Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Katika kuboresha miundombinu ya barabara, Serikali kupitia TANROADS imeendelea kutekeleza miradi kabambe na muhimu ya Maendeleo ya barabara Sehemu mbalimbali Nchini, ikiwemo katika Jiji la Arusha, ambapo Makamu wa Rais Dkt Phillip Isdor Mpango ameweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa barabara ya Mianzini - Olemringaringa - Ngaramtoni Juu na Olemringaringa - Sambasha - Timbolo km 18, Jijini humo.
Akizungumza mara baada ya kuweka jiwe la Msingi kwenye Mradi huo tarehe 18 Mei -2023 Jijini Arusha Makamu wa Rais Dkt Mpango amesema barabara hiyo ni Muhimu kwani itafungua fursa nyingi, Itarahisisha usafiri, itachochea Utalii, kuongeza uzalishaji na kupendezesha Jiji hili, ambapo kutakuwa na taa za barabarani katika maeneo wanayoishi watu.
Ameitaka TANROADS na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuhakikisha kuwa Ujenzi wa barabara hiyo unaambatana na taa za barabarani, upandaji miti na maua huku akiwaomba wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha ili mradi huo ukamilike haraka iwezekanavyo.
Makamu wa Rais amesisitiza "Tunajenga barabara hizi kuuhisha maendeleo, ndicho tulichoapa kuwafanyia Mhe Rais Dkt Samia halali Usingizi, kutafuta fedha pale ambapo za kwetu wenyewe hazitoshi ili Jiji hili lizidi kuwa kitovu kikuu katika Uchumi wa Taifa, tunataka kurahisisha usafiri, nisema mapema lengo la kuboresha Barabara hizi sio kuongeza vifo niwakumbushe, madereva wa vyombo vya moto, Vijana wetu wa bodaboda wakumbuke kuwa wanabeba robo za watu, na za kwao wenyewe, ajali katika Taifa letu zinatupotezea watu wengi mnoo na kuathiri sana nguvu kazi ya Taifa letu".