Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris awataja Harmonize, JUX, Darasa, Zuchu, Alikiba, Mbosso, Jay Melody, Marioo na Platform kwenye Playlist yake

Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris awataja Harmonize, JUX, Darasa, Zuchu, Alikiba, Mbosso, Jay Melody, Marioo na Platform kwenye Playlist yake

anakuja kuzindua kiwanda cha diapers Tz
wakala wa ushoga hao
 
Unakataa kitu umebandika mwenyewe?
Ulibandika haya

Chini ndivyo nilivyoongezea kufuatana na mtiririko....

Kilichokuwa sio kweli ni nini?
Umesema "tatizo lao ni kutuweka tik tok tukiwa watupu. Uchi uchi tuu"

Tik Tok ni China-based company so unailaumu China?
 
Umesema "tatizo lao ni kutuweka tik tok tukiwa watupu. Uchi uchi tuu"
na wewe ulidai kuwa....China
imewakaba kooni
Ukimaanisha Marekani, na kwa tafsiri ya kitendo cha Makamu wa Raisi huyo ndio ukasema
lazima wajikombe
Hapo ndipo nami nikaja kusema, kwa lugha nyingine kuwa hao wachina "tatizo lao" ni kutuweka uchi uchi tik tok nikiwa na maana angalau hao wamarekani wamekuwa wabunifu zaidi na "kujikomba"

Mzee nilienda na mtiririko wa mada na yale uliyoyasema, nadhani ulipotea sehemu??
Tik Tok ni China-based company so unailaumu China?
Silaumu Tik Tok wala China....ila Wachina kama vile wewe ulivyowalaumu hao wamarekan kwa kujikomba......nimelaumu hulka[tatizo lao]za watu wa.... na wala sio tik toc au china per se
 
Kweli China imewakaba kooni kwa hapa Afrika, lazima wajikombe kwa namna yoyote ile

Kwa sasa mshirika mkubwa wa Afrika ni China
Kujikomba Kwa Marekani ni Afya Kwa Tanzania kuliko kujipendekeza Kwa China..

Kamala kuwataja ni promo kubwa Kwa Utalii kuliko wangealikwa Ikulu na Xi Jinpin
 
Amefanya hivyo kwa sababu ana ratiba ya kuja Tanzania🐒🐒🐒
 
Kujikomba Kwa Marekani ni Afya Kwa Tanzania kuliko kujipendekeza Kwa China..

Kamala kuwataja ni promo kubwa Kwa Utalii kuliko wangealikwa Ikulu na Xi Jinpin
Wewe choisi nawe,
Yaani unaona watanzania kama wanyama wamrekani waje watalii tu? ha ha
Afrika nzima,na Tqnzania ikiwemo, tumekuwa tukitaka au niseme, tukiomba tufanye biashara badala kuwa wapokezi wa mabakuli ya misaada. We have begged quite literaly for investments and businesses for a long time. US never had any Interest whatsover nor any policy to engage Afrika katika biashara Sasa wamarekani wanaona Wachina wamewapiku kwa "Investements" ndio wanaanza kung'aka tena kwa yale yale tu manguvu. Sasa yule mbunge ambae wanadai hawamtaki(republicans) Santos, amefikisha muswada wa kuzuia mtiririko wa Fedha kwa nchi ambazo hazita kubali kuweka sheria za kuwakubali mashoga......whaaat? Kule kule a carot and a stick Marekani iwe ni Dems au Reps sera yao ya nje ni moja....Imperialistic
Bora safari ya Ikulu badala ya kuwekwa zoo katika nchi yetu wenyewe
 
Ushirika wa China ni Maumivu maana ukichelewa kuwalipa wanachukua Airport kama Zambia na Sri Lanka
Wewe unajua vizuri habari za Sri Lanka au ndio unasikia na kusema kile unakisikia. Acha uvivu wa kujifunza. Nenda mtandaoni kasome na kutazama documentary utaelewa nini kiliendelea.

Ipo hivi, serikali ya Sri Lanka ilikuwa ni serikali badhirifu na ya wahujumu uchumi kama hii ya CCM mnayoichekea.

Jamaa wanaufujaji mkubwa wa mali na fedha za uma kiasi kwamba wakaanza kutegemea mikopo kuendesha inchi. Ilifika point sasa wameishiwa hakuna hata cha kuweka rehani tena na matumizi ya serikali ni ya hovyo kupita maelezo.

Serikali ya Sri Lanka wakaingia mkataba na China kuomba mkopo wa kuendeleza bandari yao. Wakapewa mkopo wa masharti nafuu ambao kutokana na maswala ya upigaji na ubadhirifu pesa zilitumika vibaya na hatimaye wakafeli kulipa kama kalenda ilivyowataka.

Mwisho wa siku masharti ya mkataba wa mkopo yaliwataka kama watashindwa kwenda sambamba na kalenda ya malipo basi wanatakiwa kusurrender hilo deni kwa serikali ya china ambayo itachukua hiyo bandari na kurun operations wao wenyewe kwa asilimia 100% na kujilipa deni lao plus Management costs za kusimamia hiyo bandari wao wenyewe.

