Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maswali Mengi Majibu Machache

Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maswali Mengi Majibu Machache

Maana Muungano tuupe mkono wa kwaheri
 
Leo nimefuatilia mahojiano aliyoyafanya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Othman Masoud Othman kupitia kipindi cha Clouds360 cha Clouds TV na nimbaki na maswali mengi kuliko majibu

Othman Masoud Othman amewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar kabla ya kung’olewa kwa kile kinachosemwa chinichini kuwa ni kusimamia msimamo wake wa kudai Serikali tatu.

Katika mahojiano ya leo, Othman bado ameendelea na msimamo wake wa kudai serikali tatu. Ni jambo jema kuwa bado ana msimamo uleule na leo emesema wazi kuwa mfumo wa Serikali mbili una kasoro lakini swali langu ni:

Je kwanini anaendelea kuhudumu akipata stahiki zote, posho na mishahara katika Serikali ambayo iko na ushirika (muungano) na Serikali Mama ambayo haamini muundo wake?

Kwa kuwa sasa yupo ndani ya Serikali (japo tunaelewa ni ceremonial) je anafanya nini kutetea anachoamini?

Je tukisema kwa maneno anataka Serikali tatu lakini kwa matendoo ya kila siku anaishi na kuitumikia Serikali mbili nitakuwa nimekosea?

Katika mahojiano amegusia masuala mengi zaidi ikiwemo mahusiano yake na Rais Mwinyi, Uhitaji wa Katiba Mpya na mengine kadha wa kadha lakini mimi bado nina maswali mengi kuliko majibu.

Kama una muda bofya hapa utazame sehemu ya aliyoyasema

View attachment 2274424

Huyu ndiye mtanzania anayetakiwa kwenye utawala! wa leo!
The guys has been bold and still bold standing by his values!!
Hivi kuna mtu akiingia kwenye siasa anabadilika kama likinyonga! Hivi ndivyo vianzo vya shida zetu!
Huyu jamaa alikataa laiv bungeni miswada ya kishenzi na Ali shein akamfukuza UAG wa zenj.
Mawazo yake ndiyo mawazo ya chama chake!
Hivi ukimsikiliza Kabudi wa katiba mpya na Kabudi wa sasa (jalalani) utamuelewa?
Je pole pole?
Viko vimtu kama vimsigwa vikipata ahadi kidogo vinageuka hata kabla ya utekelezaji.

Huyu mtu na wenye misimamo kama huyu ni wa kuenzi!! Go Bro Goo
 
..Na Tanganyika.

..Hivi Huseni ni wa kumshinda Maalim Seif ktk uchaguzi huru?
Hata kwenye kuteua mgombea. Kama wazanzibari wa ccm wangeachiwa wateue mgombea wao wenyewe, Hussein asingepata hata nafasi ya 5.

Hili la kuwateulia mgombea ni moja ya kero kuu kwao.

Kwa upande mwingine; kama kutakuwa na katiba mpya, chama cha upinzani kitakachokubali katiba ya serikali mbili kitakuwa kimewasaliti wananchi.
 
Katika mahojiano ya leo, Othman bado ameendelea na msimamo wake wa kudai serikali tatu. Ni jambo jema kuwa bado ana msimamo uleule na leo emesema wazi kuwa mfumo wa Serikali mbili una kasoro lakini swali langu ni:

Je kwanini anaendelea kuhudumu akipata stahiki zote, posho na mishahara katika Serikali ambayo iko na ushirika (muungano) na Serikali Mama ambayo haamini muundo wake?
Mkuu benzemah, kwanza asante sana kwa uzi huu, akina sie tulimsikia kitambo na Kumuita ni mmwaga sumu na tukashauri Dr. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii
Kwa kuwa sasa yupo ndani ya Serikali (japo tunaelewa ni ceremonial) je anafanya nini kutetea anachoamini?
ACT ndani ya SUK wanatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM, hivyo there is nothing he can do!
Je tukisema kwa maneno anataka Serikali tatu lakini kwa matendoo ya kila siku anaishi na kuitumikia Serikali mbili nitakuwa nimekosea?
No hujakosea na hakuna ubaya wowote kwa mtu yoyote ku wish lolote mfano mimi napenda serikali moja lakini naitumikia serikali mbili kikamilifu.
Katika mahojiano amegusia masuala mengi zaidi ikiwemo mahusiano yake na Rais Mwinyi, Uhitaji wa Katiba Mpya na mengine kadha wa kadha lakini mimi bado nina maswali mengi kuliko majibu.

Kama una muda bofya hapa utazame sehemu ya aliyoyasema

View attachment 2274424
Ila pia huyu ndiye rais wa Zanzibar ajaye 2025 kama hii sauti niliyoisikia ni kweli Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, Sauti Imeshauri Mama Amkabidhi Kwanza Dr. Mwinyi, Urais wa JMT, Ndipo Aje Mwanamke!
P
 
Sasa kiongozi, unajua kabisa serikali iliyopo inaongozwa na CCM, kwani kuna ubaya gani yeye akiendelea kuamini na kuelezea kile anachokiamini kwa njia ya amani?

Unajua kabisa kule Zanzibar kuna muafaka, sasa unataka atoke kwenye serikali ya umoja wa kitaifa ndio aanze kuipigania katiba ya serikali tatu? Akishatoka na chama chake maana yake si ndiyo kuleta chokochoko?

Maoni yangu naona yupo sawa kutoa maoni yoyote ambayo si matusi.
 
Othman Masoud huyu ni mwanasheria pia kwa sasa ni kiongozi(makamo wa kwanza wa rais SUK) katiba ya zanzibar inasema serikali ya kitaifa (ushirikiano kati ya chama kiloshinda na wapili kwenye uchaguzi) huyu hajaomba kuwa makamo wa kwanza Bali chama chake kimemteua kuchukuwa hio nafasi. Yupo kwenye nafasi ya kuteuliwa kwa mujibu wa katiba lakini chama na msimamo wake upo palepale juu ya uono wake sio uono wa serikali aliopo. Siasa kama dini unaweza kuwa muislam au mkristo lakini ndani ya hizi dini kuna madhehebu yake na tofauti zake.

Kukuuuu [emoji239][emoji239][emoji239]
[emoji109][emoji123]
 
Ndo ujinga wako huo watu hatukimbii matatizo tunapambana nayo ili kukabili yenyewe na vyanzo vyake wewe vipi bwana
 
Back
Top Bottom