Makamu wa Rais Dkt. Mpango: Kuna mivutano kati ya Makatibu wakuu na Manaibu makatibu wakuu hasa naibu akihoji matumizi ya fedha!

Makamu wa Rais Dkt. Mpango: Kuna mivutano kati ya Makatibu wakuu na Manaibu makatibu wakuu hasa naibu akihoji matumizi ya fedha!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Makamu wa Rais Dkt. Mpango amemtaka Katibu mkuu Kiongozi Balozi Hussein Katanga kuwaangalia kwa makini Makatibu Wakuu wa Wizara na Manaibu wao kwani kuna kutoelewana kwingi.

Dkt. Mpango amesema inakuwa nongwa pale Naibu Katibu Mkuu anapomhoji Katibu Mkuu kuhusu matumizi ya fedha.
Dkt. Mpango ameahidi kuwafuatilia kwa makini Makatibu Wakuu wote.

Kadhalika Dkt. Mpango amemtaka Dkt. Mwigulu Nchemba kuhakikisha ifikapo Desemba mwaka huu mapato ya TRA yanafikia sh trillion 2 kwa mwezi.

Chanzo: TBC

Maendeleo hayana vyama!
 
Wow! Kaanza kuuma. Sina shaka naye Muha huyu,najua tutafika tu. Wale waliokaa chonjo kusubiri the reversal of Magufulis' stance are in for a disappointment. Watasubiri sana.
 
Anahakikisha mapato vipi? Issue sio Kukusanya tu, bali ni kuhakikisha kule zinapotakiwa kukuasanywa zipo za kutosha.

Hivi hawa kwanini wasituoneshe kwa vitendo hizi issue wote waende pale kariakoo wafungue maduka na wengine wakalime korosho na pamba. Bure Kabisa hawa Watu.
 
Mpango kazi yake ni kukata utepe,anafanya overtaking kwenye mazungumzo mpaka Mama Samia anakosa ya kuongea.
Naona anajiona yeye ndio Rais sababu Mama Samia ni Mwanamke!angalia anavyongea utadhani yeye ndio Rais.
Mama mwenyewe alisema jana kamuongezea Mpango majukumu 2, kumshauri kuhusu uchumi na kusimamia fedha za serikali, ambapo hapo awali hayakuwa majukumu ya VP, ana baraka zote kutoka kwa Mama hayo anayoongea. Acheni unafiki na kukurupuka wabongo, ujuaji mwingiii.
 
Mpango kazi yake ni kukata utepe,anafanya overtaking kwenye mazungumzo mpaka Mama Samia anakosa ya kuongea.
Naona anajiona yeye ndio Rais sababu Mama Samia ni Mwanamke!angalia anavyongea utadhani yeye ndio Rais.
Sio mkuu, kazi yake ni kumsaidia Rais.
 
2T za Dec 2020 zilipatikana kwa jasho na damu.Haya maelekezo nadhani awape mawaziri kuweka fursa nzuri kuvutia wawekezaji na uzalishaji,ikiwemo kuwapanga machinga katika maeneo stahiki.
 
Mama keshatoa green light kwa wafanya biashara sasa kodi ni kipaombele utalipa kulingana na biashara yako
 
Back
Top Bottom