Makampuni ya Mawasiliano yaboreshe vifurushi viwe rafiki kwa ajili ya viziwi

Makampuni ya Mawasiliano yaboreshe vifurushi viwe rafiki kwa ajili ya viziwi

MLUGURU

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2012
Posts
2,929
Reaction score
3,710
TCRA pamoja na haya makampuni ya simu ya Tanzania (Tigo, Vodacom, Halotel, Zantel, Airtel,ttcl), miongoni mwa wateja wenu kuna hawa wenye mahitaji maalumu ambao ni viziwi kiasili. KIZIWI maana yake ni mtu ambae hawezi kuwasiliana kwa namna yoyote ile kwa njia ya sauti zaidi ya video call na sms.

Ombi langu kwenu wadau wakubwa kabisa wa tasnia hii ya mawasiliano nchini ni kuweza kuboresha vifurushi vyenu ili hawa ndugu zetu nao waweze kunufaika.

Kwa mfano ukiangalia vifurushi vingi ni vya internet tupu, na vingine ni vya muda wa maongezi pamoja sms ambavyo hivi vingeboreshwa vipatikane vifurushi maalumu vya internet pamoja sms ambavyo ni familia kabisa kwa watu wenye uziwi maana dakika za maongezi kwao sio sehemu ya matumizi kabisa.

Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom