TANZIA Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad afariki dunia

TANZIA Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad afariki dunia


Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar na Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Maalim Seif amefariki ktk Hospitali ya Muhimbili. Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi ametangaza siku 7 za maombolezo ya Kitaifa

Pia soma > Wasifu/ CV ya Maalim Seif Sharif Hamad, Historia yake kwa Ufupi

Kupitia ukurasa wa Twitter, Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli atoa salamu za rambirambi pamoja na kutangaza siku tatu za maombolezo Kitaifa.

"Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar. Natoa pole kwa Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Mwinyi, Familia, Wazanzibari, wanachama wa ACT-Wazalendo na Watanzania wote. Mungu amweke mahali pema peponi,Amina"


Pia soma > Zanzibar 2020 - Uchambuzi Urais Zanzibar 2020: Nafasi ya Maalim Seif Sharif Hamad
View attachment 1704550
Maalim Seif alizaliwa kutokana na familia ya wakulima wa kijiji cha Mtambwe, nje kidogo ya mji wa Wete, Pemba, katika Oktoba 22, 1943, Maalim Seif alivuka bahari ya mkondo wa Pemba kuja Zanzibar kuendelea na masomo ya sekondari kutoka 1958 hadi 1963.

Hakuweza kuendelea na masomo ya chuo kikuu pale alipotakiwa aende kusomesha katika shule za sekondari ili kujaza mapengo yaliowachwa na walimu wengi wa Kiingereza na wachache wa kizalendo baada ya Mapinduzi ya 1964. Wakati ule siasa kali za utawala wa mkono wa chuma ulishuhudia serikali ikitaifisha vikataa vidogo vya mashamba na nyumba za makazi za watu walioonekana maadui wa Mapinduzi ziliipelekea Zanzibar kuelezwa na nchi za Magharibi kama Cuba ya Afrika Mashariki.

Hata hivyo, alifanikiwa kuchukua shahada ya kwanza ya Elimu, Sayansi ya Kisiasa na Uhusiano wa Kimataifa´kutoka mwaka 1972 hadi 1975 na aliporudi Zanzibar alichaguliwa msaidizi maalum wa Rais wa Zanzibar mpaka mwaka 1977 alipochaguliwa Waziri wa Elimu.

Katika medani ya siasa Maalim Seif alichaguliwa mjumbe wa Halamshauri Kuu ya Taifa ya CCM ambayo aliitumikia kwa miaka 11. Katika mwaka 1984 kufuatia kile kilichojulikana kama kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa Visiwani kulikoshuhudia kulazimishwa kustaafu kwa aliyekuwa Rais wa pili wa Zanzibar, Sheikh Aboud Jumbe, Maalim Seif alichaguliwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Lakini kauli zake za uwazi za mara kwa mara za kuonyesha hafurahishwi na mwenendo mzima wa Muungano na kueleza Zanzibar haitendewi haki kwa baadhi ya mambo ndani ya Mungano kuliepelea kutimuliwa katika chama na pia kupoteza wadhifa wa Waziri Kiongozi kufuatia hatuahio ya chama.

Tokea wakati huo aliandamwa kwa kuonekana tishio la kisiasa na mwaka 1989 alifunguliwa mashitaka bandia ya kupatikana na nyaraka za siri za serikali. Alikaa miaka miwili gerezani, baadhi ya wakati katika chumba akiwa peke yake kwa muda unaoweza kufikia wiki mbili mpaka alipoachiwa na Mahakama ya Rufaa ya Tanzania kwa kuwa hakuwa na kesi ya kujibu.

Tanzania ilipofungua milango yake na kuruhusu mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992, Maalim Seif na baadhi ya wenzake aliofukuzwa nao Halmashauri Kuu ya CCM walikuwa miongoni ma walioanzisha Chama chaWananchi (CUF) na kuwa Makamo Mwenyekiti wake wa kwanza

Aligombea Urais wa Zanzibar katika uchaguzi wa kwanza wa mfumo wa vyama vingi mwaka 1995, mwaka 2000, 2005, 2010,2015 na 2020, Alishindwa kwa kura chache, lakini mwenyewe amekuwa akiamini alishinda chaguzi zote hizo na aliporwa ushindi kwa sababu Tanzania na hasa Zanzibar haijakuwa tayari kupokea mfumo wa demokrasia kwa moyo safi.

Mnamo tarehe 18 machi 2019 maalim self alitangaza kujiunga na chanma cha ACT wazalendo baada ya kutokea kutokuelewana na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof Ibrahim Lipumba katika Mgogoro uliwafikisha Mahakani na Upande wa Seif Ukashindwa kesi.

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi alimteua Dec 07, 2020 Mwenyekiti wa Chama cha ACT- Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad kuwa makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar. Uteuzi uliozingatia matakwa ya kifungu cha 9(3) cha katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kinachosomeka kwamba, muundo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar utakuwa wa Umoja wa Kitaifa na utendaji wa kazi zake utafanywa katika utaratibu utakaohakikisha kuendelezwa kwa umoja nchini na lengo la kufikia demokrasia.

Hadi mauti unamkuta, Maalim Seif Sharif Hamad alikuwa makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar na Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa.

