benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Leo nimefuatilia mahojiano aliyoyafanya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Othman Masoud Othman kupitia kipindi cha Clouds360 cha Clouds TV na nimbaki na maswali mengi kuliko majibu
Othman Masoud Othman amewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar kabla ya kung’olewa kwa kile kinachosemwa chinichini kuwa ni kusimamia msimamo wake wa kudai Serikali tatu.
Katika mahojiano ya leo, Othman bado ameendelea na msimamo wake wa kudai serikali tatu. Ni jambo jema kuwa bado ana msimamo uleule na leo emesema wazi kuwa mfumo wa Serikali mbili una kasoro lakini swali langu ni:
Je kwanini anaendelea kuhudumu akipata stahiki zote, posho na mishahara katika Serikali ambayo iko na ushirika (muungano) na Serikali Mama ambayo haamini muundo wake?
Kwa kuwa sasa yupo ndani ya Serikali (japo tunaelewa ni ceremonial) je anafanya nini kutetea anachoamini?
Je tukisema kwa maneno anataka Serikali tatu lakini kwa matendoo ya kila siku anaishi na kuitumikia Serikali mbili nitakuwa nimekosea?
Katika mahojiano amegusia masuala mengi zaidi ikiwemo mahusiano yake na Rais Mwinyi, Uhitaji wa Katiba Mpya na mengine kadha wa kadha lakini mimi bado nina maswali mengi kuliko majibu.
Kama una muda bofya hapa utazame sehemu ya aliyoyasema