Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar: Acheni kuchukua fedha ili muwafiche wanaowafanyia ukatili Watoto na Wanawake

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar: Acheni kuchukua fedha ili muwafiche wanaowafanyia ukatili Watoto na Wanawake

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Snapinsta.app_470339380_1270599784140057_6250585693664628496_n_1080.jpg

Snapinsta.app_470095010_1209032934124108_4317542864764801050_n_1080.jpg
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema hatua zaidi zinatakiwa kuchukuliwa dhidi ya matukio ya Ukatili hasa kwa Watoto na Wanawake na pia Jamii imetakiwa kutoa ushirikiano zaidi kwa Mamlaka zinazohusika kukabiliana na changamoto hiyo.

Hayo yameleza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Taifa ya Mtoto Ni Mboni Yangu iliyofanyika Desemba 14, 2024 katika Mkoa wa Mjini Magharibi chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Taasisi ya Ndoto Ajira ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla.

Marathon ya Mtoto Mboni Yangu imeambatana na utoaji zawadi kwa washindi walioshiriki mbio za Kilomita 5 na Kilomita 10 pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Uzinduzi huo ulienda sambamba na ushiriki wa Marathon iliyoshirikisha zaidi ya Washiriki 20,000 kutoka Bara na Visiwani iliyofanyika Forodhani, Zanzibar.

Viongozi mbalimbali walishiriki mbio hizo pamoja na Washiriki wengine na kupata nafasi ya kuzungumza mambo kadhaa kuhusu ujumbe wa kampeni hiyo.

Waziri Riziki Pembe: Kujirudia kwa matukio ya ukatili, Wananchi wanahoji labda Adhabu zinawabembeleza wanakutwa na hatia
Snapinsta.app_470090741_9540069112699275_7065352901372521366_n_1080.jpg

Snapinsta.app_470091293_1764194650787410_6177099784299493468_n_1080.jpg
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Zanzibar, Riziki Pembe anasema: Tunaposema Ukatili Sasa Basi, tunamaanisha, juzikati kuna mtu aliniuliza hizi adhabu zinazotolewa kwa wanaokutwa na hatia ya makosa ya ukatili na udhalilishaji, je, adhabu zake ni Miaka 30 tu basi? Nikamwambia ni Sheria zilivyosema.

Hizo ni salamu za Mwananchi sio za kwangu mimi Waziri, labda inaonekana kama adhabu zinazotolewa zinawabembeleza sana Watuhumiwa ndio maana makosa yamekuwa yakijirudia, hilo suala naliacha kwa Jaji Mkuu ambapo unaweza kulifikisha kwa Wadau wa kisha Baraza la Wawakilishi na hatua nyingine tuone namna gani tunakwenda.

Mbali yote nawashukuru wote waliotuchangia na kutusaidia kufika hadi hapa tulipofika zikiwemo Taasisi za Kiserikali na Taasisi Binafsi, suala la udhalilishaji lazima lipigwe kwa nguvu zote, hata Rais Mwinyi amelisema hilo mara kadhaa.

Amesema Marathon ya Mtoto Mboni Yangu imefanikiwa kwa mashirikiano makubwa baina ya Wizara na Taasisi mbalimbali ikiwemo Taasisi ya Ndoto Ajira, ambapo amezishukuTaasisi hizo kutokana na mchango wao katika kufanikisha shughuli hiyo.

Mkuu wa Mkoa
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa ameipongeza Wizara kwa kuipa marathon hiyo jina la Mtoto Mboni yangu kwani inaleta faraja ya kumlinda mtoto kwa kila nyanja.
Snapinsta.app_470340367_1296963204812195_8885173748337880864_n_1080.jpg
Hemed Suleiman Abdulla aitaka Jamii kubadilika
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla anasema: Takwimu za masuala ya ukatili bado haziridhishi, hakuna hatua ambayo itafika tutasema kuwa kwa takwimu fulani zinaridisha, hiyo ni kwa kuwa mkakati wetu ndani ya Tanzania na mkakati wetu ndani ya Zanzibar ni kuondoa kabisa udhalilishaji na ukatili.

Tukisema tuelekeze nguvu kwenye kupunguza inamaanisha tunaunga mkono matukio machache ya ukatili na udhalilishaji ambayo yataendelea kutokea.

