, it took no time to get 'appropriate response' from 'mhusika'
Ndiye huyo huyo. Si zawadi tu nasikia hata arusi iligharimiwa na.....Jasusi,
Yaani wana Bumbuli wanajua zaidi ung'eng'e ndo maana kawaandikia kitabu cha ung'enge maana angeeandika kiswahili wasingemwelewa ha ha ha, hivi si huyu wakati anaoa alipewa zawadi ya BMW X5 na mtu jina kapuni kama
Yombax2
Mimi nimekunwa na point moja. Kwamba ameamua kuandika kitabu juu ya Bumbuli na mustakabali wake katika lugha ya Kiingereza akiwalenga wale wanaoishi nje ya Bumbuli na Tanzania, na baadaye ndipo kitafsiriwe kwa Kiswahili kuwalenga Watanzania na wakazi wa Bumbuli wasiojua king'eng'e. A very telling point.
I am quite ambivalent about Nyerere, lakini kuna mambo mengi alisema yanaleta maana. Nyerere alisema Tanzania inahitaji kiongozi kichaa ili kuendelea. Na ingawa kuna watu wameleta some crazy talk about January kugombea urais 2015 (obvious hogwash) lakini I would not put this ubunge business being past a stepping stone kenda uwaziri au kazi nyingine kubwa, kwa hiyo hapa ni zaidi ya kuchagua mbunge, Bumbuli wanachagua mtu anayeweza kuwa na cheo chochote mbeleni.
Na nikimuangalia katika level hiyo January hana kichaa cha kutosha, hata hicho kidogo alichokuwa nacho enzi za YA kinaonekana kishapozwa na kufanya kazi na wakubwa, kumzunguka rais, safari na marupurupu etc.Ukikaa na wakubwa sana unakuwa katika hatari ya kuona matatizo ya Watanzania yanatokana si na uongozi mbaya, bali na uvivu wa wananchi, wananchi ambao wengi wao hawana elimu wala nyenzo. Ingawa kuna ukweli fulani katika hili, viongozi wetu wanalipa a disporportionate importance na kuji absolve kutoka katika responsibility.Mkapa alishawahi kusema wazi kabisa kauli hii ya aibu.
Sasa huyu January kwa kauli zake za "A million flies can't be wrong, they eat shyt" yupo katika hatari ya kuona matatizo ya Bumbuli ni makubwa sana na yeye kujitia kuyatatua ni ndoto, kwa hiyo atafanya show tu kama anajali, ataingia bungeni, atajenga jina na connections na kufanya mambo yake, atatumia ukubwa na mwisho wa safari maisha yake yatakuwa safi, atatoa hotuba, ataheshimiwa kibunge na kuendeleza dinasty ya Makamba.
Sioni kichaa cha kutosha kuleta maendeleo hapa.Kichaa amfanyie nani wakati yeye mwenyewe ndiye status quo?
Unfortunately, hivi sasa, to many, bunge ni stepping stone. Siyo kwa lengo la kuhudumia Watanzania, lakini kwa lengo la kujiendeleza binafsi. Vijana wa leo wanaotafuta short cuts wanaona njia pekee ya kujiendeleza ni kugombea ubunge, baada ya hapo upate bahati ya kuchaguliwa kuwa waziri au naibu waziri katika serikali and the rest ni mwendo mdundo. Nchi haina vision, nchi ina ombwe la uongozi, yet utawasikia wabunge watarajiwa wakitoa ahadi kem kem mithili ya maisha bora kwa kila Mtanzania. Hakuna hata mmoja amekuja na ruuya ya Tanzania tunayoitaka na jinsi ya kuifikia. Kwa hiyo ufisadi unafunikwa. Siyo issue tena but a way of life. Ningependa kusikia wagombea vijana wakijitokeza na kusema jinsi wanavyokerwa na rushwa serikalini na jinsi watakavyojitoa kupambana nayo. Hiyo ni bora mara kumi badala ya kuniahidi ujenzi wa barabara na shule.Mheshimiwa Jasusi hii inaonesha kwamba kwa January watu wa Bumbuli ambao ndio wapiga kura ni second best, ila watu nje hasa wafadhili ndio anaotegemea kuwatumikia [ wasambaa wangapi wapiga kura Bumbuli wanatema English]!!! Kijana hana jipya isipokuwa kuendeleza ufisadi wa wafadhili wake akiwemo GT ambae hivi sasa yuko nae Bumbuli!!
Sijali kabisa mgombea anasema atafanya nini jimboni kwake; nimeandika kwa kirefu hili kwenye makala ya MwanaHalisi kesho kuwa wagombea wanatudanganya - makala yangu iliandikwa kabla January hajatangaza nia yake ya kugomba. Kwa ufupi ni kuwa huwezi kutenganisha kinachofanyika Jimboni na kile kinachotokea Dodoma (Bungeni). Nataka nijue mbunge ataenda kufanya nini kubadilisha mfumo wa kifisadi akiwa Dodoma, je anatambua kwamba mfumo huo upo au yote ni bahati mbaya tu. Wanaotaka kuwa wabunge wanataka wafanye nini kubadilisha mfumo mbovu wa uutawala? sheria gani watapendekeza zibadilishwe au taasisi gani zibadilishwe na kwa muda gani watafanya hivyo..
Thats all I care about.. haya ya "sijui nitafanya x,y jimboni" ni irrelevant kwa sababu yana presume kuendelea kwa mfumo ule ule uliopo.
Sijali kabisa mgombea anasema atafanya nini jimboni kwake; nimeandika kwa kirefu hili kwenye makala ya MwanaHalisi kesho kuwa wagombea wanatudanganya - makala yangu iliandikwa kabla January hajatangaza nia yake ya kugomba. Kwa ufupi ni kuwa huwezi kutenganisha kinachofanyika Jimboni na kile kinachotokea Dodoma (Bungeni). Nataka nijue mbunge ataenda kufanya nini kubadilisha mfumo wa kifisadi akiwa Dodoma, je anatambua kwamba mfumo huo upo au yote ni bahati mbaya tu. Wanaotaka kuwa wabunge wanataka wafanye nini kubadilisha mfumo mbovu wa uutawala? sheria gani watapendekeza zibadilishwe au taasisi gani zibadilishwe na kwa muda gani watafanya hivyo..
Thats all I care about.. haya ya "sijui nitafanya x,y jimboni" ni irrelevant kwa sababu yana presume kuendelea kwa mfumo ule ule uliopo.