KERO Makampuni ya ujenzi wa barabara yanaharibu mazingira kwa uchimbaji holela wa Moramu-Ilemela

KERO Makampuni ya ujenzi wa barabara yanaharibu mazingira kwa uchimbaji holela wa Moramu-Ilemela

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kumekua na tabia ambayo imeota mizizi kwa makampuni ya ujenzi kuchimba udongo wa moramu kwa ajili ya ujenzi wa barabara na kuaacha mashimo ambayo ni hatari kwa maisha ya binadam na uharibifu wa mazingira.

Makampuni haya ya ujenzi baada ya kuchimba molamu kwa ajili ya ujenzi wa barabara mradi unqpoisha uwa hawafukii mashimo waliyochimba kwa ajili ya molamu hivo kusababisha uharibifu wa mazingira.

Jambo ili limekua sugu katika wilaya ya Ilemela hasa katika maeneo yalio pembezoni mwa mji hasa kata za buswelu,shibula,bugogwa na Sangabuye.

Makampuni haya yamekua hayana plan ya kuyafukia mashimo hayo mara miradi inapokamilika hvo kulrta athari hasi kwa mazingira na jamii zinazozunguka maeneo hayo.

Madhara yq uchimbaji wa mchanga na molamu holela ni makubwa ikiwemo watu au mifugo kudondokea kwenye makorongo, wakati wa masika mashimo yanatuamisha maji hvo kua chanzo cha mazalia ya mbu na kuhatarisha maisha ya watoto ambao wanayachezea maji hayo machafu.

Wito wangu ni serikali ya halmashauri kuweka mkakati wa kuyabana haya makampuni wawe na mitigation strategies dhidi ya uchimbaji wa udongo holela na ikiwezekana kila anaechimba akimaliza mradi wake basi wayafukie mashimo haya.

Pia nashauri NEMC mwanza ambao ndip wasimamizi wa mazingira wache kukaa ofisini waje mitaani waone jinsi gani watu wanavoharibu mazingira bila kuchukuliwa hatua.

IMG_2482.jpeg
IMG_3708.jpeg
IMG_2481.jpeg
img_3710-jpeg.3316282
IMG_3698.jpeg
IMG_0808.jpeg
 

Attachments

  • IMG_3710.jpeg
    IMG_3710.jpeg
    328.4 KB · Views: 67
Back
Top Bottom