Makamu wa Rais Dkt. Mpango asema wananchi waweke chakula huku mipaka hawajazuia kupeleka nje ya nchi

RWANDES

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2019
Posts
1,788
Reaction score
4,401
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amewataka wananchi mkoani Kilimanjaro kuweka akiba ya chakula kutokana na mazao yaliyolimwa mwaka huu kukauka kwa kukosa mvua.

Kauli ya mpango inautata mkubwa kwani huwezi kuambia wananchi watunze chakula huku mipaka serikali imefungua na bado chakula kinapelekwa nje ya nchi leo makamu wa rais amekumbuka jua limeshachomoza asubuhi gharama za vyakula kwa sasa hazishiki mfano ni unga mchele na mahitaji mengine bei zipo juu kuwahi kutokea tangu tupate uhuru.
 
Wananchi washaambiwa waweke akiba wao sio watoto kwamba hawaelewi, wakiamua kuuza nje basi wajiandae na athari sio kila kitu wafanyiwe kana kwamba hawana brain za kuendesha maisha yao.

Leo hii una gunia zako 20 za mahindi ndani, unauza zinabaki gunia 5, watu wanakushauri kwamba kuna dalili ya uhaba wa mahindi hivyo usiuze tena weka akiba yako ya chakula, wewe bado unauza unataka mpaka watu waje kwako wakufungie mlango kwamba usitoe gunia lingine kuuza?

Mipaka isifungwe maana hamna mtu analazimishwa kuuza mazao, wanauza wenyewe. Watanzania wanapenda sana kudekezwa.
 
Kama wewe mleta mada ni mkulima basi tunza chakula chako wewe na familia yako.
Kama ni mfanyakazi nunua sasa na utunze.

Acha wakulima wauze ziada yao kwa pesa nzuri....pembejeo ziko juu mno.
 
School wakulima wauze mazao yao.

Waliyoyazalisha kwa nguvu na gharama zao wenyewe,bila kupata msaada wa mtu yoyote.

Nyie mjini huko endeleeni kukata mauno tu na kuwaona watu wanaofanya mambo ya ovyo ovyo ndiyo wa muhimu kwenu.

Ila Nov huko ndiyo mtawajua wakulima ni nani na umuhimu wao.

Ova
 
Hawa watendaji wa serikali nao kila mmoja ana kaulI yake tofauti.

Bashe anasema wakulima wauze nje hawajafunga mipaka, huku Dr. Mpango akisema mtunze chakula mlichonacho.

Hapo ukichunguza hizo kauli mbili vizuri, jibu lake ni kwamba kila mmoja wetu atumie akili yake kuamua hatma yake, serikali haimfundishi mtu cha kufanya.
 
Wqziri wake kwa Kilimo kwenye gazeti la Mwananchi anasema hakutakuwa na upungufu wa chakula wakulima waendelee kuuza tu. sasa hapo tunamsikiliza VP au WK? SOMA ATTACHMENT

20220719_105411.jpg
 
Hii nchi ni mazingaombwe tu.

Yaani tuna viongozi wa ajabu sana.

Wana fahamu hakuna mavuno, wanatoa vyakula kwenye maghala ya serikali, halafu wanacha kiondike nchini.. Aibuuuu
 
VUTA NI KUVUTE.

Rais yuko kuomba mikopo nje huko.
 
Wananchi washaambiwa waweke akiba wao sio watoto kwamba hawaelewi, wakiamua kuuza nje basi wajiandae na athari sio kila kitu wafanyiwe kana kwamba hawana brain za kuendesha maisha yao.

Leo hii una gunia zako 20 za mahindi ndani unauza zinabaki gunia 5 watu wanakushauri kwamba kuna dalili ya uhaba wa mahindi hivyo usiuze tena weka akiba yako ya chakula, wewe bado unauza unataka mpaka watu waje kwako wakufungie mlango kwamba usitoe gunia lingine kuuza?

Mipaka isifungwe maana hamna mtu analazimishwa kuuza mazao wanauza wenyewe watanzania wanapenda sana kudekezwa.
Fikiria wanauza kwa sababu vitu vingine vimepanda Bei na hakuna hela ,watoto wanataja Ada ,na mahitaji mengine je kufikia hapo mwanachi kwnn asiuze mazao
Hapo Cha kufanya ni kupunguza gharama ya vitu vingine ili mtu aweze kujikimu kulingana na hali halisi kw wananchi na si vinginevyo
 
Wananchi washaambiwa waweke akiba wao sio watoto kwamba hawaelewi, wakiamua kuuza nje basi wajiandae na athari sio kila kitu wafanyiwe kana kwamba hawana brain za kuendesha maisha yao.

