Makamu wa Rais Dkt. Mpango awasili Rwanda kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi za Jumuiya ya Madola

Makamu wa Rais Dkt. Mpango awasili Rwanda kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi za Jumuiya ya Madola

View attachment 2269769
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akizungumza na baadhi ya viongozi wa Serikali wanaoshiriki Mkutano wa 26 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola unaofanyika jijini Kigali, Rwanda, Juni 20-25, 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amewasili Nchini Rwanda tarehe 22 Juni 2022 kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi za Jumuiya ya Madola (Commonwealth Heads of Government Meeting-CHOGM) unaofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kigali.

Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano huo ulioanza tarehe 20 Juni na utahitimishwa tarehe 25 Juni 2022.

Makamu wa Rais, mbali ya kushiriki kwenye mkutano huo ameombwa pia miadi ya kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wakiwemo Rais wa Namibia, Hage Geingob; Waziri Mkuu wa Mauritius; Pravind Jugnauth; Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau na Melinda Gates.

Inaelezwa kuwa miadi hiyo ni ishara ya dhahiri ya kuendelea kuimarika kwa diplomasia ya Tanzania duniani chini ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia.

Hivyo, Makamu wa Rais anatarajiwa kutumia miadi hiyo kusisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya pande mbili na hasa ushirikiano katika eneo la uwekezaji na biashara pamoja na utoaji wa huduma za kijamii kwa wananchi.

View attachment 2269770
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akiwa katika kikao cha maandalizi na ujumbe wake kabla ya kushiriki kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola unaofanyika jijini Kigali, Rwanda, Juni 20-25, 2022.

Aidha, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula naye yupo nchini humo kushiriki Mkutano huo katika ngazi ya Mawaziri tarehe 23 Juni 2022.

Kama ilivyo kwa Makamu wa Rais, Balozi Mulamula ameombwa miadi ya kufanya mazungumzo na Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za India, Zambia, Botswana, Eswatini, Singapore na mke wa Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony Blair, Bibi Cherie Blair ambaye ni mwanzilishi wa Cherie Foundation.

Wakati huohuo, mikutano ya utangalizi ya mkutano huo, inaendelea ambapo tarehe 20 hadi 23 Juni 2022 ilifanyika mikutano ya jukwaa la vijana, jukwaa la wanawake na jukwaa la biashara. Tanzania ilishiriki katika majukwaa yote hayo.

Wakati wa mkutano wa jukwaa la biashara, washiriki pamoja na mambo mengine, walijadili namna bora ya kufanya biashara huku dunia ikiwa bado inakabiliwa na janga la ugonjwa wa Corona na athari za vita kati ya Urusi na Ukraine.

Ujumbe wa Tanzaia katika mkutano huo uliongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara katika Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah ambaye alieleza hatua zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya sita za kuboresha mazingira ya biashara na fursa lukuki za uwekezaji zinazopatikana nchini.

Kwa upande wa mkutano wa jukwaa la vijana ambapo Tanzania iliwakilishwa na vijana saba, ulisistizwa umuhimu wa kuwaendeleza vijana. Ilielezwa kuwa endapo nchi za Jumuiya ya Madola zinahitaji kufikia maendeleo ya kweli, hazina budi kuwekeza kwa vijana kwa sababu katika nchi hizo vijana ni zaidi ya asilimia 60.

Kuhusu mkutano wa jukwaa la wanawake, ulisisitizwa umuhimu wa kumuendeleza mwanamke ikiwa ni pamoja na kumpatia elimu ya kumiliki, kukuza na kufanya biashara, kuweka usawa wa kijinsia na kukomesha vitendo vyote vya unyanyasaji dhidi ya wanawake.

View attachment 2269773
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akifafanua jambo kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango kuhusu ushiriki wa Tanzania katika mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola unaofanyika Jijini Kigali, Rwanda, Juni 20-25, 2022.
Lazima kuna sababu za Mama kutokwenda,maana haikutarajiwa asihudhurie mkutano huu ambao ni mkubwa na una heads of Gvt karibu 60 ikiwemo Boris,Trudeau, mashirika makubwa ya maendeleo imf,Afdb,WB na makampuni makubwa ya kiuwekezaji. lazima kunasababu siyo bure.Maana ile tu ya Nairobi kumtuma Balozi ilileta ? kidogo na hii tena.
 
Lazima kuna sababu za Mama kutokwenda,maana haikutarajiwa asihudhurie mkutano huu ambao ni mkubwa na una heads of Gvt karibu 60 ikiwemo Boris,Trudeau, mashirika makubwa ya maendeleo imf,Afdb,WB na makampuni makubwa ya kiuwekezaji. lazima kunasababu siyo bure.Maana ile tu ya Nairobi kumtuma Balozi ilileta ? kidogo na hii tena.
The bad news is "The world won't wait for us, not ever."
 
Mbona wao hawajamleta malkia badala yake kaja kuwakilishwa na mwanamfalme?
Kila mtu ashinde mechi zake.
Mbona Muda tu ilishatangazwa Malkia ana matatizo ya miguu na function kibao hajahudhuria.
 
Speech ni official statement from the government na huwa kwenye written form na inaweza kutolewa na rais au kiongoz mwingine yeyote kwa niaba yake na to put it in context speech hyo imetolewa leo na makamu wa rais inatosha kabisa.
"Speech hyo imetolewa leo na makamu wa rais inatosha kabisa".

😄😄😄😄 Aiseeee.
 
Watambue tu kwamba waingereza awapendi dharau.

Wanakuona unapaa huko kusiko na kichwa wala miguu; halafu safari ya masaa mawili nchi jirani walipo unatuma mtu wa kukuwakilisha.

Wakati wao hilo jambo ni serious anaenda waziri mkuu na Queen (Prince Charles anamwakilisha mama yake). Hiyo ni highest dignitaries U.K. can send anywhere halafu we hunamuda.

Jamaa watu wa visasi watch this space
We jamaa una chekesha. Akienda ni nongwa, asipo enda pia nongwa.
 
23 June 2022

Kigali Summit on Malaria and NTDs | Remarks by His Royal Highness Prince Charles

 
Mbona Muda tu ilishatangazwa Malkia ana matatizo ya miguu na function kibao hajahudhuria.
Nasie rais anadharura za msing ndomaana hajahudhuria.
Achen inferiority complex Tanzania ni nchi huru wala haiwajibik kwa UK.
Wala hakuna nchi iliyoendelea dunian kwa kutegemea misaada kutoka UK.
 
Queen kwa umri wake public engagement zake zote anazotakiwa kutokea sasa hivi anaenda mtoto wake ata huko kwao majuzi walimfanyia sherehe kubwa siku tatu bila ya kazi + mbili za weekend hakutokea public zaidi ya kurusha video tu.

Subiri waanze kuminya misaada yao kidogo; uongezewe tozo ndio utajua.
Africa utumwa wa kifikra bado ni tatzo kubwa saana.
 
Nasie rais anadharura za msing ndomaana hajahudhuria.
Achen inferiority complex Tanzania ni nchi huru wala haiwajibik kwa UK.
Wala hakuna nchi iliyoendelea dunian kwa kutegemea misaada kutoka UK.
😄😄😄 Napenda kutuma salamu kupitia NMB.
 
Back
Top Bottom