Makamu Mwenyekiti THBUB: Hali ya haki za binadamu nchini inaendelea kuimarika kutokana na uelewa wa watu kuongezeka

Joined
Sep 17, 2024
Posts
21
Reaction score
16
Akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Salmin Amour iliyopo katika Manispaa ya Singida hivi karibuni Makamu Mwenyekiti Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Mhe. Mohamed Khamis Hamad, alisema, hii ni kutokana na watu kuwa na uelewa wa kuibua masuala ya uvunjifu wa haki za binadamu.

"Watu wanaibua masuala mbalimbali yanatokea katika jamii lakini pia Serikali inachukua hatua stahiki kuhakikisha kuwa haki za watu zinalindwa" amesema Mhe. Mohamed

Aidha, Mhe. Mohamed aliongeza kuwa THBUB inaendelea na jukumu la kutoa elimu kwa jamii na kufanya uchunguzi kwa lengo la kuzuia vitendo vya kikatili.

Katika hatua nyingine, Mhe. Mohamed ametoa wito kwa Wazazi kukomesha vitendo vya kikatili kwa Watoto ili kuendelea kulinda haki za mtoto.

Naye Mwalimu, Veronica Emmanuel ametoa shukrani kwa THBUB kwa kutembelea na kutoa elimu kwa wanafunzi na Walimu wa Shule hiyo kwani elimu hiyo itawasaidia Wanafunzi na Walimu kujua haki na wajibu wao ili waweze kujisimamia nakufanya maamuzi sahihi hususan pale wanapokutana na vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora
 
Kwa hawa watu wanaopotea/kutekwa inakuwa inawagusa nyie au ni Polisi?
 
Mkuu hujasoma kilichopo ndani kabisa, maana ungekuwa ushaona kirefu chake🌚🌚🌚

Hata kwenye ID yao kirefu na kifupi vyote vimeandika😂😂
Nilikua na mashaka na ile UB ya mwisho. Kumbe Utawala Bora 😆😆😆
 
Back
Top Bottom