Elections 2010 Makamba atinga jimboni Bumbuli leo na ufanya vikao vya siri.....

Elections 2010 Makamba atinga jimboni Bumbuli leo na ufanya vikao vya siri.....

Mi namchukulia huyu kijana kama mvivu wa akili, kwani kuna bwana flani kaacha kazi World Bank (akiwa ktk very senior level) kaja kugombea ubunge simply anasema anataka atulize kichwa, kazi za kutumia akili nyingi zinamzeesha!! hope nae huyu jnauary ni hivyo, pia ushawishi wa baba yake na kina jk etc!
 
Its funny how you chose to ignore my two detailed posts (that have answered your question) and picked the one that was not even directed to you.

Anyways babu. To each on his own-
 
uwanja sawa kati ya wazee na vijana au nini? anacholalamikia ni nini kwa kuwa ni mtoto wa makamba? na je angekuwa si mtoto wa makamba?
Amekuwa mbunge hapo for 25yrs na aliahidi kutogombea 2010, hii inamaanisha bila kumsukia fitina hawezi kutoka, aachie wengine, whether is January au mwingine ye yote. Tunahitaji fikra mpya.

My take; I don't think JM is that fir and good to be MP for Lushoto though. I would support someone else, not the two of them.
Lumbe

Nilifikiri mna sababu za msingi kumbe mnamsukia fitina, ukimtoa mtu kwa fitina na wewe utatoka kwa njia hiyo hiyo huenda iliyo mbaya zaidi.
 
This was an irresistible bait. You got a response kaka. Haya shangilia. Anytime you want to debate ishuz instead of this silly baits--holla at your guala.

"My intelligence begins where yours peaks at" -CANIBUS

I call it , a perfect shot made from a cross-haired device, not a silly bait bro.

With 'nataka sitaki' zilikuepo hapa JF na kwene media kwa ujumla kuhusu Bumbuli, at least zile nilizozishuhudia, I can only give my ribs and lungs a perfect exercise with a big phat BWE HE HE HE HE..

Ok, will be back shortly kuanalyse ur 'appropriate responses'.
 
:lie:Huyu mzee mcharuko tu, wakati anaomba kura 2005 alisema hataki tena ubunge 2010 sasa anapiga kelele ya nini wakati huu ndio 2010 aliosema hagombei? Amuachie kijana akamate jimbo kwani muda wake umeisha na hakuna alicho fanya, miaka 25 nothing, hebu asepe mazeya ebooooo.
he he hee,kama kweli aliahidi nadhani aliona 2010 mbaaali ndio mana anakua mbishi haamini kama imefika.
 
Bahati nzuri namfahamu Mzee Shelukindo kama mwenyekiti wa bodi wa iliyokuwa General Tyre [ea] Ltd kwa zaidi ya miaka kumi na tano.Mzee Shelukindo ni kati ya watu waliochangia kifo cha General Tyre,nasema tena bila ya kutafuna tafuna maneno huyu Mzee ni fisadi kama mafisadi wengine tunaowajua kwa majina na vitendo.

Mzee Shelukindo kama mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi General Tyre alishindwa kusimamia mkopo wa tsh 12 bilioni kutoka NSSF 2005.Chini ya uongozi wake General Tyre haikukaguliwa mahesabu yake kuanzia mwaka 2005 mpaka mwaka 2009 iliipozikwa.Mzee Shelukindo simfagilii January Makamba kwasababu najua nae pia ni zao la mafisadi lakini wewe ni miongoni mwa watu ambao sitawasahau katika maisha yangu yote hapa duniani kwa kusababisha watanzania zaidi ya mia nne 400 kukosa kazi kwasababu ya ulafi wako.Nilimshangaa sana Mzee Shelukindo jinsi alivyokuwa shupavu katika lile sakata la Richmond lakini akawa lege lege kusimamia fedha zetu za kodi.
 
Kama nchi zote zilizoendelea zingekuwa zinajiendesha kwa kudai kuwa wazee waondoke, basi watu kama Senetor Kennedy (RIP) na Senator Byrd (RIP) wasingekaa kwenye senate huko Marekani kiasi cha miaka miaka yote hiyo. Kennedy aliingia senate mwaka 1963 hadi alipofariki mwaka jana, na Senator Byrd aliingia Senate mwaka 1957 hadi alipofariki majuzi tu. Nadhani kinachoangaliwa zaidi hapa hasa bungeni iwe ni uwezo wa kufanya kazi bila kuogopa na kuwa mnafiki kuliko kuliko umri na urafiki mtu serikalini; tukumbuke serikali huwa zitabadilikabadilika kwa hiyo urafiki huwa una mwisho wake.
 
