Tatizo la mfumo wa Tanzania, hata uwe umesoma kiwango gani au fani muhimu kiasi gani, bila kuingia kwenye siasa, hujioni kama umefanikisha lolote la maana katika maisha yako.
Zakumi,
..there has to be a revolving door kati ya akademia, siasa, sekta binafsi, etc etc.
..haiwezekani tuwe na wahadhiri wa Political Science ambao hawajashiriki ktk harakati zozote za kisiasa, au hata kutoa ushauri kwa vyama vya siasa na wagombea.
..pia majaji wastaafu na mawakili wanaweza kuwa wahadhiri wazuri ktk idara za sheria ktk vyuo vyetu vikuu.
..tatizo letu ni kwamba hatusomeshi wataalamu wa kutosha. sasa akitokea mtu kama Sarungi kwenda kushiriki siasa basi watu wanaanza kulalamika kwamba utaalamu wake unapotea.
NB:
..katika wagombea wanaochuana kupata tiketi ya kum-challenge Obama, yumo Daktari.Ron Paul.
Nchi hii toka mashirika ya umma yafirisike na kuuzwa,kazi iliyobaki inayolipa ni siasa tu na ndio maana wabunge wanaongezewa posho kiulaini wakati waganga mabingwa hawalipwi haki zao!! That is Tanzania for you with your President being ridiculed by newspapers in europe as a beggar attending the DAVOS conference!!
Mkuu unajua tena simu za kichina. ni kweli nimechanganya. Vipi Rage bado anakuja hapo kijiweni? The Big Mayai vipi?
Kama sikosei kijiwe cha Saigon kimehama pale Sikukuu, huwa nawaona kina Hussein (Yanga) pale nyumba ya Bakhresa Narung'ombe na Livingston. Huyu Yanga, kwetu ni mtaa mmoja, wao pale Udoe, mimi Udoe na Lumumba marehem mdogo wake Shufaa, tumekuwa nae ingawa yeye alikuwa kidogo mdogo kwetu. Mkandara anawajuwa sana hawa, ananambia ndio ilikuwa mitaa yake.
Hapana, nyumba ya kona, inayopakana na CCM, kwa sasa linajengwa ghorofa.
Mwingine anaitwa Dr. Mohamed Tulli alikuwa anafundisha Kuwait. Toto la Kariakoo.
Sioni la kumlaumu Dr. Bilali hapa kwani hata mwanasayansi anahitaji ku-survive. Mfumo tulio nao unadiscourage wataalam na haswa wanasayansi kuendeleza fani zao kwani maslahi yao yanakandamizwa na hutegemea huruma za wanasiasa ili waishi. Ndiyo maana tunashuhudia wengi wakichangamkia siasa na kuacha uzalishaji na utendaji ambao ungeweza kulinasua taifa kiuchumi na kitekinolojia. Katika hali ya kawaida ingeshangaza kuona maprofesa wakiacha kufundisha na kwenda kugombea ubunge ili wakasinzie tu Bungeni lakini wajaze mifuko na wanenepe kama wengine. Baadhi wenye roho ngumu wameamua kwenda kufanyia kazi nje ya nchi ambako fani za sayansi zinaheshimiwa na kulipa. Kwa mtindo huu Tanzania na labda nchi za kiafrika zitabaki duni kiteknolojia milele.Tatizo la mfumo wa Tanzania, hata uwe umesoma kiwango gani au fani muhimu kiasi gani, bila kuingia kwenye siasa, hujioni kama umefanikisha lolote la maana katika maisha yako.
sina pingamizi na elimu yake kuwa mwana sayansi wa nuklia , darasani watu husoma 1+1>2 lakini ukishatoka darasani unatakiwa uifanye 1+1 > 3 kama ulisoma kwa kupata cheti hii test ya nje ya darasa wala hutakuwa na umuhimu nao .
hili ndiyo tatizo kubwa la wasomi wa Tanzania wanavyeti lakini kazi hawawezi ,kila sababu wanatowa ,mitaji , uongozi mbaya , bla bla . bla na kibaya zaidi huwawanataka kuwa viongozi wa juu ukiuliza yeye ni profesa , Dr , hebu tujiulize huyu mheshimiwa kama kasoma hiyo fani ambayo sina wasi wasi naye ,jee kaelewa ?? hapa ndiyo mbinde , huyu mheshimiwa anacheti cha kupamba ukuta tuu lakini hana uwezo wakuwa mwanasayansi , ametaka kusoma kuwa ili afike hapo alipo , ninasema hivi kwasababu ninauhakika , TANZANIA tumegunduwa URANIUM wakati mheshima yuko chuo na tukiwa gizani , ameingia madarakani tukiwa gizani atakufa atatuacha gizani na hapo ndiyo yeye atakwenda kuishi gizani huko futi sita chini ,
ANGELIKUWA ANIIJUWA FANI VIZURI BASI TUNGELIKUWA TUMESHAPATA UMEME WA BEI YA CHINI NA KUUZA EAST AFRICA NZIMA , KWENYE MITI HAKUNA WAJENZI
Sioni la kumlaumu Dr. Bilali hapa kwani hata mwanasayansi anahitaji ku-survive. Mfumo tulio nao unadiscourage wataalam na haswa wanasayansi kuendeleza fani zao kwani maslahi yao yanakandamizwa na hutegemea huruma za wanasiasa ili waishi. Ndiyo maana tunashuhudia wengi wakichangamkia siasa na kuacha uzalishaji na utendaji ambao ungeweza kulinasua taifa kiuchumi na kitekinolojia. Katika hali ya kawaida ingeshangaza kuona maprofesa wakiacha kufundisha na kwenda kugombea ubunge ili wakasinzie tu Bungeni lakini wajaze mifuko na wanenepe kama wengine. Baadhi wenye roho ngumu wameamua kwenda kufanyia kazi nje ya nchi ambako fani za sayansi zinaheshimiwa na kulipa. Kwa mtindo huu Tanzania na labda nchi za kiafrika zitabaki duni kiteknolojia milele.