Kuendelea kulaumu Viongozi wakiwemo, Sheha, Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa na kiongozi mwengine yeyote sio sawa, utayari wetu unatakiwa kuwa kwetu sote kwa asilimia 100.
Snapinsta.app_470275684_923951666054010_254900407387602070_n_1080.jpg

Snapinsta.app_470270263_581926531099617_7539490645404226867_n_1080.jpg

Snapinsta.app_469724032_947008477310444_6198967760366382669_n_1080.jpg
Kufanikiwa hili lazima tuondoe muhali, muhali hauna nafasi kwenye kupinga udhalilishaji, kwenye kupinga udhalilishaji na ukatili kwa Wanawake na Watoto.

Kuna watu wengi wamekuwa wakilalamika kwa nini kesi nyingi zinazohusiana na matukio hayo hazimaliziki vizuri au zikimalizika hakuna anayewajibishwa, changamoto ni ushirikiano kutoka kwa mashahidi ambao wengi wao ni Wananchi.

Mkurugenzi wa Mashtaka anasema watu wengi wanaotoa ushahidi Mahakamani au kwenye Vyombo vya Sheria, mwanzo unakuta anatoa ushahidi vizuri lakini baada ya muda anabadilika, anageuka na kutoonesha ushirikiano baadhi yao wanafanya hivyo baada ya kuwa wamepewa kiasi fulani cha fedha.

Vitendo hivyo havina afya katika kupinga vita udhalilishaji, nawaomba Watanzania tuwe na msimamo katika kupiga vita.

Mambo hayo yanahitaji maamuzi magumu, kuna wakati inatokea mhalifu ni mtu ambaye upo karibu naye lakini siku zote ukiacha kukemea uhalifu anaoufanya kwa wengine, ujue kwamba siku moja kituo kitakachofuata ni kwako.

Kama unaona jirani yako amefanyiwa ukatili, mtoto wake ameharibiwa na upo kimya ujume kesho ni zamu yako.

Lazima tukubali, tuamue kurudi katika zama za Wazee wetu, mtoto wa mwenzako alikuwa wako, hata mzazi alipoonekana amebeba mzigo ilikuwa ni kawaida mtoto kwenda kumpokea hata kama sio mzazi wake, lakini sasa hivi Watoto ndio wanataka wapokelewe mizigo na wazee wao.

Kila zama ina mambo yake lakini hayo mambo yake yanatakiwa kuendana na Mila na Desturi zenye kuchangia uwepo wa maadili mema.

Ndugu zetu, tuanzishe oparesheni maalum kuona watu wanaofanya vitendo vya ukatili na udhalilishaji ili tuwajue watu wasiojulikana.

Hata wale ambao wanakuwepo mitaani na Jamii haijui wanachokifanya, basi taarifa itoke mapema kwenye Mamlaka za Usalama ili waseme kile wanachokifanya lakini sio wasumbuliwe.

Kama kuna maeneo yanatumika vibaya basi napo hatua zichukuliwe, mfano tumejenga nyumba, tumepangisha watu na hatujui wanachokifanya ndani ya nyumba hizo au wanatumia kufanyia udhalilishaji taarifa zitolewe na hatua zichukuliwe.

Wale wanaojenga majengo ambayo hayakamiliki muda mrefu kiasi kwamba watu wamekuwa wakiyatumia kudhalilisha wengine, bado wahusika wafanye mpango wa kudhibiti hilo.

Pia wale wanaojenga hawakamilishi majengo hayo, tutashauri Serikalini hatua zichukuliwe ili ione utaratibu ufanyike kuona ni namna gani inaweza kufanyika ili majengo hayo yasiendelee kutumika vibaya.

Kauli hii wanaweza kuitafsiri vibaya, hatuzungumzi Serikali kumnyang’anya mtu kitu chochote bali inatakiwa kuwekwa utaratibu ili majengo ambayo hayajakamilika yasitumiwe vibaya na wahalifu hasa katika kufanya ukatili.

Wanaofanya matukio ya ukatili wanaharibu asili ya Zanzibar, hatukuwa na mambo hayo, zipo taasisi zinazotumika kudhaliliusha vijana wetu, niombe sana Vyombo vinazohusika kuangalia zile taasisi ambazo hazina sababu za msingi hatua zichukuliwe.

Serikali itaendelea kuridhika kile inachokipata, marafiki tunaowahitaji ni Marafiki wema, hatuhitaji fedha zinazoweza kutumika kudhalilisha Watanzania.

Unapomdhalilisha Mwanamke, unapofanya hivyo kwa kijana bila shaka unadhalilisha Taifa letu.Tuendelee kushirikiana na Serikali kupinga ukatili na udhalilishaji.

Snapinsta.app_470094937_591436246619835_2345855531736395245_n_1080.jpg
 
Back
Top Bottom