Bahati nzuri namfahamu Mzee Shelukindo kama mwenyekiti wa bodi wa iliyokuwa General Tyre [ea] Ltd kwa zaidi ya miaka kumi na tano.Mzee Shelukindo ni kati ya watu waliochangia kifo cha General Tyre,nasema tena bila ya kutafuna tafuna maneno huyu Mzee ni fisadi kama mafisadi wengine tunaowajua kwa majina na vitendo.

Mzee Shelukindo kama mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi General Tyre alishindwa kusimamia mkopo wa tsh 12 bilioni kutoka NSSF 2005.Chini ya uongozi wake General Tyre haikukaguliwa mahesabu yake kuanzia mwaka 2005 mpaka mwaka 2009 iliipozikwa.Mzee Shelukindo simfagilii January Makamba kwasababu najua nae pia ni zao la mafisadi lakini wewe ni miongoni mwa watu ambao sitawasahau katika maisha yangu yote hapa duniani kwa kusababisha watanzania zaidi ya mia nne 400 kukosa kazi kwasababu ya ulafi wako.Nilimshangaa sana Mzee Shelukindo jinsi alivyokuwa shupavu katika lile sakata la Richmond lakini akawa lege lege kusimamia fedha zetu za kodi.

Duhh Mkuuu naoana kinakugusa sana hiko kitendo cha watu 400, kweli ni mbaya sana

Tatizo siasa zimetawala sana na pia wengi wanaficha makucha yao kwa mgongo wa siasa na vyama vyao na kuweka mapandikizi mengine why now people are hastening to Politics sooo badly?
 
Jasusi,

Yaani wana Bumbuli wanajua zaidi ung'eng'e ndo maana kawaandikia kitabu cha ung'enge maana angeeandika kiswahili wasingemwelewa ha ha ha, hivi si huyu wakati anaoa alipewa zawadi ya BMW X5 na mtu jina kapuni kama

Yombax2
 
Ndiye huyo huyo. Si zawadi tu nasikia hata arusi iligharimiwa na.....
 
Mimi nimekunwa na point moja. Kwamba ameamua kuandika kitabu juu ya Bumbuli na mustakabali wake katika lugha ya Kiingereza akiwalenga wale wanaoishi nje ya Bumbuli na Tanzania, na baadaye ndipo kitafsiriwe kwa Kiswahili kuwalenga Watanzania na wakazi wa Bumbuli wasiojua king'eng'e. A very telling point.

Mheshimiwa Jasusi hii inaonesha kwamba kwa January watu wa Bumbuli ambao ndio wapiga kura ni second best, ila watu nje hasa wafadhili ndio anaotegemea kuwatumikia [ wasambaa wangapi wapiga kura Bumbuli wanatema English]!!! Kijana hana jipya isipokuwa kuendeleza ufisadi wa wafadhili wake akiwemo GT ambae hivi sasa yuko nae Bumbuli!!
 
I am quite ambivalent about Nyerere, lakini kuna mambo mengi alisema yanaleta maana. Nyerere alisema Tanzania inahitaji kiongozi kichaa ili kuendelea. Na ingawa kuna watu wameleta some crazy talk about January kugombea urais 2015 (obvious hogwash) lakini I would not put this ubunge business being past a stepping stone kenda uwaziri au kazi nyingine kubwa, kwa hiyo hapa ni zaidi ya kuchagua mbunge, Bumbuli wanachagua mtu anayeweza kuwa na cheo chochote mbeleni.

Na nikimuangalia katika level hiyo January hana kichaa cha kutosha, hata hicho kidogo alichokuwa nacho enzi za YA kinaonekana kishapozwa na kufanya kazi na wakubwa, kumzunguka rais, safari na marupurupu etc.Ukikaa na wakubwa sana unakuwa katika hatari ya kuona matatizo ya Watanzania yanatokana si na uongozi mbaya, bali na uvivu wa wananchi, wananchi ambao wengi wao hawana elimu wala nyenzo. Ingawa kuna ukweli fulani katika hili, viongozi wetu wanalipa a disporportionate importance na kuji absolve kutoka katika responsibility.Mkapa alishawahi kusema wazi kabisa kauli hii ya aibu.