Leo hii una gunia zako 20 za mahindi ndani unauza zinabaki gunia 5 watu wanakushauri kwamba kuna dalili ya uhaba wa mahindi hivyo usiuze tena weka akiba yako ya chakula, wewe bado unauza unataka mpaka watu waje kwako wakufungie mlango kwamba usitoe gunia lingine kuuza?

Mipaka isifungwe maana hamna mtu analazimishwa kuuza mazao wanauza wenyewe watanzania wanapenda sana kudekezwa.

Wewe kama ni kiongozi, basi ni mmoja wa wale irresponsible leaders!

Ni Serikali gani inayoweza kuwaacha wananchi wafe kwa njaa kwasababu waliuza vyakula vyao kwa hiari yao?
 
Aliyekwambia uwe mjini ukicheza pool kutwa nzima nani? Yaani mkulima ahangaike kulima na kuvuna wewe mcheza pool uonewe huruma kwa kumkandamiza mkulima asiuze mazao mahala atakapo?
 
Kumbe makamu wa Raisi yupo!!
Bei zilivyo unaachaje kuuza kwa mfano lol
 
Aliyekwambia uwe mjini ukicheza pool kutwa nzima nani? Yaani mkulima ahangaike kulima na kuvuna wewe mcheza pool uonewe huruma kwa kumkandamiza mkulima asiuze mazao mahala atakapo?

Anayeambiwa atunze chakula ni mcheza pool?
 
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amewataka wananchi mkoani Kilimanjaro kuweka akiba ya chakula kutokana na mazao yaliyolimwa mwaka huu kukauka kwa kukosa mvua.

Kauli ya mpango inautata mkubwa kwani huwezi kuambia wananchi watunze chakula huku mipaka serikali imefungua na bado chakula kinapelekwa nje ya nchi leo makamu wa rais amekumbuka jua limeshachomoza asubuhi gharama za vyakula kwa sasa hazishiki mfano ni unga mchele na mahitaji mengine bei zipo juu kuwahi kutokea tangu tupate uhuru.
Mpumbavu sana wewe tabu aipate babu yangu au wako kule kijijini halafu utake mazao akuuzie kwa bei ya kukunufaisha wewe mlaji tena inaonekana unataka upewe hata bure,waswahili tuna shida kubwa sana tatizo serikali ilitulemaza kwa kumnyonya mkulima ikimpa nafuu kubwa asiyelima sasa imeamua itende haki.
 
Kauli ya Mhe. Makamu wa Rais haina utata wala kupingana na kiongozi yeyote. Unapewa ushauri kama unauza uza...ila uweke akiba yako ya kula! Serikali ikizuia uuzaji chakula nje bado mtasema..# Tuwaache viongozi wetu wafanye kazi.🙏🙏🙏
 
Wewe kama ni kiongozi, basi ni mmoja wa wale irresponsible leaders!

Ni Serikali gani inayoweza kuwaacha wananchi wafe kwa njaa kwasababu waliuza vyakula vyao kwa hiari yao?
Kabla ya kutegemea kiongozi awe responsible, wewe mwananchi inatakiwa uwe responsible sio kila kitu mpaka kiongozi aseme.

Lini watu watakuwa na akili za kujitegemea sio kila kitu mpaka asimame kiongozi aseme?
 
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amewataka wananchi mkoani Kilimanjaro kuweka akiba ya chakula kutokana na mazao yaliyolimwa mwaka huu kukauka kwa kukosa mvua.

Kauli ya mpango inautata mkubwa kwani huwezi kuambia wananchi watunze chakula huku mipaka serikali imefungua na bado chakula kinapelekwa nje ya nchi leo makamu wa rais amekumbuka jua limeshachomoza asubuhi gharama za vyakula kwa sasa hazishiki mfano ni unga mchele na mahitaji mengine bei zipo juu kuwahi kutokea tangu tupate uhuru.
Wapumbavu wanaishi Dar es Salaam na mijini wanataka wanunue unga kilo Tsh 1,000 milele. Hawajui mkulima anavyohangaika kufyeka pori, kulima na kupalilia. Hawajui bei ya pembejeo eti leo wanalalamika mahindi na Michele vinakwenda nje ya mipaka ya Tanzania.

Huu ndiyo wakati wa mkulima wa Tanzania kupata bei nzuri, hakuna kufunga mipaka. Chakula kikiisha na sisi Tanzania tutanunua nje ya Tanzania. Vile vile kama tutauza nje basi soko litakua hivyo basi watu wengi watajishirikisha na kilimo
 
Back
Top Bottom