Makampuni 49 ya Tanzania yaruhusiwa kuuza maharage soya China

Hili ni jambo jema, ila elewa kuwa maharage ya Soya (Soy beans) yana ushindani mkubwa sana kutoka marekani na Brazil. Yale ya marekani yana ubora wa hali ya juu sana kutokana na namna wanavyoendesha kilimo chao, ila serikali ya Trump ilichapochafuana na wachina kwa kuwekeana tarrifs za kujinga kijinga, wachina wao wakaamua kukomesha wakulima wa Marekani ambao walikuwa supporter wakubwa wa Trump kwa kuyawekea tariff kubwa maharage hayo pia iliyosababisha watumiaje kuacha kuyanunua kwa wingi, wakahamia yale ya Brazil. Uhusiano baina ya Marekani ukitengamaa watayarudia tu, hivyo soko la Soya la uchina siyo la kutegemea kwa muda mrefu labda tubadilishe sana kilimo chetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…