Ndugu umeibua mada nyingine tena. Nimekuwa nikiangalia makala mbalimbali za video na nimeona kuna ukinzani wa hoja kwa watu wanaotamani kuishi maisha yanayoshabihiana na mazingira asili na watu waliochagua kuishi maisha ya ustaarabu wa kisasa, maisha ya mjini yanayotegemea bidhaa mbalimbali za kununuliwa ambazo zinatokana na kubadili/kuharibu mazingira asilia.
Ubaya ni kwamba primitive civilization ilipunguzwa nguvu na kuonekana kwamba 'haifai' ili kuingiza mfumo mpya wa maisha uliosababishwa na mapinduzi ya viwanda. Na hii ndio modern civilization ambayo watu wengi wanaipenda, wanatoka vijijini kwenye maisha ya asili na kwenda mjini kwenye maisha ya 'uharibifu' ya kisasa.
Wengi wetu tunatamani kuishi kwenye nyumba ya kisasa, gari nzuri, kusoma elimu inayosaidia kukidhi na kukuza modern civilization n.k; yote haya yanahitaji pesa na kwa kuwa mtindo wa maisha umebadilika si wa kale tena basi yatupasa kufanya shughuli inayoleta mantiki kiuchumi.