PostGE2025 Makamu wa Rais, Dkt. Nchimbi: Vijana wengi hawajui umuhimu wa Muungano

PostGE2025 Makamu wa Rais, Dkt. Nchimbi: Vijana wengi hawajui umuhimu wa Muungano

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
muungano ambao mtanganyika hawezi kuwa rais zanzibar ila mzanzibar anaweza kuwa rais tanganyika, mtanganyika hawez kuwa waziri zanzibar ila mzanzibar anaweza kuwa waziri tanganyika kwa uchache.

HUO SIYO MUUNGANO.
Sio kweli hili uloliongea chunguza mwenyewe hlf uje kuthibitisha tena hili uloliandika
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Emmanuel Nchimbi ameitaka Wizara ya Muungano na Mazingira kujipanga katika suala la elimu ya muungano hususani kwa vijana kwani wengi hawajui historia na umuhimu wa muungano.

Dkt. Nchimbi ambaye alikuwa kwenye kikao kazi akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira, amesema eneo pekee linaloweza kusaidia kuweka muungano salama ni kuhakikisha vijana wanaelewa historia, sababu na umuhimu wa Muungano.

“Kwenye eneo la muungano tusisubiri hoja zijitokeze, daima tuangalie mazingira yanayoweza kusababisha hoja na tunatengeneza majibu ya haraka au urekebishaji wa haraka ili kufanya mazingira ya kwamba muungano wetu uendelee kuwa imara siku zote,” amesema Dk Nchimbi

Mojawapo ya majanga aliotuachia Nyerere! Ni kongwa la utumwa! Watu 300,000 wanapotawala 60 Millioni! Watanganyika wamekuwa kama mazezeta!
 
Alitakiwa mwenyewe afafanue Hata kwa muhitasari historia, sababu, na umuhimu wa Muungano. Sasa na Yeye katuacha hewani, tutafika?
Anaweza kutoa historia tu, sababu za Muungano za wakati ule sio za leo! Kwa leo ni kulinda Himaya ya CCM tu! Ukiuvunja hao wabunge wa CCM toka Zanzibar watafanya nini hasa? Wanajua itawaletea ugomvi! Ni source nzuri ya ajira kwa Wazanzibari.
 
Back
Top Bottom