PostGE2025 Makamu wa Rais, Dkt. Nchimbi: Vijana wengi hawajui umuhimu wa Muungano

PostGE2025 Makamu wa Rais, Dkt. Nchimbi: Vijana wengi hawajui umuhimu wa Muungano

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Emmanuel Nchimbi ameitaka Wizara ya Muungano na Mazingira kujipanga katika suala la elimu ya muungano hususani kwa vijana kwani wengi hawajui historia na umuhimu wa muungano.

Dkt. Nchimbi ambaye alikuwa kwenye kikao kazi akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira, amesema eneo pekee linaloweza kusaidia kuweka muungano salama ni kuhakikisha vijana wanaelewa historia, sababu na umuhimu wa Muungano.

“Kwenye eneo la muungano tusisubiri hoja zijitokeze, daima tuangalie mazingira yanayoweza kusababisha hoja na tunatengeneza majibu ya haraka au urekebishaji wa haraka ili kufanya mazingira ya kwamba muungano wetu uendelee kuwa imara siku zote,” amesema Dk Nchimbi

 
muungano ambao mtanganyika hawezi kuwa rais zanzibar ila mzanzibar anaweza kuwa rais tanganyika, mtanganyika hawez kuwa waziri zanzibar ila mzanzibar anaweza kuwa waziri tanganyika kwa uchache.

HUO SIYO MUUNGANO.
 
Mtanganyika analipa ada ya chuo Zanzibar kama mgeni ilihali mzanzibar akija Tanganyika analipa chuo kama mtanganyika TU , siombi muungano UVUNJWE ila nacho omba ni changes lifanyike utapofika wakati wa sisi kukaa madarakani msiwe na visingizio kua hakuambiwa
 
Pamoja na mapungufu yake sina hamu na muungano pale kmkm walipoua ndgu zetu kisa wanalipa kisasi.bora tuwe na tanganyka yetu yenye amani kuliko muungano wenye vinyongo ndni yake
 
Muungano wenu siyo muhimu kwetu.

Hatuhitaji muungano unaopendelea upande mmoja.

Vijana wa tanganyika tunahitaji kuungana D9 kuwaondoa hawa wauaji wetu wao ccm na mapolisi yao.

mtekaji na Muuaji hawezi kuwa sehemu ya usuluhishi.

Njia pekee ni kuwaondoa.

Haya matamko pelekeni kwenye majukwaa ya ccm, siyo humu.
 
Nchi hii hatujafanya uchaguzi, hatuna rais wala makamu wala mbunge, hizo drama pelekeni ccm.

Nahisi JF iko kompromised sasa, kwanini wanaruhusu ujinga huu kuletwa humu?
 
Pamoja na mapungufu yake sina hamu na muungano pale kmkm walipoua ndgu zetu kisa wanalipa kisasi.bora tuwe na tanganyka yetu yenye amani kuliko muungano wenye vinyongo ndni yake
Maneno hayo ni ya kumkingia kifua Samia aliyewaita na kuwapa oda ya kuua.
 
Madiru bwana sijui dokta wa nini ? Huyu .Tunaomba utufafanulie bilioni 5 iliwezaje kuingia kwenye simu tena mtandao wa simu ,simu si ingepasuka kwa uzito wa pesa
 
muungano ambao mtanganyika hawezi kuwa rais zanzibar ila mzanzibar anaweza kuwa rais tanganyika, mtanganyika hawez kuwa waziri zanzibar ila mzanzibar anaweza kuwa waziri tanganyika kwa uchache.

HUO SIYO MUUNGANO.
Nipo nakunywa pombe hapa... naogopa hapa..
 
Tuna wazanzibar wamewahi kuwa wabunge Tanganyika lakini hakuna mtanganyika amewahi kuwa hata sheha Zanzibar!!

*Kupata Kitambulisho cha Mzanzibar Mkaazi wewe mtanganyika ni kipengele na ndiyo fursa zote zilipofichwa!!
 
Sio vijana tu, hata sisi wazee tuliowahi kuwepo kwenye utawala wa Tanganyika japo kwa muda mfupi hatukuweza kuelewa lengo lenye faida kwa umma wa watanganyika.
Haiingii akilini kwa nchi yenye ukubwa wa eneo la kilomita za mraba 945000 na watanganyika millioni 9 kuungana na kisiwa chenye ukubwa wa kilometa za eneo la 2642 na wazanzibari laki tatu wakati huo.
Dhana ya muungano huu unaofanana sana na ndoa za utotoni hauwezi kuelezwa ukaeleweka kwa kizazi cha sasa.....
 
Usiseme hawaujui umuhimu wa muungano sema vjana wameelimika wameyaona mapungufu mengi ya muungano na imegundulika hauna manufaa hasa kwa TANGANYIKA angalau nchi ya zanzibar wananufaika, muungano gn zanzibar ni nchi yenye katiba, rais, bunge, baraza la mawaziri na taasisi zote muhimu za kserikali, muungano upi huu ambao mzanzibar anakuja kutawala Tanganyika anakuwa rais, rc, dc, waziri kwa mgongo wa muungano wkt mtanganyika hawez kuwa hata mjumbe huko zanzibar, muungano gn ambao zanzibar inatambulika kama nchi wkt Tanganyika haipo kama nchi hata jna tu halipo huu ni muungano wny manufaa kwa zanzibar na wazanzibar MPK HAPO NI YUPI ANAUJUA VEMA MUUNGANO KATI YA NCHIMBI NA MACCM na vjana wa TANGANYIKA wasiotaka muungano. nywi nywi nywi.
 
Wanatudanganya kwa petty issue wanaacha kuzungumzia rasilimali za Nchi na Friday kwa Watanzania mwaka utaisha Muungano,Vijaya wajiajiri,tumewatengenezea fursa,Vijaya hawajui mana ya Muungano,uchaguzi wa Mameya Tanzania nzima Ila hautakuja kumsikia kiongozi peyote akizungumzia rasilimali za Nchi na faida zake nani mwekezaji na tunapata nini...
 
Back
Top Bottom