Sasa huyu January kwa kauli zake za "A million flies can't be wrong, they eat shyt" yupo katika hatari ya kuona matatizo ya Bumbuli ni makubwa sana na yeye kujitia kuyatatua ni ndoto, kwa hiyo atafanya show tu kama anajali, ataingia bungeni, atajenga jina na connections na kufanya mambo yake, atatumia ukubwa na mwisho wa safari maisha yake yatakuwa safi, atatoa hotuba, ataheshimiwa kibunge na kuendeleza dinasty ya Makamba.

Sioni kichaa cha kutosha kuleta maendeleo hapa.Kichaa amfanyie nani wakati yeye mwenyewe ndiye status quo?
 
Sijali kabisa mgombea anasema atafanya nini jimboni kwake; nimeandika kwa kirefu hili kwenye makala ya MwanaHalisi kesho kuwa wagombea wanatudanganya - makala yangu iliandikwa kabla January hajatangaza nia yake ya kugomba. Kwa ufupi ni kuwa huwezi kutenganisha kinachofanyika Jimboni na kile kinachotokea Dodoma (Bungeni). Nataka nijue mbunge ataenda kufanya nini kubadilisha mfumo wa kifisadi akiwa Dodoma, je anatambua kwamba mfumo huo upo au yote ni bahati mbaya tu. Wanaotaka kuwa wabunge wanataka wafanye nini kubadilisha mfumo mbovu wa uutawala? sheria gani watapendekeza zibadilishwe au taasisi gani zibadilishwe na kwa muda gani watafanya hivyo..

Thats all I care about.. haya ya "sijui nitafanya x,y jimboni" ni irrelevant kwa sababu yana presume kuendelea kwa mfumo ule ule uliopo.
 
Kiranga... January ni kama Masha.. ndio maana mimi siamini katika nadharia ya "tuwaache vijana wagombe". Madaraka mikononi mwa vijana tutakoma!!
 
Mzee Shelukindo ana haki ya kulalamika. Watu wa Bumbuli wataamua wanamtaka nani kuwawakilisha bunge. Uwanja uwe sawa wa mapambano.
 
Baada ya kukumbwa na kashfa mbalimbali za ufisadi, kama Richmond, EPA, rada, nk, genge la wanasiasa waovu liliunda an "unholy alliance" ili likusanye nguvu pamoja dhidi ya their common enemies Bungeni.
Genge hilo ambalo vinara wake ni Edward Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge (Pembe Tatu ya Ufisadi Bungeni), liliamua kuwashuhulikia Wabunge kadhaa wanaopinga ufisadi serikalini.

Lengo lao ni kuhakikisha kuwa wabunge wafuatao watatu waliosimamia suala zima la Richmond, hawarudi tena Bungeni baada ya uchaguzi wa 2010 ili waweze kujiandaa kurithishwa nchi na Kikwete 2015 kama walivyokubaliana kwenye mtandao tangu mwaka 2005:

1. Spika wa Bunge, Samuel Sitta

Huyu ndiye mwiba mkuu wa wanasiasa mafisadi hapa Tanzania. Baada ya jaribio la kumfukuza Sitta unachama wa CCM kwa kuitumia Sekretariat ya chama na baadhi ya wajumbe wa NEC kushindikana, sasa jitihada kubwa zinafanywa ili kuhakikisha kuwa harudi tena Bungeni. Hii inafanywa kwa kumpandikiza kijana mmoja anayefanya kazi kampuni ya simu ili yeye ndiye apite kwenye kura za maoni kama mgombea wa jimbo la Sitta huko Urambo, Tabora. Pesa nyingi sana zimemwagwa Urambo na zoezi zima hili la kumuengua Sitta linasimamiwa na Waziri wa Kazi, Prof. Juma Kapuya.

Iwapo itashindikana kumwengua Sitta kwenye kupata ubunge, basi watahakikisha kuwa harudi tena kuwa Spika wa Bunge. Eti wamepanga kuwa Lowassa au Chenge ndiye awe Spika mpya baada ya uchaguzi wa 2010 ili kuzima kabisa hoja zote za ufisadi bungeni.

