I am quite ambivalent about Nyerere, lakini kuna mambo mengi alisema yanaleta maana. Nyerere alisema Tanzania inahitaji kiongozi kichaa ili kuendelea. Na ingawa kuna watu wameleta some crazy talk about January kugombea urais 2015 (obvious hogwash) lakini I would not put this ubunge business being past a stepping stone kenda uwaziri au kazi nyingine kubwa, kwa hiyo hapa ni zaidi ya kuchagua mbunge, Bumbuli wanachagua mtu anayeweza kuwa na cheo chochote mbeleni.
Na nikimuangalia katika level hiyo January hana kichaa cha kutosha, hata hicho kidogo alichokuwa nacho enzi za YA kinaonekana kishapozwa na kufanya kazi na wakubwa, kumzunguka rais, safari na marupurupu etc.Ukikaa na wakubwa sana unakuwa katika hatari ya kuona matatizo ya Watanzania yanatokana si na uongozi mbaya, bali na uvivu wa wananchi, wananchi ambao wengi wao hawana elimu wala nyenzo. Ingawa kuna ukweli fulani katika hili, viongozi wetu wanalipa a disporportionate importance na kuji absolve kutoka katika responsibility.Mkapa alishawahi kusema wazi kabisa kauli hii ya aibu.
Sasa huyu January kwa kauli zake za "A million flies can't be wrong, they eat shyt" yupo katika hatari ya kuona matatizo ya Bumbuli ni makubwa sana na yeye kujitia kuyatatua ni ndoto, kwa hiyo atafanya show tu kama anajali, ataingia bungeni, atajenga jina na connections na kufanya mambo yake, atatumia ukubwa na mwisho wa safari maisha yake yatakuwa safi, atatoa hotuba, ataheshimiwa kibunge na kuendeleza dinasty ya Makamba.
Sioni kichaa cha kutosha kuleta maendeleo hapa.Kichaa amfanyie nani wakati yeye mwenyewe ndiye status quo?