Wakifanya hivyo haimaanishi wanajimilikisha bandari bali wanafanya kitu wanaita kushika usimamizi wa uendeshaji sio kuchukua umiliki.

Sasa marekani na vibaraka wake kupitia media huwa wanatoa ushuhuda wa uongo na wa kupika kuwa china anakopesha mataifa ya afrika mikopo ya kibiashara yenye riba kubwa kisha yeye anakuja kuchukua mali walizoweka bondi jambo ambalo si kweli.

Mikopo ya china ni rahisi kwa upande wa riba na ina lenga kujenga mahusiano mapya ya kirafiki na mataifa mengine jambo ambalo marekani hataki.

Marekani na wenzake wa magharibi wanachofanya ni kukupatia pesa na kukuelekeza ziende maeneo gani ambayo anajua wewe hayo maeneo hayatakuwa na faida kwako miaka inayo au hata akikupa pesa kwenye maeneo muhimu anajua hautaweza mudu kujiendeleza.

Nenda katazame chati au takwimu za kifedha eneo la mikopo uone mchango wa mataifa ya kimagharibi ndio utajua hawana lolote mbwa wale.

Wao misaada ni kwenye maeneo yanayotuletea mitafaruku tu ya kijamii ndipo watatia nguvu ila kwenye maeneo ya kutuimarisha huwezi kuta anaweka pesa au nguvu zake kusapoti.

Nenda mtandaoni katazame documentary kuhusu Sri Lanka utaelewa.

Kuna siku Zitto Kabwe akaja na hizi mbaya Twitter akijua watanzania ni vilaza na yeye ndie Smart boy Tanzania nzima. Anatupatia takwimu zake za World Bank za kupika kuhusu mkopo wa Sri Lanka na China. Tulimbana maswali na kumletea takwimu ambazo alisanda kujibu na kukubali alikuwa hana taarifa sawa sawa.
 
Wewe choisi nawe,
Yaani unaona watanzania kama wanyama wamrekani waje watalii tu? ha ha
Afrika nzima,na Tqnzania ikiwemo, tumekuwa tukitaka au niseme, tukiomba tufanye biashara badala kuwa wapokezi wa mabakuli ya misaada. We have begged quite literaly for investments and businesses for a long time. US never had any Interest whatsover nor any policy to engage Afrika katika biashara Sasa wamarekani wanaona Wachina wamewapiku kwa "Investements" ndio wanaanza kung'aka tena kwa yale yale tu manguvu. Sasa yule mbunge ambae wanadai hawamtaki(republicans) Santos, amefikisha muswada wa kuzuia mtiririko wa Fedha kwa nchi ambazo hazita kubali kuweka sheria za kuwakubali mashoga......whaaat? Kule kule a carot and a stick Marekani iwe ni Dems au Reps sera yao ya nje ni moja....Imperialistic
Bora safari ya Ikulu badala ya kuwekwa zoo katika nchi yetu wenyewe
Utalii sio biashara?

View attachment 2568241
Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris ametoa Spotify playlits yake ya nyimbo 25 za Wasanii wa Afrika ambazo anazikubali ambayo ameipa jina la “Safari Zangu: Ghana, Tanzania na Zambia”, kama sehemu ya kukuza muziki na kuwapa hamasa zaidi Wasanii wa Afrika wakati huu ambapo anafanya ziara katika Nchi hizi tatu ndani ya Wiki hii.

Mtandao maarufu wa Billboard umeitaja orodha hiyo ya Wasanii wa Nchi hizi tatu na nyimbo zao ambazo Wapenzi wa Muziki Duniani wanaweza kusikiliza kupitia Spotify na platform nyingine lengo likiwa ni kukuza Wasanii na mdundo wa Kiafrika hususani kutoka kwa Wasanii wa Ghana, Tanzania na Zambia.

Wasanii wa Tanzania ambao wamo kwenye orodha hiyo ni pamoja na Harmonize na wimbo wake mpya ambao video yake imeachiwa rasmi leo ya Single Again, pia Zuchu (Utaniua), Alikiba (Mahaba) Jay Melody (Sawa), Mbosso (Shetani), Jux & Marioo (Nice Kiss), Darassa (No Body) , Marioo & Abbah (Lonenly), Platform & Marioo (Fall).

Tayari Kamala ameanza ziara Barani Afrika na anatarajia kuwasili Nchini Tanzania Machi 29, 2023 ambapo pamoja na mengine anayoyapa kipaumbele kwenye ziara yake ikiwemo maendeleo ya kiuchumi, mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na ongezeko la idadi ya vijana pia anatarajia kukutana na Wasanii wa Kiafrika ikiwemo wale ambapo wapo kwenye playlist yake ili kuongea nao na kuona namna bora ya kuufikisha muziki wao kwenye masoko makubwa ya muziki Marekani.
photo-output-8-scaled.jpg
akija muulizeni kama anamjua hata mmoja
 
Huu uzi ni kuhusu mziki ila vinavyojadiliwa humu ni tofauti kabisa😂😂
 
Back
Top Bottom