Makamu wa Rais Dkt. Mpango awasili Rwanda kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi za Jumuiya ya Madola

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mpango 1.jpg

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akizungumza na baadhi ya viongozi wa Serikali wanaoshiriki Mkutano wa 26 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola unaofanyika jijini Kigali, Rwanda, Juni 20-25, 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amewasili Nchini Rwanda tarehe 22 Juni 2022 kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi za Jumuiya ya Madola (Commonwealth Heads of Government Meeting-CHOGM) unaofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kigali.

Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano huo ulioanza tarehe 20 Juni na utahitimishwa tarehe 25 Juni 2022.

Makamu wa Rais, mbali ya kushiriki kwenye mkutano huo ameombwa pia miadi ya kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wakiwemo Rais wa Namibia, Hage Geingob; Waziri Mkuu wa Mauritius; Pravind Jugnauth; Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau na Melinda Gates.

Inaelezwa kuwa miadi hiyo ni ishara ya dhahiri ya kuendelea kuimarika kwa diplomasia ya Tanzania duniani chini ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia.

Hivyo, Makamu wa Rais anatarajiwa kutumia miadi hiyo kusisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya pande mbili na hasa ushirikiano katika eneo la uwekezaji na biashara pamoja na utoaji wa huduma za kijamii kwa wananchi.

Mpango kikao.jpg

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akiwa katika kikao cha maandalizi na ujumbe wake kabla ya kushiriki kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola unaofanyika jijini Kigali, Rwanda, Juni 20-25, 2022.

Aidha, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula naye yupo nchini humo kushiriki Mkutano huo katika ngazi ya Mawaziri tarehe 23 Juni 2022.

Kama ilivyo kwa Makamu wa Rais, Balozi Mulamula ameombwa miadi ya kufanya mazungumzo na Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za India, Zambia, Botswana, Eswatini, Singapore na mke wa Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony Blair, Bibi Cherie Blair ambaye ni mwanzilishi wa Cherie Foundation.

Wakati huohuo, mikutano ya utangalizi ya mkutano huo, inaendelea ambapo tarehe 20 hadi 23 Juni 2022 ilifanyika mikutano ya jukwaa la vijana, jukwaa la wanawake na jukwaa la biashara. Tanzania ilishiriki katika majukwaa yote hayo.

Wakati wa mkutano wa jukwaa la biashara, washiriki pamoja na mambo mengine, walijadili namna bora ya kufanya biashara huku dunia ikiwa bado inakabiliwa na janga la ugonjwa wa Corona na athari za vita kati ya Urusi na Ukraine.

Ujumbe wa Tanzaia katika mkutano huo uliongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara katika Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah ambaye alieleza hatua zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya sita za kuboresha mazingira ya biashara na fursa lukuki za uwekezaji zinazopatikana nchini.

Kwa upande wa mkutano wa jukwaa la vijana ambapo Tanzania iliwakilishwa na vijana saba, ulisistizwa umuhimu wa kuwaendeleza vijana. Ilielezwa kuwa endapo nchi za Jumuiya ya Madola zinahitaji kufikia maendeleo ya kweli, hazina budi kuwekeza kwa vijana kwa sababu katika nchi hizo vijana ni zaidi ya asilimia 60.

Kuhusu mkutano wa jukwaa la wanawake, ulisisitizwa umuhimu wa kumuendeleza mwanamke ikiwa ni pamoja na kumpatia elimu ya kumiliki, kukuza na kufanya biashara, kuweka usawa wa kijinsia na kukomesha vitendo vyote vya unyanyasaji dhidi ya wanawake.

Mpango 3.jpg

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akifafanua jambo kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango kuhusu ushiriki wa Tanzania katika mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola unaofanyika Jijini Kigali, Rwanda, Juni 20-25, 2022.
 
Kila kitu kiko set, hata kikao cha globalist Davos alienda Mpango na kwa Kagame pia anaenda Mpango, sasa nimeamimi Mpango ni raisi ajaye, …
 
View attachment 2269769
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akizungumza na baadhi ya viongozi wa Serikali wanaoshiriki Mkutano wa 26 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola unaofanyika jijini Kigali, Rwanda, Juni 20-25, 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amewasili Nchini Rwanda tarehe 22 Juni 2022 kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi za Jumuiya ya Madola (Commonwealth Heads of Government Meeting-CHOGM) unaofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kigali.

Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano huo ulioanza tarehe 20 Juni na utahitimishwa tarehe 25 Juni 2022.

Makamu wa Rais, mbali ya kushiriki kwenye mkutano huo ameombwa pia miadi ya kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wakiwemo Rais wa Namibia, Hage Geingob; Waziri Mkuu wa Mauritius; Pravind Jugnauth; Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau na Melinda Gates.

Inaelezwa kuwa miadi hiyo ni ishara ya dhahiri ya kuendelea kuimarika kwa diplomasia ya Tanzania duniani chini ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia.

Hivyo, Makamu wa Rais anatarajiwa kutumia miadi hiyo kusisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya pande mbili na hasa ushirikiano katika eneo la uwekezaji na biashara pamoja na utoaji wa huduma za kijamii kwa wananchi.

View attachment 2269770

View attachment 2269773
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akifafanua jambo kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango kuhusu ushiriki wa Tanzania katika mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola unaofanyika Jijini Kigali, Rwanda, Juni 20-25, 2022.
Umakamu wa Rais Raha sana ! zaidi ya kula bata , hakuna kingine yaani !!
 
Common wealthy countries huo umoja hauna mvuto tena si Dhani kama head of States wengi wata udhuria wengi watatuma wakilishi wao.
Russia kasha expose madhaifu yao kiuchimi na military inacability kumbe Nato US na Britain ni super power za media, hata chumi zao zinaumba kwa Oparation ya Russia uko Ukraine, hao watatusaidia je zaidi ya kutujazia ma mikopo
 
Kama ametumia ndege ni uharibifu wa hela angeenda tuu na gari akikagua miradi ikiwemo barabara mbovu kabisa ya lusahunga-rusumo
 
Hangaya anamkwepa PK... anafuata maelekezo kutoka msoga ndiomana hata Nairobi hakwenda kujadili ishu ya DRC, na sasa drc wametuma ujumbe wao kuja bongo kupanga fitna
 
Kumbe akienda safari huyu jamaa hamna shida!! Ila akienda Samia ndo shida ? Mara utasikia ...Kodi zetu zitakoma!!duuh kumbe hutakiwi kumridhisha mwanadamu kwenye maisha yako ..
Umewahi kuniona nikipinga safari zenye tija? Mimi naunga mkono raisi kwenda mikutano yenye manufaa kwa taifa.
 
Hangaya anamkwepa PK... anafuata maelekezo kutoka msoga ndiomana hata Nairobi hakwenda kujadili ishu ya DRC, na sasa drc wametuma ujumbe wao kuja bongo kupanga fitna
Hii Jumuiya ya Afrika Mashariki ya hovyo kweli .... yaani Member State wanapigana vita halafu bado unategemea Jumuiya iwe na Maendeleo. Hivi kati ya malengo ya Jumuiya ni nini hasa kama siyo peace na Uchumi ...!!
 
Jumuiya Kama ECOWAS sometimes naionaga iko serious kiasi Fulani.Hizi jumuia nyingine Ni za kisanii tu,hata SADC yenyewe haina cha maana zaidi ya story za enzi za ukombozi wa nchi hizo kitu ambacho kwa Sasa vijana hawaelewi hizo story.
 
Back
Top Bottom