Makamba futa tarif 4 na tarrif 6, ambapo Bei ya unit moja ni sh 100 na sh 12 ilihali TANESCO wanaonunua zaidi ya 200

Kwani tanesco wananunua umeme kutoka kwa nani?
Sina habari kama shirika lilishabinafsishwa
 
Kwani tanesco wananunua umeme kutoka kwa nani?
Sina habari kama shirika lilishabinafsishwa
Wanauziwa na Songas, pia Gesi ya kuzalisha kinyerezi wanauziwa na wenye Gesi kupitia Tpdc
 
Kimekuuma nini? Ulikosa vigezo nini ndo povu
 


Mheshimiwa JANUARY MAKAMBA WAZIRI WA NISHATI UPO ???!!--- huu ni ushauri mujarabu.

Nakuunga mkono mtoa hoja.🙏🏻🙏🏻🙏🏻
 
Kimekuuma nini? Ulikosa vigezo nini ndo povu


Hizi ni tarifu wa wizi wa mali ya umma.---- mbona kwenye bili za maji hakuna kitu hicho je huko nako hakuna masikini au Matumizi madogo ya maji kama hivyo ndio vigezo???!!😱
 
Huu ndio mkapa alisema wivu wa kike!
Kama na wewe unaqualify kuingia hiyo tariff Si uingie
Kusema kwamba matajiri ndio wanaitumia Si kweli kwasababu kigezo kikubwa ni uwe na matumizi chini ya units 75 Kwa mwezi, sasa tajiri anatumia chini ya units 75?
Huo mfumo unafanya kazi automatic, ukizidi unit Hata moja unapigwa Penati, ukirudia unaondolewa automatic.

Kama mtu ana sifa hizo aombe aingizwe kwenye tarifu husika tuache wivu wa kijinga.
Wafanyakazi wa shirika kupewa ofa ya units sioni tatizo,mashirika mbali mbali wanatoa bonus Kama motisha tuache kijicho
 
Wabongo bwana!! Badala ya kulia umeme wa majumbani ushushwe bei nyie mna taka bei zirnde juu ati Tanesco wana pata hadara. Jema kwenu nyie ni lipi??


Jema ni kwamba kuweopo na haki sawa katika tariffs za umeme ili Tanesco wasipandishe bei ya umeme kutokana na gharama za ununuzi kuwa ni kubwa kuliko gharama za ugavi kwa wateja wao, kifupi ni kwamba kama tariffs 4 na 6 zikiondolewa basi hao wateja wa hizo tariffs watachagia gharama za unit kama wateja wengine, kuwepo kwa hizo tariffs ni sawa na UBAGUZI wa kijamii ambalo sio jambo zuri na halikubaliki, nchi moja lakini kuna ubaguzi wa kijamii wenye athari kwa shirika la umma!!?--- hiyo sio sawa hata kidogo.
 
Ni kweli tariff hiyo ya sh 100 wanaoitumia wengi ni wenye vipato, ifutwe tu maana ni hasara kwa shirika,
Sijui unamaanisha nini unaposema wenye vipato; lakini kama kuna watu kwenye middle income bracket wanaotumia chini ya unit 75 kwa mwezi watakuwa watu wa ajabu sana.
 
Acha povu lisilo na mantiki, hiyo tariff imewekewa hiyo Kilimanjaro tu au ni sera ya shirika Kwa nchi nzima? Kama huko kwenu ni mbumbumbu hamjui kutumia fursa Kama hizo tulia.
Hiyo Kilimanjaro inapendelewa na Nani? Rais gani mchaga? PM gani mchaga?Makamu gani wa Rais mchaga?

Mjomba wako alivyopata Madaraka si alikimbilia kujenga uwanja wa kutumia peke yake? Jifunze Kutoka Kilimanjaro kufanya kazi kwa bidii, kutumia fursa zilizopo na kuacha kulalamika hovyo
 
Wabongo bwana!! Badala ya kulia umeme wa majumbani ushushwe bei nyie mna taka bei zirnde juu ati Tanesco wana pata hadara. Jema kwenu nyie ni lipi??
Nimemshangaa huyu jamaa mkuu
 
Ukiangalia kwa undani utagundua mabeberu bado ndo wanatuuzia Gesi kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme kwahiyo kiufupi Bei ya umeme inapangwa na mabeberu ya Gesi songas na kinyerezi. Cc ni tuna kauli kwenye vubwawa tu hivo
Kiwango gani cha umeme unatoka kwenye gas?
 
Ina maana we ndo unajua sanaaaa Sana kuliko wahusika? Kwa mfano Mimi ninatumia Unit 20 kwa mwezi unataka nilipe mabilioni??????
 
Tuache roho za umasikini na roho mbaya zisizo na sababu. Kila mtanzania anafursa ya kuwa kwenye hii Tarif. Mtoa mada anadanganya kuwa Matajiri ndo walioko kwenye hii tarif kitu ambacho ni uongo.

Kujibana kwa mtu mwenye nyumba kubwa pamoja na vifaa vya umeme kama pasi fridge na vingine ili kubakia kwenye hii tarifu ni ngumau sana. Ukweli watu wa kipato cha chini wanatumia umeme kidogo kwa ajili ya mwanga tv na matumizi madogo.

Tumia umeme kwa kujiongezea kipato. Usijaribu kubana shuhuli za uzalishaji ili kurudi tarif zero kwani utakuwa hautumii umeme kujiongezea kipato.
Uamuzi ni wako kuwa tarif zero. Kunahuduma nyingi tu ambazo unazipata kwa bei ya chini kwasababu tu serikali imeshaweka ufadhili wake. Hii ndo kazi ya serikali kusaidia wasio jiweza. Tusifanye kila kitu kiwe biashara.
 
This is double standards. Nashauri wafanyakazi wa Tanesco waongezwe mishahara, ila kila mtu anunue umeme kwa bei moja, kama niliwahi kushauri kwenye kodi, viongozi ambao hawalipi kodi, waongezwe mishahara, walipe kodi, wote tulipe kodi.
P
 
Usitetee hii tarrif inaua shirika hata Kama inakunufaisha wewe binafsi
 
Kaka Mayalla hii umeongea Bonge la point, win win situation
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…