Makamu wa Rais Philip Mpango kwanini Ofisi yako inashindwa kuifanya Dodoma ya kijani kwa kupanda miti msimu huu wa mvua?

Kwa nini mamlaka zisitunge sheria ndogo za Jiji kwamba kila nyumba/kiwanga kipandwe si chini ya miti kumi kulingana na ukubwa wa eneo?

Kwa nini kila nyumba kusisitungwe sheria ndogo ya kupanda miti na kufanya USAFI mita kadhaa kutoka jengo lilipo?

Kwa nini kusitungwe sheria ndogo zinazoelekeza kila mkaazi wa nyumba kufanya usafi wa kufyeka, kufagia, kukatia miti kusafisha mtaro kuzunguka nyumba?

Haya yakifanyika na Mamlaka kugawa miche ya miti BURE baada ya miaka mitano Dodoma haitakuwa hivi ilivyo.

Jambo hili kwa kiasi kikubwa linahitaji USIMAMIZI wa SHERIA kuliko fedha. Ila kwa kuwa jambo hili hakuwapo fedha wakubwa na watunga sheria na wasimamizi, HAWAONI UMUHIMU.
 
Taasisi ya misitu ifanye utafiti wa miti inayostahili ukame, moja ya miti hiyo ni muarobaini
 
Nchi hii inaongozwa na matukio ya kisiasa yanayoibuka siku moja na kupoteza siku inayofuata kama uhai wa uyoga.
Kuna mdau mmoja aliamua kupanda miti kwenye maeneo yake tangu miaka ya 80.
Serikali hiyo hiyo imeamua kujenga barabara ya lami, barabara itakayopita kwenye eneo lenye miti yenye umri wa miaka ishirini na zaidi. Serekali sikivu ilitoa amri miti ikatwe tena bila fidia kuashiria kuwa barabara ni muhimu sasa kuliko miti ambayo huku nyuma iliwahi kuwa kipaumbele cha mazingira.

Dodoma inatakiwa ipandwe miti ya kutosha tu, tena bila kutegemea pesa za wafadhili. Wizara ya Makamu wa Rais inayosimamia mazingira ni mkakati tu wa kuchota pesa za wafadhili.
 
okay
 
Taasisi ya misitu ifanye utafiti wa miti inayostahili ukame, moja ya miti hiyo ni muarobaini
Fuatilia NGO moja inaitwa Lead foundation. Inapiga kazi moja matata sana kwenye maeneo makame.
 
Hii kitu huwa najiuliza sana.... Nashindwa kupata majibu....
 
Asante kwa kukumbusha, kampeni itaanza karibuni sana
Chuo cha UDOM wana mpango upi wa kupanda miti katika eneo lao?? Huwa nikipita pale University of Dar es Salaam hali ya hewa huwa inabadilika kabisa.... Inakuwa so fresh... UDOM ni chuo kikubwa.... Wana eneo kubwa. Mikakati yao ya kila mwaka ya upandaji wa miti ni ipi ??
 
Na hiki kipupwe kweli dodoma miti itaota kweli
 

Kwanza ujue hizi mvua zinazo Dodoma hazipo!
 
Una uhakika Dodoma wameshapata tone la mvua? Au kuishi Dar unafikiri mvua inayonyesha Dar ipo kila mahali
 
maandalizi yako tayari, sio kwa udom pekee ni kwa mkoa wote wa Dodoma,

Miche ya miti aina mbalimbali inasambazwa kila kona ya dodoma na wilaya zake, tayari kusambazwa vijijini ili walau kila kaya ipate na kupanda miti kadhaa, mara tu mvua za masika zitakapoanza kunyesha.
Kuna dalili mvua za mwaka ujao wa kilimo kwa mkoa wa dodoma kuanza mapema, hata hivyo ni vizuri kusubiri taarifa rasmi ya mamlaka ya hali ya hewa...

Kwa ujumla tangu Mh. Rais Dr. SSH azindue kampeni ya upandaji miti, kuifanya Dodoma ya kijani, wananchi na taasisi mbalimbali za umma na za kiraia wamehamasika sana na ni mategemeo baada ya miaka kdhaa Dodoma itabadilika kabisa....
Kumbuka ni zoezi endelevu la kila mwaka....
 
Kwani Kasulu ni ya kijani? kama ameshindwa mji mdogo kama wa Kasulu ataweza Dodoma?
 
Waziri wa mazingira yupo kwani?

Tz sikukuu nyiiingi hazina mshiko
Wangetumia siku kadhaa za sikukuu majira za mvua ‘ kutumia kupanda miti nchi nzima na iwe ni mandatory’
Sikukuu za dini yoyote hazihusiki kwa hili zoezi pls
Hatuko serious kabisa katika hili wakati huo huo asilimia 99%ya wananchi tunachemshia maharage kwa kutumia mkaa/kuni.... Miaka nenda rudi.....
 
U
Umeliweka vizuri sana.
Kipindi cha kama miaka 2-3 nyuma nakumbuka kibali cha ujenzi kilikuwa hakitolewi hadi mchoro wa ramani ya nyumba ioneshe miti. Kulikuwa na idadi ya miti kwa viwanja vya high, medium na low density. Shida ni kuwa ufuatiliaji wa hiyo miti ndiyo kizungumkuti. Na sidhani kama hata hilo la miti kwenye ramani linatekelezwa tena
 
Hiki kitu sidhani kama kipo... Nadhani ilikuwa ni Pure politics🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…