Kenya 2022 Makamishina IEBC: Jumla ya kura zilizohakikiwa ni 100.1% ndio tunauliza hiyo ziada sawa na kura 143,000 imetoka wapi?

Kenya 2022 Makamishina IEBC: Jumla ya kura zilizohakikiwa ni 100.1% ndio tunauliza hiyo ziada sawa na kura 143,000 imetoka wapi?

Kenya 2022 General Election
Hata mkipinga matokeo mahakamani hakuna mabadiliko ,subiri uone maigizo ya demokrasia. Hii ndo afrika
Wewe una tatizo moja. Umejaa tabia ya ''bisha kwanza fikiri baadae''. Kipindi kile cha uchaguzi mwingine yale matokeo yaliyotenguliwa mahakamani yaliyenguliwa na shetani? Hujui ile hukumu ilikuwa muhimu sana na ndiyo iliweka maelekezo muhimu kuhusu hatua ambazo uchaguzi unatakiwa ufanywe?
 
wewee umetaja 2020 pekee it means unaona uchaguzi huo ndio mbovu kuliko zilizopita
Yes! 2020 kulikuwa hakuna uchaguzi bali uporaji ulipachikwa jina la uchaguzi. 2020 ilikuwa ni kilele cha uchaguzi mbovu kuwahi kutokea.
 
Wewe una tatizo la kukurupuka na kujigeuza mleta mada sijakuquote wewe, au ndo mambo ya fekero. Punguza mapovu. Raila kila uchaguzi anashindwa na analalamika kuibiwa na ushahidi tele mahakama ipi ilipondua matokeo ya malalamiko yake?
Wewe una tatizo moja. Umejaa tabia ya ''bisha kwanza fikiri baadae''. Kipindi kile cha uchaguzi mwingine yale matokeo yaliyotenguliwa mahakamani yaliyenguliwa na shetani? Hujui ile hukumu ilikuwa muhimu sana na ndiyo iliweka maelekezo muhimu kuhusu hatua ambazo uchaguzi unatakiwa ufanywe?
 
Kura zilizoharibika hakuna ..wasimamizi wa uchaguzi vituoni inaonekana wamesaidia watu kupiga kura vizuri..!!
 
Ni kweli kwamba 143,000 = 1% (appr), na wala siyo 0.01%

Angalia vizuri, the 4 commissioners wanazungumzia kasoro ya kura 143,000 ama kasoro ya asilimia 0.01?

143,000 votes = 1%

0.01% = 1,400 votes
Fuatilia maelezo yao kamili wametaja yote mawili asilimia 0.1 na hiyo figure 143 000
 
Wapiga kelele za tuwaige wakenya tunawasubiria hapa
Sasa huoni hiyo ni demokrasia? Kitendo cha mtu kwenda mahakamani ndiyo demokrasia yenyewe maana hapa kwetu hairuhusiwi katu kwenda mahakamani hata kama mshindi ametangazwa huku paliwa na dosari za wazi.

Pia tume kugawanyika ndiyo uhuru wenyewe wa tume huru ya uchaguzi sio kama tanzagiza wajumbe wa tume ni kama misukule inaburuzwa tu.
 
Fuatilia maelezo yao kamili wametaja yote mawili asilimia 0.1 na hiyo figure 143 000
Basi, ngoja tungoje. Bila shaka wataleta ufafanuzi kamili. Labda mahesabu yameshabadilika siku hizi.
 
Wameshindwa kuleta hoja za msingi, dada cheupe hapendi maswali, ameulizwa unayakataa matokeo je unayo ya tofauti? hana..ameulizwa mwenyekiti chibukati si ndo mwenye mandate ya kuyatangaza? ndioo..anasema matokeo walitaka wayadiscuss..kudiscuss ili iweje? uyaedit au..
Ni sahihi aslimia kuzidi 100%?

Ushahidi wanao wataenda mahakamani ndo itafahamika. Unadhani wewe hapo ulipo huna hata mwelekeo wa maisha na wenzako ni makamishna wa tume kukataa matokeo unadhani hawakufikiri vyema?

Hiyo ndiyo demokrasia sasa siyo huku tanzagiza mwenyekiti akisema amesema wajumbe wanabaki misukule tu.
 
Imetoka hiyo,mzee odinga akalee wajukuu sasa
Hiyo labda kwa tanzagiza ndo ingekuwa imeisha. Ila kwa nchi ya wenzetu ambako kuna demokrasia ya kweli basi wakienda mahakamani ku challenge uchaguzi unaweza kufutwa kama ilivyokuwa mwaka 2017.
 
Mkuu kama chibukati mwenyewe alimuondolea Ruto kura 10000 zilizkuwa zimeongezwa katika kituo kimoja tu,ni ushahidi pasina shaka kuna kura nyingi sana ameiba.

Pole yake Mzee Odinga amisha andikiwa fungu LA kukosa,miaka yote anaibiwa kura-hamna mgombea aliyewahi kumshinda kwa kura lakini ndio hivyo hana bahati.
Acha kukariri ndugu yangu.
Hakuna kituo hata Kimoja cha kupigia kura Kenya kilichokuwa na wapiga kura wanaofikia elfu kumi. Kituo chenye wapiga kura wengi sana hakiwezi kuzidi watu elfu mbili. Hiyo issue ya kura elfu kumi za Ruto zilizoondolewa kwa kuwa sio kura halali zilikuwa kwenye fomu (hardcopy) ya majumuisho ya vituo vya eneo fulani, na ilikuwa submitted error (ama kwa makusudi au bahati mbaya) lakini wahusika waliweka wazi kuwa ni kosa na likasahihishwa.
 
Wameshindwa kuleta hoja za msingi, dada cheupe hapendi maswali, ameulizwa unayakataa matokeo je unayo ya tofauti? hana..ameulizwa mwenyekiti chibukati si ndo mwenye mandate ya kuyatangaza? ndioo..anasema matokeo walitaka wayadiscuss..kudiscuss ili iweje? uyaedit au..
Sasa mbona huwa tunalalamika hapa NEC ikitangaza matokeo.Kumbe huwa hatuna hoja pia.
 
Hata kama idadi amekosea lakini hizo hizo kura 1400 bado zina invalidate the whole results.
Kwa hiyo unataka kusema nini?
Hivi ulishawahi kushiriki moja kwa moja kwenye uchaguzi kama msimamizi, wakala au muangalizi ukaona majumuisho ya kura yanavyofanyika na namna wanavyotatua kasoro zozote za kimahesabu?

Wewe umeshaambiwa wazi kuwa hiyo 0.01% (kura 1400) kiuhalisia haipo, ni zao la summation approximated numbers.

Okay, basi tuseme ni kura zilizozidi, kwanini suluhisho liwe kufuta uchaguzi wote?

Hivi katika mazingira ya uchaguzi yenye vituo zaidi ya 4600, kunaweza kukaibuka errors, blunders, miscalculations na misconduct ngapi?
Kama kila kasoro itakayoibuliwa kwenye uchaguzi suluhisho liwe kuufuta uchaguzi wote, tutarejea kurudia uchaguzi mara ngapi?
 
NEC hivi wanaweza kutoa kasoro kwenye uchaguz wa mgombea wa ccm

Ova
Thubutu,na hapa mpaka tunaanzisha nyuzi lukuki ni kwa ajili ya uwazi wa mambo yanavyoendeshwa Kenya mpaka tumekuwa na jeuri ya kuwakebehi hao Makamishina.Hapa kwetu hata nguvu ya kuanzisha tu hizo mada za kukosoa huwa hatuna.
 
Back
Top Bottom