Jinsi mafisadi walivyopanga kummaliza Sitta:

* Plan A - kumfukuza kabisa uanachama wa CCM kupitia NEC (imeshindikana, jitihada mpya zinaendea kutimiza lengo hili)

* Plan B - kumuengua kwenye kura ya maoni (jitihada zinaendelea)

* Plan C - kutumia sheria mpya ya election financing ili awe disqualified kwenye kura za maoni au baada ya kuwa mgombea wa chama ili awekwe mgombea mwingine (jitihada zinaendelea)

* Plan D - kuhakikisha kuwa Sitta harudi tena kuwa Spika iwapo Plans A-C zitakwama (maandalizi ya awali yameanza)

2. Harison Mwakyembe

Huyu jemedari alikuwa ni mwenyekiti wa kamati maalum ya Bunge iliyochunguza Richmond. Walijaribu kumhonga pesa amuokoe Lowassa kwenye kashfa ya Richmond akakataa. Walitishia kumuuwa hakutetereka, mpaka walituma wake zao wamfate nyumbani na kumpigia magoti bado akawa ngangari kinoma. Tayari amepandikizwa mgombea mwingine kwenye jimbo la Kyela ili Mwakyembe aonekane amepata kura chache za maoni na kuenguliwa. Uko pia mpango wa eti CCM mkoa wa Mbeya kufanya vikao vyake wenyewe kuanzia ngazi ya wilaya na kuamua kumfuta uanachama wa CCM Mwakyembe.

3. William Shelukindo

Huyu ni mbunge wa Bumbuli mkoani Tanga. Shelukindo, ambaye ni mbunge wa siku nyingi na pia anaheshimika sana, pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini. Genge la mafisadi wa Richmond linamlaumu sana Shelukindo kwa kuwa kamati yake ndiyo iliyoamua kashfa ya Richmond ichunguzwe na Bunge.
Spika Sitta aliridhia pendekezo la kamati ya Shelukindo kutaka kashfa ya Richmond ichunguzwe na akaunda timu ya kina Mwakyembe kufanya kazi yake.
Genge la mafisadi wa Richmond limeapa kulipa kisasi kwa Shelukindo na kuhakikisha kuwa harudi tena Bungeni na kutoswa kwenye kura za maoni za CCM.

January Makamba (36), mmoja wa wasaidizi wa Rais Kikwete Ikulu ambaye pia ni mtoto wa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, ndiye aliyepandikizwa na mafisadi wa Richmond ili kumng'oa Shelukindo kwenye kura za maoni Bumbuli.
January amepewa war chest (fungu la pesa) kubwa sana na wafanyabiashara mafisadi, akiwemo Yusuf Manji (rafiki wa Makamba), Tanil Somaiya (kuwadi wa rada), Rostam Aziz na wengineo ili kumng'oa Shelukindo Bumbuli.

Waandishi wa habari nao wamenunuliwa ili kumjenga January. Gazeti la Rostam Aziz, Mtanzania, na mengine yalimpamba kijana huyu na front page stories and pictures leo baada ya kutangaza nia ya kugombea Bumbuli.

If all fails, PCCB (chini ya uongozi ule ule uliosema hakuna ufisadi kwenye Richmond), Tume ya Uchaguzi (NEC), polisi, vyombo vingine vya dola, viongozi wa CCM ngazi ya wilaya, mkoa na taifa, watatumika kuwaengua hawa Wabunge watatu na wengineo wafikao zaidi ya 10 ambao wako kwenye listi ya maangamizi.

Kuna mpango kabambe wa kuwatega wabunge walio kwenye listi ya maangamizi (hit list) kwa kutumia sheria mpya ya election financing ili washikwe na tuhuma za kupikwa za rushwa na hivyo wafungwe jela au kuenguliwa na CCM yenyewe, Tume ya Uchaguzi au mahakama.

Pia upo mpango wa kumwaga fedha nyingi kwa wagombea wa vyama vya upinzani kwenye majimbo ya kina Sitta, Shelukindo, Mwakyembe na wengine iwapo jitihada za kuwang'oa kwenye kura za maoni za CCM zitashindikana.
 
Mheshimiwa Jasusi hii inaonesha kwamba kwa January watu wa Bumbuli ambao ndio wapiga kura ni second best, ila watu nje hasa wafadhili ndio anaotegemea kuwatumikia [ wasambaa wangapi wapiga kura Bumbuli wanatema English]!!! Kijana hana jipya isipokuwa kuendeleza ufisadi wa wafadhili wake akiwemo GT ambae hivi sasa yuko nae Bumbuli!!
Unfortunately, hivi sasa, to many, bunge ni stepping stone. Siyo kwa lengo la kuhudumia Watanzania, lakini kwa lengo la kujiendeleza binafsi. Vijana wa leo wanaotafuta short cuts wanaona njia pekee ya kujiendeleza ni kugombea ubunge, baada ya hapo upate bahati ya kuchaguliwa kuwa waziri au naibu waziri katika serikali and the rest ni mwendo mdundo. Nchi haina vision, nchi ina ombwe la uongozi, yet utawasikia wabunge watarajiwa wakitoa ahadi kem kem mithili ya maisha bora kwa kila Mtanzania. Hakuna hata mmoja amekuja na ruuya ya Tanzania tunayoitaka na jinsi ya kuifikia. Kwa hiyo ufisadi unafunikwa. Siyo issue tena but a way of life. Ningependa kusikia wagombea vijana wakijitokeza na kusema jinsi wanavyokerwa na rushwa serikalini na jinsi watakavyojitoa kupambana nayo. Hiyo ni bora mara kumi badala ya kuniahidi ujenzi wa barabara na shule.
 