Tarehe 31 Januari 2021 chama chake cha ACT Wazalendo kilisema kuwa wasaidizi kadhaa wa Bw Maalim Seif wamepatwa na maambukizi ya virusi vya corona. Pia kiliwafahamisha wanachama wake, Wazanzibari, pamoja na umma wa Watanzania kuwa mwenyekiti wake Maalim Seif Sharif Hamad na mkewe Bi Awena, wamethibitika kupata maambukizi ya Covid 19. Taarifa hiyo iliendelea kusema kwamba


''Katika hali ya kuchukua tahadhari zaidi madaktari walimshauri Maalim Seif kuwa ni vyema awepo chini ya uangalizi maalum katika kipindi chote atakachokuwa anaendelea na matibabu'', ilisema taarifa ya ACT Wazalendo. Maalim Seif alipumzishwa katika Hospitali ya Mzazi Mmoja, Unguja.

Zaidi soma; Zanzibar: Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad, Mkewe Bi Awena waambukizwa virusi vya Corona

Apumzike kwa Amani

---
PICHA

View attachment 1704565
Maalim Seif na Mwalimu Nyerere nyumbani kwa Mwalimu (The Clinic) Msasani

View attachment 1704567
Vipande vya picha mbalimbali vikionesha harakati za Maalim Seif

View attachment 1704569
Maalim Seif na Salmin Amour mwaka 1999 baada ya Mazungumzo ya Mwafaka

Tujikumbushe ahadi zake Uchaguzi 2020

View attachment 1704645
korona zaidi mwezi?!!!!
 
Katiba ya Zanzibar inasemaje?
ACT watatoa mtu wa kumReplace Maalim au ndio nitolee?
 
Apumziike pema mwendazake... Naona shavu la umakamu linaweza muangukia jussa, au duni
 
Kweli corona ipo ila nilichogundua ikikupata usikimbilie hospital we kaa kwako upige nyungu za kutosha kama alivyofanya jiwe

..kuna corona ya kukaa nyumbani, na kuna corona ya kukimbilia hospitali.

..kuna watu vijana kuliko Maalim Seif lakini corona imewasumbua zaidi ya mwezi hawajakaa sawa.
 
Sijui alikwenda kufanya nini Chato.Huko ndo chanzo cha kifo chake. R.I.P Maalim. Hatimae upinzani Zanzibar nao umezikwa.
Iloboye kwa sie tulioishi Zanzibar Seifu alikuwa kama Mtume. Upinzani umefutika rasmi bara na Visiwani naamini upande ule unatoa machozi ya mamba tu. Corona ipo dada yangu nina maboss wangu huko wameponea chupuchupu Aghakan
 
Mwanasiasa aliyehimili vishindo vingi yawezekana kuliko wanasiasa wote walio hai Tanzania.Hakufa kwa sababu yoyote mpaka siku na saa yake ilipofika.
Alipenda sana kuzika wenzake kwa utulivu kabisa na imani.Na yeye azikwe kwa namna hiyo hiyo.
 
20210217_200207.jpg

My deepest condolences to the family, ACT-Wazalendo, the Zanzibari nation and Tanzanians on the sad passing of Maalim Seif Shariff Hamad. Maalim Seif was the most influential leader and fearless defender of the Zanzibari people and their national aspirations. May he Rest In Peace https://t.co/zjcaMVhLeg
 
Ofisi ya makamu wa pili wa Rais Zanzibar imesema maalimu Seif rip atazikwa kesho kijijini kwao huko Pemba.

Mwili wa maalimu Seif utaondolewa hospitali ya Lugalo kesho saa 4 asubuhi na kuswaliwa katika msikiti wa Upanga kabla ya kusafirishwa kwenda Unguja saa 5 asubuhi.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Unamatatizo makubwa Sana ambayo hujui kama unayo
Ila amesema ukweli,Kuna watu wakipata Corona kumpeleka hospital ni matumizi mabaya ya resources maana hawezi toboa na nchi hii wapo wengi.Hata hao wenye viburi siku ukisikia wamepata,ndo bye bye hiyo
 
View attachment 1704854
My deepest condolences to the family, ACT-Wazalendo, the Zanzibari nation and Tanzanians on the sad passing of Maalim Seif Shariff Hamad. Maalim Seif was the most influential leader and fearless defender of the Zanzibari people and their national aspirations. May he Rest In Peace https://t.co/zjcaMVhLeg
Hapa hakuwa nayo,aliipata kwenye hizi trip za hapa na pale baada ya watu fulani kuamua kujitoa ufahamu na kutumia nafasi zao vibaya kuwatoa watanzania masikini ufahamu kwamba nchi hii hakuna corona
 
Hapa hakuwa nayo,aliipata kwenye hizi trip za hapa na pale baada ya watu fulani kuamua kujitoa ufahamu na kutumia nafasi zao vibaya kuwatoa watanzania masikini ufahamu kwamba nchi hii hakuna corona
Maalimu Seif akikuwa masikini?

Kwani chama chake cha ACT kilikubali kwamba corona haipo?

Je, wakati anazunguka kupiga kampeni alikuwa anachukua tahadhali yeyote?
 
Back
Top Bottom