Makampuni ya China yatoa nafasi za ajira zaidi ya 500 kwenye maonesho ya ajira ya Chuo Kikuu cha UDSM

Makampuni ya China yatoa nafasi za ajira zaidi ya 500 kwenye maonesho ya ajira ya Chuo Kikuu cha UDSM

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
1728608849095.png


Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kikishirikiana na Taasisi ya Confucius, hivi karibuni kiliandaa Maonesho ya tatu ya Ajira kati ya China na Tanzania baada ya maonesho hayo kusita kwa takriban miaka sita kutokana na changamoto kama vile janga la UVIKO-19. Baada ya kurejea kwake sasa maonesho hayo yanawapatia tena wanafunzi na wahitimu wa vyuo vikuu mbalimbali nchini Tanzania fursa ya kukutana na waajiri watarajiwa.

Tukio hili adhimu linalenga kuimarisha uhusiano kati ya China na Tanzania kwa kukuza mawasiliano ya kiutamaduni na ushirikiano. Pia linaunga mkono juhudi za serikali ya Tanzania kukabiliana na ukosefu wa ajira nchini kwa kuwaunganisha wahitimu wenye ujuzi na makampuni yanayoongoza, pamoja na kutoa fursa za uwekezaji.

Kwa wale waliohudhuria maonesho hayo ya ajira ilikuwa ni fursa nzuri sana ya kukutana na waajiri wa makampuni makubwa, kuangalia ofa za kazi, na kujipatia ajira.

Maonesho hayo yaliyovutia zaidi ya makampuni 100 ya China nchini Tanzania, yalishuhudiwa yakitoa nafasi za ajira zaidi ya 500 katika sekta mbalimbali. Akiongea kwenye maonesho hayo, mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa China nchini Tanzania, Bw Shi Yong, alisisitiza faida za muda mrefu za uwepo wa wafanyabiashara wa China nchini Tanzania, hasa katika kutoa fursa za ajira za moja kwa moja kwa Watanzania.

Nia njema ya China ya kuhakikisha kuwa nchi mbalimbali za Afrika zinaendelea kunufaika pakubwa kwa sasa inaonekana dhahiri.

Na hii ni kuanzia kutoa udhamini wa masomo katika vyuo mbalimbali vya China na nchi wenyeji, hadi kutoa nafasi nyingi za ajira, ambapo nchini Tanzania makampuni ya China yameazimia kuhimiza ukuaji endelevu wa soko la ajira na kuhakikisha kuwa Watanzania wananufaika moja kwa moja na uwepo wa makampuni haya.

China na Tanzania zina historia ndefu ya ushirikiano katika masuala ya elimu, biashara na maendeleo.

Kwa maana hiyo maonesho kama haya ya ajira yanaonesha dhamira endelevu ya mataifa yote mawili ya kushirikiana pamoja kwa ajili ya maendeleo katika sekta zote na pia kuondoa changamoto ya ukosefu wa ajira inayowakabili vijana wengi wa Tanzania na kutoa jukwaa muhimu kwa baadhi yao kubadilika kutoka watafuta ajira hadi kuwa waajiriwa.

Ikumbukwe kuwa ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa ILO kuhusu mtazamo wa ajira na kijamii imeonya juu ya kuongezeka kwa ukosefu wa ajira duniani kwa mwaka huu wa 2024, sambamba na pengo la usawa na kudumaa kwa kiwango cha uzalishaji hali ambayo inaibua wasiwasi. Hivyo mchango wa makampuni ya China katika kuwapatia ajira vijana nchini Tanzania, utaiondolea wasiwasi na mzigo mzito serikali ya Tanzania, na pia kutoa afueni kubwa katika kukabiliana na changamoto hii ya ukosefu wa ajira.

Makampuni haya ya China mbali na kutoa nafasi za ajira pia yanajitahidi kuwaandaa vijana wanaosoma katika vyuo vikuu vya Tanzania ili baadaye waje kuwa waajiriwa wenye ujuzi kamili kwa kuwapatia udhamini wa masomo. Chini ya makubaliano ya udhamini huo, wanafunzi wanaodhaminiwa na makampuni ya China watafaidika kwa kupewa fursa ya kwenda kufanya mazoezi ya kazi katika kampuni za China nchini Tanzania na baada ya kuhitimu kuweza kuajiriwa.

Ushirikiano huu mkubwa kati ya China na Tanzania umeleta matokeo chanya katika nyanja mbalimbali za maendeleo ya uchumi wa Tanzania, na pia kuleta manufaa yanayoonekana waziwazi kwa Watanzania, ikiwemo elimu, ajira na hata kupata ujuzi mbalimbali katika sekta za kilimo, biashara na teknolojia.

Kwa mujibu wa ripoti ya Taasisi ya Utafiti na Kupunguza Umasikini Tanzania (REPOA) ya mwaka 2019, takribani vijana milioni moja wanahitimu kila mwaka katika taasisi mbalimbali za kielimu, huku idadi ya ajira zinazozalishwa kutoka serikalini na sekta binafsi ikiwa ni 250,000, na kwa wastani kila mhitimu anatumia miaka 5.5 kupata ajira.
 
Back
Top Bottom