Sijali kabisa mgombea anasema atafanya nini jimboni kwake; nimeandika kwa kirefu hili kwenye makala ya MwanaHalisi kesho kuwa wagombea wanatudanganya - makala yangu iliandikwa kabla January hajatangaza nia yake ya kugomba. Kwa ufupi ni kuwa huwezi kutenganisha kinachofanyika Jimboni na kile kinachotokea Dodoma (Bungeni). Nataka nijue mbunge ataenda kufanya nini kubadilisha mfumo wa kifisadi akiwa Dodoma, je anatambua kwamba mfumo huo upo au yote ni bahati mbaya tu. Wanaotaka kuwa wabunge wanataka wafanye nini kubadilisha mfumo mbovu wa uutawala? sheria gani watapendekeza zibadilishwe au taasisi gani zibadilishwe na kwa muda gani watafanya hivyo..

Thats all I care about.. haya ya "sijui nitafanya x,y jimboni" ni irrelevant kwa sababu yana presume kuendelea kwa mfumo ule ule uliopo.

Hili linawezekana iwapo tu mbunge huyo atatoka upinzani. Kama anatoka CCM hawezi kufanya lolote, tumeona kelele za akina mwakyembe na Seleli kuhusu richmond, zimeishia wapi? Wametulizwa, halafu na richmond ikafia mbali, sasa ni mfumo gani utabadilishwa hapo? Tukitaka mabadiliko haya unayoyasema mwanakijiji ni lazima tuwe na bunge lenye angalau asilimia 40 ya wabunge wa upinzani. Kwa sababu hao wakiamua kusimama kidedea, hawabanwi na vikao vya CCM wakitoka bungeni. To me hakuna mbunge yeyote anayegombea kupitia CCM atakayesaidia kuleta mabadiliko katika nchi yetu. Kwa sababu wakifika huko wataanza kuimba nyimbo za CCM na kuvaa mashati ya kijani, basi ni pumba tu, hakuna la maana. A simple example, kama si Dr Slaa mbunge wa upinzani kufichua issue ya ufisadi, ni nani angejua kama nchi hii ina ufisadi mkubwa kiasi hiki? Na hata Dr Slaa angefanikiwa kushinda ubunge kupitia CCM asingekaa aseme hizo habari za ufisadi wa nchi hii, na mambo yangekuwa yanaendelea tu. Kwa kweli tunahitaji wabunge wa upinzani rather than these thieves from CCM.
 
Sijali kabisa mgombea anasema atafanya nini jimboni kwake; nimeandika kwa kirefu hili kwenye makala ya MwanaHalisi kesho kuwa wagombea wanatudanganya - makala yangu iliandikwa kabla January hajatangaza nia yake ya kugomba. Kwa ufupi ni kuwa huwezi kutenganisha kinachofanyika Jimboni na kile kinachotokea Dodoma (Bungeni). Nataka nijue mbunge ataenda kufanya nini kubadilisha mfumo wa kifisadi akiwa Dodoma, je anatambua kwamba mfumo huo upo au yote ni bahati mbaya tu. Wanaotaka kuwa wabunge wanataka wafanye nini kubadilisha mfumo mbovu wa uutawala? sheria gani watapendekeza zibadilishwe au taasisi gani zibadilishwe na kwa muda gani watafanya hivyo..

Thats all I care about.. haya ya "sijui nitafanya x,y jimboni" ni irrelevant kwa sababu yana presume kuendelea kwa mfumo ule ule uliopo.

Thanks MKuu

Na hili ndilo tatizo langu kwa January... kwa mfumo uliopo hata iweje we have to expect the same!!!!

The worst part kuhusu kampeni za vijana ni kwamba they speak like Kingunge, Malechela and the likes... wameshindwa kabisa kuja na something different
 
Back
Top Bottom