Makampuni ya Utalii na Hoteli za Kitalii

Makampuni ya Utalii na Hoteli za Kitalii

MPadmire

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Posts
3,957
Reaction score
3,245
Hali si shwari, Corona virus imeleta madhara makubwa katika sekta ya utalii

A - Hakuna biashara na hakuna nafuu katika miezi 3 ijayo

B - Wafanyakazi wengi sana wamepewa likizo bila malipo

C - Serikali kukosa mapato (Park entry fees $$$ £££) foreign money kwa kiasi kikubwa

D - Je, bado TRA inawadai Kodi Hoteli na Makampuni ya kitalii?

Kuna haki ya kukamua maziwa kutoka kwa Ng'ombe mwenye njaa?

Ombi kwa Mheshimiwa Waziri na Rais wetu

TRA - wasamehe Corporate tax kwa miezi 3

Wafanyakazi wa Sekta ya utalii (Private sekta) wapewe Robo ya akiba yao katika kipindi hiki cha mpito.

Lingine: Wizara ya Mali asili na utalii na TTB, wabuni mikakati ili kukabili Kipindi kigumu cha uchumi Duniani. Watalii watakuwa hawana pesa za kutosha...Kupunguza gharama za kutembelea Tanzania. Nashauri yafuatayo

A - Kupunguza JET fuel (kupunguza bei mafuta ya ndege)

B- Kupunguza landing fee ya ndege

C- Kupunguza VAT kutoka 18 hadi 12% kwenye park fee za mbuga za wanyama

D - Kupunguza Park fee kwenye mbuga za wanyama

E - LOdges kupunguziwa kodi ili na wao wapunguze room price

F - Kupunguza VISA fee

G - Kukaa na Private sector (Hotel na Kampuni za utalii) na kusikiliza Maoni.

Waziri Kigwangala alifanya vizuri sana kukaa na wadau pale mwanzoni na kusikia maoni. Waziri asichoke.

Wabunge pia waishauri serikali.

Wana JF, mnakaribishwa kwa maoni.

Uzalendo mbele kwanza..
 
Corporate tax inakuwa baada ya faida hivyo kama wanapata hasara muda huu then hawatachajiwa
 
NSSF watoe kiasi fulani cha akiba kwa kila mfanyakazi wa Private sekta (utalii) ili waweze kujikimu.

Mkoa wa Arusha utoe ushauri kwa Wenye nyumba, ili wapunguze Kodi au watoe unafuu, labda kulipa baadae.

Kama Serikali itaona umuhimu kutazama LUKU na bili za maji
 
Mzee Baba wa Chato alikataa kuweka Dar kwenye lockdown huku akihofia kupoteza mapato ya serikali! Sasa hii hoja ya kupunguziwa Kodi nk kweli ataikubali??

Halafu hata kama tukifuta ada zote, haitawaleta watalii, kwa sababu nchi zao zimekataza raia wao kusafiri nje!

Airlines zote zinahofia kufilisika kwa sababu ya kukosa abiria, na wameshaanza kupunguza wafanyakazi.

Samahani kwa kuwa pessimistic wa kupitiliza. Lakini kwa miezi zinazokuja tujaribu kuhamasisha utalii wa ndani, na hapo pengine mapunguzo ya gharama yanaweza kusaidia!
 
Utalii umeshajifia. Labda baada ya miaka 2 ndio hali itarudi kama kawaida. Dunia imefungwa, karibu nchi zote duniani zimefunga airport. Na huko wanakotoka watalii nchi nyingi zilikuwa lock down.

Kazi nyingi zilisimama, hivyo watu wengi kwenye hizo nchi walitegemea ruzuku toka kwenye serikali zao ili kuishi. Shughuli za kiuchumi kwenye hizo nchi kurudi katika hali ya kawaida labda ni mwisho wa mwaka.

Hapo hapo itategemea na vipato vya watu baada ya Corona kwisha kwenye hizo nchi, na hali ya ugonjwa wa Corona Africa itakuwaje, maana imeshaonekana tunaficha takwimu halisi za ugonjwa,.

Kuja kutalii Africa mara nyingi inamchukua mtu si chini ya Miezi 6 hadi mwaka kupanga safari, maana kuja kutalii Africa ni gharama kubwa kulinganisha na kutalii ndani ya ulaya au kwenda sehemu kama Dubai.
 
Sekta ya utalii nadhani labda itaimarika mwakani 2021,sababu hizi hapa:

Mosi-Idadi kubwa ya watalii ambao wengi ni wazungu/ mabeberu wengi wao ambao ni wazee huenda wamefariki.

Pili-Kipato chao wengi kimepungua kwa sababu ya corona hakuna uzalishaji,baada ya corona nchi zao zitajiimarosha kiuchumi halafu uchumi wa mtu mmoja mmoja utaimarika.

Tatu-Transparency and accountability
 
Sekta ya utalii nadhani labda itaimarika mwakani 2021,sababu hizi hapa:

Mosi-Idadi kubwa ya watalii ambao wengi ni wazungu/ mabeberu wengi wao ambao ni wazee huenda wamefariki...
Kwa hiyo unamaanisha hadi hawa wa umri wa kati watakapozeeka ndipo watakapoanza kuja kutalii Afrika siyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mdau wa utalii huko Ars kaniambia wanategemea kukutana na Uongozi wa juu wa Serikali kujadili suala hili likiwemo pia la self isolation for 14 days liondolewe na Serikali mara watakapoanza kuja kwa mara nyingine. Tusubiri tuone watakuja na majibu gani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom